Lema apewa chopa kujenga Chadema

Lema apewa chopa kujenga Chadema

lema kipaumbele iwe tanga,pemba,unguja,mtwara,lindi,tabora,pwani,morogoro,upareni,kagera,manyara zingatia haya maeneo
 
kama kuwapa wananchi elimu ni kupoteza fedha, mbona huwaoni ccm wanavyotafuna pesa za walalahoi huku wakieneza propaganda na kushindwa kutimiza ahadi zao kwa wananchi, na inapo fika kipindi cha uchaguzi wanaishia kutukana badala ya kusema walichofanya. lakini sishangai kwa sababu kama hawajafanya kitu kuna nini cha kusema zaidi ya kutukana. Taifa linaangamia, rasilimali za nchi zinaporwa, fedha za umma zinafujwa. Wewe unaona kuelimisha watanzania kuhusu nchi yao ni ufujaji wa hela, acha watanzania wajue ukweli kuhusu serikali yao na wajue uhuni wanaofanyiwa na kinachosababisha hali ngumu ya maisha wanayoyapata kila siku.

Ebu fikiria tu? mpaka wageni wataalamu wa uchumi wanatushangaa ndani ya mwaka mmoja kutoka 1200/= hadi 2500/=. kuna nchi hawana ardhi nzuri kama yakwetu lakini mfumuko wa bei hauko hivi.

Huchoki viongozi ambao kazi wanayojua ni kupiga "DOMO" ?
 
As long as lengo n kujenga chama, thats g'd idea...kikubwa kwenye huo msafara, wasisahau 'magwanda' kwa ajl ya promo na CD za a.k.a Mr.Mitusi...ili magamba wote wasikie viongozi wao wakimwaga sera!
 
Lema for presicency 2015?..... No, No I am just dreaming...
 
Asanteeeeeeeeeeee! !!!!!!!!!

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.

“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.

Gazeti la Nipashe.
 
Umeingia choo cha kike; CDM siri zao anazo Mheshimiwa Lusinde!!! Ama wewe ni mfuasi wa Waziri Mkuu wa Uingereza??
Mbona baada ya kusikia Lema atazunguka nchi nzima vibaraka wa CCM mmekuja kwa kasi kubwa? Hofu yenu ni nini kama jambo hilo halina manufaa kwa CDM? Kwa taarifa yenu uamuzi huu wa Lema kuzuru nchi nzima ni jeraha kubwa kwa CCM.Kama hamuamini subirini muone
 
Kamanda Lema Tunakutakia kila la kheri ktk kukistawisha Chama Chetu,naamini hakika kazii hii utaimudu vizuri.
 
Tuwe wakweli hivi Lema ana Influence gani kwenye siasa za Tanzania?

Siasa za Lema ni sehemu za kaskazini maeneo ya Arusha, Kilimanjaro.
Ngoja aanze kazi ndo tutajua ana mvuto Tanzania au hana., Maneno yako ni invalid kwa sasa.
 
Atakuwa mgombea mwenza wa pili kwa ukilaza katika historia ya Tanzania. Wakwanza alikuwa yule wa CDM wa 2010!!
Kukaaleki RAJEO akili yako imevia/dumaa kama kidevu chako!!!! unaposema kilaza unamaanisha nini??. watanzania hatuhitaji viongozi lege lege waliopambwa na doctorate za heshima lakini wanasaini mikataba bila kuisoma wanawaangalia wezi wa mali za umma bila kuwakemea.

Ni bora tukaongozwa na mtu mwenye elimu ndogo lakini anayeweza kutoa amri ikatekelezwa, anayetoa ahadi ikatekelezwa, anayeweza kuwapeleka mafisadi na wezi wa mali za umma magerezani bila kujali urafiki uliopo baina yake na muhusika. This is my take kama wewe unahita semina elekezi ili kuutambua ukweli huu basi subiri muda ufike maana semina hiyo itaendeshwa kwenye magereza ya kilimo na itaambatana na kazi ngumu.
 
Uamuzi mbovu, matumizi mabaya ya rasilimali. Mbaya zaidi kazi anapewa kilaza asiyekwena shule aifanye.

Kwa mwendo huu, hivi mkiona chama kinaporomoka au kufa mtashangaa??

Mkuu kwenye CDM usizungumzie swala la shule,sio muhimu maadam unatokea kaskazini, na pili kama uko dini rasmi ya chama,elimu sio tatizo. Unataka Lema ashawishike kwenda shule aige mfano wa nani,kama viongozi wake ni hawa: Mbowe, Slaa, Mnyika..
 
Huwezi kujenga chama kwa Chopa ni matumizi mabaya ya pesa kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya chama hakina ofisi mikoani hata makao makuu hali sio nzuri...mnawachangisha pesa wananchi halafu mnamkodishia Lema Chopa.

Tuwe wakweli hivi Lema ana Influence gani kwenye siasa za Tanzania?

Siasa za Lema ni sehemu za kaskazini maeneo ya Arusha, Kilimanjaro.

Ritz utasema yote ila ukweli utabaki daima kuwa Lema ni jembe hata kama hutaki! Tatizo umemjua Lema mwaka jana baada ya kuwa mbunge ila ukitaka kumjua vizuri muulize Ba Riz! Bora kukosa ofs ila ukajenga chama kuliko kuwa na ofs nzuri na chama bovu ka Magamba. Chama ni watu wala si ofs!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempatia aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, helikopta na vifaa vingine kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho, wakati huu ambapo anasubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa kuhusu kuenguliwa ubunge wake.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu Dodoma jana.

“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.

“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.

Gazeti la Nipashe.

Sababu za kinteligesia zitatumika kuzuia mikutano yake...wameanza na dom.stay tune
 
Mkuu kwenye CDM usizungumzie swala la shule,sio muhimu maadam unatokea kaskazini, na pili kama uko dini rasmi ya chama,elimu sio tatizo. Unataka Lema ashawishike kwenda shule aige mfano wa nani,kama viongozi wake ni hawa: Mbowe, Slaa, Mnyika..

Lusinde na maji marefu hapo vipi?
 
Kilichoipata CCM baada ya kumfukuza Zitto bungeni,ndicho kitakachoipata CCM baada ya kutengua ubunge wa Lema.
 
Sasa hivi utamskia msemaji wa jeshi la polisi au JWTZ anasema chopa za vyama vya siasa marufuku. Zinaziba rada yao kipindi hiki wanapomulika Al-shaabab!
kaka hii nimeipenda,kweli haya magamba yakiona hewa imechafuka,wanaweza kuja na mkakati huu!!
 
Huwezi kujenga chama kwa Chopa ni matumizi mabaya ya pesa kuna mambo mengi ya msingi ya kufanya chama hakina ofisi mikoani hata makao makuu hali sio nzuri...mnawachangisha pesa wananchi halafu mnamkodishia Lema Chopa.

Tuwe wakweli hivi Lema ana Influence gani kwenye siasa za Tanzania?

Siasa za Lema ni sehemu za kaskazini maeneo ya Arusha, Kilimanjaro.

magamba yameanza kuwawasha,
 
Back
Top Bottom