LEMA anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa faida ya nani?!

Status
Not open for further replies.
hatuhitaji machizi kama yeye, wewe kama una hamu sana na lema kaanzisheni nchi yenu ya machizi, hukoo baharini

Nimetoka kwenye ban aliyonisababishia mtu mwenye magonjwa mengi humu jamvini! sasa huyu tahahira anataka nirudi huko! unawaitaje wenzako machizi? MOD be fair! kabla sijatoka ngoja nikwambie. SELUROPE YOU!
 
Linalonishangaza ni kuwa sijaona chochote kibaya alichokifanya lema.
Pia sijaona lolote la maana alilofanya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Sikubaliani pia na wanafunzi walivyo behave alipokuja mkuu wa mkoa, ila nao ni watu wazima na wana uhuru wa kutoa hisia zao.
Combination ya wanafunzi kuwa na munkari na kuanza kuzomea na ulimbukeni wa mkuu wa mkoa ndiyo vilivyofanya Lema akamatwe na hizo pande zote mbili naweza kuzilinganisha na wendawazimu wenye munkari usio na maana yeyote.

Mwisho kabisa, ili kupata haki zako, ukiitwa polisi au hata kusikia tetesi kuwa unatafutwa na polisi, ni bora uende kituoni na mwanasheria wako kama utaweza kuwa naye. Sijui ni nani huwa anawashauri viongozi wa CDM (mfano Mbowe) kuwa kwa kukimbiakimbia mapolisi somehow kesi itapotea ..... thats a very stupid habit.
 
Lema MMoja tu vyombo vyote vya dola vinatunga mpango wa namna ya kumkaba koo,ona alivyomwadhili mulongo kamvua nguo mpaka mwenyekiti wa CCM Arusha anamwambia afungue chuo hiyo ni messaji kubwa sana manake mullongo ameamua maamuzi ya kipuzi

Mkuu ni jambo gumu sana kudeal na kichaa, inahitajika muda na hata resources mpaka kumcontain, so serikali kama baba, inajaribu kumtibu kichaa chake mtoto wake mpendwa Lema, atapona tu
 
Godbless Jonathan Lema,hataishiwa matukio ya kukamatwa na kusimamishwa vikao vya Bunge. Hatamaliza shahidi zake kwa Spika. Lema 'si' mtanzania. Hana tabia za mtanzania za uoga,kujivuta,kutojiamini,kujipendekeza,kusema asichokiamini,na kusahau mapema. Yeye ana tabia kinyume na hizo. Kwahiyo, hataishiwa safari za polisi,mahakamani na nje ya Bunge. Ina heri nchi hii yenye LEMA mmoja!

Utawala wa mabavu si suluhisho la amani. Ni tatizo kubwa kudhani "repression" ni kuonesha nchi inatawalika.
 
Linalonishangaza ni kuwa sijaona chochote kibaya alichokifanya lema.
Pia sijaona lolote la maana alilofanya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Sikubaliani pia na wanafunzi walivyo behave alipokuja mkuu wa mkoa, ila nao ni watu wazima na wana uhuru wa kutoa hisia zao.
Combination ya wanafunzi kuwa na munkari na kuanza kuzomea na ulimbukeni wa mkuu wa mkoa ndiyo vilivyofanya Lema akamatwe na hizo pande zote mbili naweza kuzilinganisha na wendawazimu wenye munkari usio na maana yeyote.

Mwisho kabisa, ili kupata haki zako, ukiitwa polisi au hata kusikia tetesi kuwa unatafutwa na polisi, ni bora uende kituoni na mwanasheria wako kama utaweza kuwa naye. Sijui ni nani huwa anawashauri viongozi wa CDM (mfano Mbowe) kuwa kwa kukimbiakimbia mapolisi somehow kesi itapotea ..... thats a very stupid habit.
kama hujaona tatizo la lema, utakua na tabia kama zake, either ganja kwa sana au viroba mkuu
 
