Lema apewa chopa kujenga Chadema

Lema apewa chopa kujenga Chadema

Hongera sana Lema, hiyo ndiyo kazi saizi yako. Ubunge ulikuwa haukufai, kukupa ubunge wananchi wa Arusha waliku overdose.

Hawaku mu- overdose bali walimu-under utilize; Ni masahihisho kidogo tu mkuu naona kiingereza kidogo unachanganya misamiati ya kulia unapeleka kushoto na ya kushoto unapeleka nyuma.
 
Tunashuhudia upotevu wa MABILIONI ya pesa za wananchi kwa kumtengenezea LEMA ajira!
Hii ni hatari sana kwa taifa.
Kama katemwa ubunge apumzike mbona wengine hatuna job na tunasurvive?

Wewe na akili yako ndogo ndio hatari kwa taifa. Umetemwa job unapumzika. Hulipi kodi halafu unalalamika pesa za wananchi zinapotea. Tafuta kazi kwanza ndio uwe na haki ya kuzungumza. Unategemea kodi za wanaume wenzako zikujengee barabara na mahospitali. Shame on you.
 
ccm hawakuelewa wanamuongezea huyu jamaa umaarufu sasa hili pigo lake watajutia maisha yao yoteee. nchi nzima ishamjua lema wamemlainishia njia yake ya kuzambaza injili ya CdmTanzania..kazi ipo magamba leteni nyingine tuwazike.
piiiiipoooooooooooooooooziiiiiiiiii
Lema mwenyewe akiitamkaga hyo salamu utaipendaaaaaaaaaaaaaa
Gooooooooooooooo Broda ts tym we turn pages finish chapters and exchange the books

Lema bado ni jembe la Tanzania,watake wasitake.
 
Sasa hivi utamskia msemaji wa jeshi la polisi au JWTZ anasema chopa za vyama vya siasa marufuku. Zinaziba rada yao kipindi hiki wanapomulika Al-shaabab!

Nimeipenda. na inawezekana hio hawaeleweki hawa magamba.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Huwezi kujenga chama kwa Chopa ni matumizi mabaya ya pesa kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya chama hakina ofisi mikoani hata makao makuu hali sio nzuri...mnawachangisha pesa wananchi halafu mnamkodishia Lema Chopa.

Tuwe wakweli hivi Lema ana Influence gani kwenye siasa za Tanzania?

Siasa za Lema ni sehemu za kaskazini maeneo ya Arusha, Kilimanjaro.

Teh teh teh, GAMBAGUMU, na bado sana, nyi'mnatumia sh.ngapi kununua watu waje ktk mihadhara yenu mkuu, ya ngonsweeeeeee?
 
Hongera sana Lema, hiyo ndiyo kazi saizi yako. Ubunge ulikuwa haukufai, kukupa ubunge wananchi wa Arusha waliku overdose.
Pole sana kwa upeo wako mdogo wa kuona mambo yajayo RAJEO. kwa taarifa yako hili jembe linaandaliwa kuwa mgombea mwenza wa Dr. SLAA 2015 . Habari ndiyo hiyo CDM wako focused sana kumbuka operation sangara inavyowatesa hadi mnaigwa mawe kila mlikoenda kujisafisha. CCM endeleeni kulala wenzenu ndio kwaaaza kazi imeanza siku mkija kukumbuka shuka tayari kumekucha. Safari hii msishangae mkimwagiwa kinyesi mtakapoenda kujinadi maeneo ambayo mpigania haki za wanyonge atapokuwa amepita akiwajuza wananchi mabaya ya ccm pamoja na serikali yake. Kila la heri LEMA kaza buti.
 
Huwezi kujenga chama kwa Chopa ni matumizi mabaya ya pesa kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya chama hakina ofisi mikoani hata makao makuu hali sio nzuri...mnawachangisha pesa wananchi halafu mnamkodishia Lema Chopa.

Tuwe wakweli hivi Lema ana Influence gani kwenye siasa za Tanzania?

Siasa za Lema ni sehemu za kaskazini maeneo ya Arusha, Kilimanjaro.

Ila utajenga kwa EPA,RICHMOND,KIWIRA,DEEPGREEN,TICS,MEREMETA na KAMPUNI IKULU,WIZI WA KURA,KURITHISHANA MADARAKA,KUUZA NYUMBA ZOTE ZA SERIKALI,KUWEKEANA SUMU! USITUFANYE WAJINGA SASA HIVI TUNAJUA KILA KITU!ENZI ZA UJINGA ZIMEPITWA NA WAKATI HII NI GENERATION MPYA!

Ruvuma tunamsubiri kwa hamu sana! hadithi za Mgamba hatusikilizi,hamna cha kaskazini wala nini huo ni uzushi wako wa CCM, na bado utazusha mengi tu!ulishau kuchoomeka na Udini! LEMA NJOOOOOOOOOOOOO RUVUMA! NYINYI CDM NDIYO MNAJARI MATATIZO YETU WATU MASKINI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hawaku mu- overdose bali walimu-under utilize; Ni masahihisho kidogo tu mkuu naona kiingereza kidogo unachanganya misamiati ya kulia unapeleka kushoto na ya kushoto unapeleka nyuma.
Hicho nilichoandika ndicho sahihi....usitake niamini unachoamini wewe, tuone kama hiyo kazi ya kuzunguka nchi nzima itamuwezesha kulipa ile mikopo yake yote!!!
 