Nimetoka kwenye ban aliyonisababishia mtu mwenye magonjwa mengi humu jamvini! sasa huyu tahahira anataka nirudi huko! unawaitaje wenzako machizi? MOD be fair! kabla sijatoka ngoja nikwambie. SELUROPE YOU!

nimewahi kuwahudumia vichaa wengi tu, so ninaweza kuishi na wewe pia, haya mkuu kalale sasa umefanya kazi kubwa sana leo, big up
 
Kwani kunatatizo gani kutafuta umaarufu wa kiasiasa? Ni nani kwa mafikirio yako ni gwiji kwenye siasa pasipo kuwa maarufu? Umaarufu katika siasa ni credit kwa mwanasiasa hai. Haya mawazo yako ni udhihirisho wa effect of socialism ya Nyerere in your blood.


Kule Hollywood people are dying to become popular, for either good or bad popularity , it doesnt matter.

Popularity is very important! Swala hapa ni hoja ya msingi wa mgogoro huu na kama kuna amicable solution iliyofikiwa. Swala la mivutano ya Lema na mkuu wa mkoa ni swala la kiutendaji zaidi, mkuu wa mkoa kama mtendaji na Lema kama mwakilishi wa wananchi, Lema hatakiwi kuside na mkuu wa mkoa, na kama ni kuside na mkuu wa mkoa basi afanye hivyo only on principle, siyo kwa kujipendekeza!!

kule ni hollywood wale ni wasanii na hapa hatujadili wasanii tuna jadili anacho kifanya lema:
hakuna jimbo,nchi yeyote duniani ambayo inachagua viongozi wake ili waje kujitafutia umaarufu unless anakua amewafanyia wananchi wake kazi waliyo mtuma kuifanya.lakini ukijaribu kumuangalia lema BUNGENI hayupo kwanini?ni kutokana na vurugu zake za ajabu ajabu ukijaribu kuangalia mikutano na vikao vyote vya bunge vilivyo kaa tangu achaguliwe vinahesabika!
NINI MAANA YAKE??
.HUYO NI KIONGOZI WA KULIONGOZA JIMBO KAMA ARUSHA MJINI'???
 
TAHADHALI IKIKUKWAZA ACHANA NAYO.

Wakuu habri ya Sikukuu?,natumaini hamjambo wote,kwa wale wagonjwa poleni mungu atawasaidia mtapona. Kwa muda mrefu nimekuwa nafuatilia siasa za Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema,na kujiuliza maswali mengi mengine nimejkuwa sipati majibu hata kidogo.

Tafadhalini naomba tujadili hili kwa uungwana mkubwa ili tusije tukaondoa maana halisi ya maudhui yangu,Tangu kuingia kwake madarakani Arusha hakujatulia,kila siku ni migogoro na vurugu ambazo mwisho wake ni lazima mtu apotee maisha!. Kwa wale wenye kumbukumbu sahihi mtakubaliana na mimi kwamba katika uongozi wake watu si chini ya wanne wamekwishapoteza maisha kutokana na vurugu,sitaki kuingia kwa undani juu ya hili lakini kwa wale wenye kumbukumbu nadhani mnalitambua.

Ni huyu huyu Lema ambaye amejikuta mara kadhaa akitolewa Bungeni kama si kukwazana na viongozi kadhaa ndani ya Bunge kutokana na maneno yake kadha wa kadha haijalishi iwe kweli ama si kweli,lakini yametokea!. Mara nyingi nimekuwa pia nikufuatilia kauli zake kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara,ukisikiliza kwa makini uangundua kwamba Lema ni Mtata,ni mtu ambaye anaonekana kukata tamaa ya maisha na sasa kujaribu kutumia njia za mkato ikiwemo jazba kutafuta ufumbuzi.

Nimemsikia mara nyingi sana akithibitisha kwamba hapndi kuonewa na pale anapobaini kwamba anataka ama ameonewa basi ni lazima asimame kidete kujitetea ama kutetea haki yake,hili ni jambo ni sahihi na namuunga mkono,lakini tunatofautiana katika kuidai hii haki,yeye anatumia nguvu kubwa zaidi. Kuna viongozi wengi sana ambao ukiwatizama wamefanya mambo makubwa na mazito katika kuhakikisha kwamba wanajitetea ama kuwatetea na wengine ama wale wanaowaongoza,lakini wamekuwa wakitumia hoja ambazo mwisho wa siku zinaleta mana halisi.

Kwa mfano yupo JOHN MNYIKA,ZITTO KABWE,DK.SLAA,HALIMA MDEE,na wengineo wengi wa leo,jana na juzi,lakini hatuawahi kusikia vurugu kwenye maeneo yao wala watu kuuawa,nilitegemea kwamba Baada ya Lema kurudi Bungeni na kwa sababu amekiangusha chama kikubwa kama CCM angetulia na kujaribu kuwaonyesha watanzania kwamba yeye ni mtu wa namna gani katika nchi hii,lakini matarajio yangu yamekuwa tofauti.

Ndiyo mana nashawishika kuamini kwamba pengine Lema anatafuta umaarufu kutokana na hivi vituko vyake vya kila siku!,lakini ni vituko ambavyo vinaanza sasa kumfanya adharaulike katika jamii,kwa sababu watu wanaanza kuzoea kwamba LEMA ni wa vurugu. Ombi langu kama Lema atatoka na kurejea tena mitaani,kuna haja ya viongozi wa CHADEMA kukutana nae na kujaribu kuzungumza nae,mbona wenzake wanakua na hoja na zinapenya na kupokelewa vizuri na jamii?!,kwa nini aisijifunze kwa wenzake.

Mwisho hakuna mtu anayependa kuonewa hapa Duniani,hata mtoto mdogo ambaye bado ananyonya akiona mama yake anamsumbua sana kwenye titi huwa anapiga ngumi ama kuficha na kupiga mateke kuashiria kwamba hapendezwi na yanayojitokeza.Narudia Lema akitoka salama Polisi na kurejea mitaani aachane na hizi vurugu akae na wananchi wake wafanya shughuli za maendeleo,naamini wameshaelewa madhumuni yake.

1. Hapa hujajenga hoja, unatoa hukumu bila kuwa na ushahidi.
2. Umesema kwamba Lema hataki kuonewa. Je, wewe ungetaka akubali kuonewa ili kusiwe na vurugu?
3. Je, unaweza kuthibitisha (kwa data na siyo kubuni kichwani) kwamba vurugu hizo anayezisababisha ni Lema?
4. Nadhani sisi Watanzania tunaweza kuwa na tatizo kwa jinsi tunavyochambua mambo. Hatuna "critical mind" - hatuwezi kuangalia tukio objectively. We are too subjective na hivyo tunashindwa kuona chanzo cha tatizo ni nini na tunakalia kulalamikia matokeo yake. Unachojaribu kueleza hapa ni matokeo ya tatizo na siyo chanzo chake, my dear!
 
mkuu labda ungejaribu kutufanya tukuelewe, anajiitafutia umaarufu kivipi? jaribu kurelate yanayotokea na uhusika wake..
Ukianzia baada ya uchaguzi,
usitake kusema kuwa lema ndiyo aliwaambia wale makada wa CCM waende, mahakamani illi ashinde na awe maarufu..

Tukio jingine ni lile la kukataa Meya, Usitake kutuambia Lema ndiyo Mwanzilishi na Alipanga matokeo yawe vile ili waandamane,

Na unadhani tukio la kuuwawa kwa mwanachuo ni mpango wa Lema..

Hebu Jaribu kucompare yote yanayotokea na Uhusika wa Lema, Picha unayojaribu Kuchora
haieleweki kwa watuu wenye akili..
Matukio Wanayatengeza wao wenyewe MACCM!
Time will Tell...

Tatizo tunaingiza siasa vyuoni,kwani mauaji haya yanahusiana vipi na CCM? Na kama wanayatengeza CCM kilichompeleka

Mb.kwenye mauaji yasiyomhusu kama mtego kwake ni nini? Na kama wameyatengeneza CCM,je CDM ndio watatuzi wa

matatizo haya kupitia Mb. huyo?Na kama ndivyo,je alitoa mchango gani wenye mashiko kwenye utatuzi wa suala lile?