Pole sana kwa upeo wako mdogo wa kuona mambo yajayo RAJEO. kwa taarifa yako hili jembe linaandaliwa kuwa mgombea mwenza wa Dr. SLAA 2015 . Habari ndiyo hiyo CDM wako focused sana kumbuka operation sangara inavyowatesa hadi mnaigwa mawe kila mlikoenda kujisafisha. CCM endeleeni kulala wenzenu ndio kwaaaza kazi imeanza siku mkija kukumbuka shuka tayari kumekucha. Safari hii msishangae mkimwagiwa kinyesi mtakapoenda kujinadi maeneo ambayo mpigania haki za wanyonge atapokuwa amepita akiwajuza wananchi mabaya ya ccm pamoja na serikali yake. Kila la heri LEMA kaza buti.
Atakuwa mgombea mwenza wa pili kwa ukilaza katika historia ya Tanzania. Wakwanza alikuwa yule wa CDM wa 2010!!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.

“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.

Gazeti la Nipashe.

Tunarudi Enzi zileeee za kupigania Uhuru
 
Hicho nilichoandika ndicho sahihi....usitake niamini unachoamini wewe, tuone kama hiyo kazi ya kuzunguka nchi nzima itamuwezesha kulipa ile mikopo yake yote!!!

Mkuu cjawahi kuona mtu roho ngumu na mbaya kama yako toka nizaliwe '86!una roho mbaya kama Mkapa,
 
a. Lema ni mchagga na Mbowe ni mchaga lazima walinde ajira ya mwenzao

b. Kila la heri Lema kwa kupata perdiems na kusafisha macho kusafiri katika anga..

c. Je ni kikao rasmi cha chama kimeamua hayo? if that is the case, then chama kiko kwenye serious problem..

Mbowe usikatishwe tamaa na wanyonyaji hao! watuambie kwanza richmond ni yanani? EPA,TICS,MEREMETA,SUMU na Uchafu wa kila aina wanaofanya kwanza! hayo mambo ya Ukabila hayana tija kwetu,sisi tunaona nia nzuri ya CDM Kwa taifa letu na wala hatusikilizi na wala mimi siyo Mchaga na chadema si chama cha Kichaga kama mnavyopiga propaganda za Kijinga tu,Mmechelewa it is too late hatudanganywi tena! LEMA zunguka na tutachangia hata hizo Gharama,hata Mwl tuliambiwa kwamba alichangiwa na maskini kama sisi wakati wa kudai uhuru wetu na yeye ndiyo mfano wetu,wengine mnatumia nembo ya chama alichoanzisha wakati wezi wakubwa na wanyonyaji! Tuanibiwa Madini mko kimya kimya,wanyama wanaibwa mko kimya du! sijaona watu hamna huruma kiasi hiki! watu wanakufa na njaa,shule mbovu,maskini wanazidi kuwa maskini,Hospital za hovyo! wewe huna hata huruma na Watanzania wenzako maskini kule vijijini!
 
Kamanda lema,tafadhali,ukija hapa kilombero njoo na makamanda wengine kama wawili,hapa napendekeza mwenyekiti Freeman Mbowe. Marehemu Regia (RIP) Alifanya kazi kubwa ya kukijenga chama, Kiukweli hapa kuna ccm masalia. Ila kazi haitakuwa kubwa ni kiasi cha kufanya brain wash tu. Njoo mkuu. Hutaamini mtakavyopata mapokezi.
 
Kweli CDM maamuzi hufanywa na watu wa kaskazini kwa manufaa yao;
1.Walianza kwa Dr. Slaa 12 milioni Tshs. kwa mwezi baada ya kukosa urais
2. Sasa Lema amepewa ulaji wa kula ruzuku ya chama kisingizio akaeneza chama ukanda wa Pwani

HUU NI UFISADI!!!!
MAFILIFILI, umeliona hilo eeh,
Hatari sana kwa kweli pesa za walalahoi zinatafunwa inasikitisha sana aisee!
 
ccm kweli ni wagonjwa wa akili.
tanzania nzima ilkuwa yao leo wanajisifia kwa kutetea kata,halafu mbaya zaidi wanajua mshikemshike wa chadema ukianza unavyo waacha uchi.mf=
operesheni sangara.
orodha ya mafisadi mwembeyanga.
maandamano,nk

hawa akina rejao na vibaraka wenzao huku wanapiga domo wakati nape,mukama na mwenyekiti wao hawalali.

TUWAPUUZE TUSONGE MBELETHE FREEDOM IS COMING TOMOROW
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.

“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.
Yaani magamba watajuta, bora wangemuacha bungeni, hizo Ari atakazo ziamsha lazima ccm kingoke 2015.
Gazeti la Nipashe.

Aminia kamanda Lema waonyeshe hao magamba kwamba peoples ni makini. Naomba hili zoezi liambatane na kuwapatia wananchi elimu kuhusu katiba ya sasa na mabadiliko ya kuweza kupata katiba nzuri. ili tuweze kupata Katiba nzuri ya Tanzania na hatimae kuwaondoa magamba 2015
 
Back
Top Bottom