Kwa mwenye utimamu wa akili wa hali ya juu na kusoma alama za nyakati hakukuwa na

umuhimu wowote wa MB. kuhudhulia mkusanyiko ule.

Ni vema wabunge wetu vijana wakawa na washauri wazee au kuwatumia viongozi wa dini kwa ushauri na nasaha za

namna ya kuishi kama kioo cha jamii.
 
Mkuu ni jambo gumu sana kudeal na kichaa, inahitajika muda na hata resources mpaka kumcontain, so serikali kama baba, inajaribu kumtibu kichaa chake mtoto wake mpendwa Lema, atapona tu

Na ni mbaya sana kudhani asiyetaka kuonewa ni kichaa. Utumiaji wa mabavu hautailetea nchi yetu amani. Utawajengea watu wetu usugu. Suluhisho la mambo yote ni vyombo vya usalama kufanya kazi kwa weledi bila kumwonea mtu kwa maslahi ya kisiasa na pia kuwa sawa mbele ya sheria. Baadhi ya watu wakiwa juu ya sheria na wengine chini ya sheria itatuletea matatizo. Si unaona magari yenye ST, SU, PT, JW kwenye foleni yanatanuwa na yanapotanuwa hata madereva wengine nao wanatanuwa? Kwa nini? Kwa sababu wanasema: kama hawa wanaotuonesha utii wa sheria bila shuruti wanafanya haya sisi tufanye yapi? So, solution ni wote kutii sheria, wote kuheshimiana, wote kufanya kazi zetu kwa weledi na tukifanya hivyo kila kitu kitaenda vizuri. Change of mind leads to change of attitude and behaviour.
 
Mkuu kwani zanzibari tu ndio kuna bahari, jiografia ulipata ngapi mkuu au ndio hukwenda shule kabisa, itakua ulifeli sana jiografia, pole
Jiografia uliyopasi wewe ndio ilikufundisha watu kuanzisha nchi baharani?......FYI nilipata B O level mwaka 1979 na A ya A level...sijui hata kama ulikuwa umezaliwa
 
My asumptions
1.LEMA ANAENDESHWA NA NGUVU YA BANGI.
2. LEMA ANATAKA KUICHAFUA SERIKALI IONEKANE UTENDAJI WAKE WA KAZI NI MBOVU NA ILI WANANCHI WAICHUKIE HUU NI MUENDELEZO WA SIASA CHAFU ZA CHADEMA.
3.LEMA ANATAKA KUWAAMINISHI WATANZANIA KUWA YEYE NI FIGHT WAKATI UHALISIA WAKE NI MCHUMIA TUMBO.
4. LEMA ANAKIPIGIA KAMPENI CHADEMA BAADA YA HARAKATI ZA M4C KUDOROLA KWA KUDHARAULIWA NA WANANCHI PAMOJA NA MBINU NYINGINE WANAZOTUMIA CDM KUGONGA MWAMBA.
Ninachokishuhudia kwa sasa ni anguko la hali ya juu la kisiasa kwa LEMA.

Hizo assumption zimejengwa kulingana na kiwango cha uelewa finyu ulionao na jinsi ulivyopumbazwa na hao waliokupa kibarua cha kujishikiza
 
Utawala wa mabavu si suluhisho la amani. Ni tatizo kubwa kudhani "repression" ni kuonesha nchi inatawalika.

Tatizo tunalazimisha mambo bila utaratibu na kujiweka juu ya sheria kupita kiasi na inapobainika uhusika wetu katika matukio tunaanza lalamika eti utawala wa mabavu ilihali tulishindwa kutumia akili kuudhibiti.

Ndugu yangu linda heshima yako na ya mwenzako kwa kufanya hivyo utapata hekima itakayo kuweka huru kwani hapa duniani ni mahala pa kupita tu.Kilicho kikubwa ni kuacha jamii isiyo na hofu,mashaka,woga,dhalau,kibuli na mambo mengine yanayoashiria utovu wa nidhamu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom