Lema ametengua kitendawili cha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema ametengua kitendawili cha polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Nov 3, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watawala wajinga huamini silaha ni nyenzo ya kazi kwa ajili ya kuogopesha, katika hali hiyo hiyo ya ukungu katika ubongo wao hudhani magereza ni tishio ambalo hakuna mwanadamu yuko tayari kukubali kwenda kuishi kwa amani na kwa furaha. Msimamo huu wa serikali dhalimu zote duniani na kwa kuwatumia polisi na vyombo vya usalama katika nchi hukwama pale wanapowapata wanadamu kama mahatima gandhi, madela, steve beko na sasa lema wa tanzania na wengineo wengi. Mheshimiwa godbless lema kawambia serikali ya tanzania na vyombo vyake vya usalama kuwa kama anapata nafasi ya kuchagua kifo na kuishi, ili watanzania na wanaarusha wakombolewa atachagua kifo, kama anapata nafasi ya kuchagua kuishi jela maisha yake yote ili wananchi wake wapate amani na uhuru wa kweli atachagua kwenda magereza na amefanya hivyo kwa vitendo.

  Sote tunatambua kuwa bunduki za polishi, mbwa wa polisi, maji washa, mabomu ya machozi yanaletwa na kutumiwa kwa ajili ya ulinzi na usalama wa wananchi na kuwaadhibu wale walioshindwa kukidhi matakwa ya amani kwa tafsiri ya katiba si vinginevyo.
  Magereza yyanajengwa kuwatunza wakosaji sasa inapotokea vyombo hivi vinakuwa tishia toto serikali na vyombo vyake vya ulinzi wamejikwaa na kuangukia pua. Tunayokila sababu ya kujua kuwa watu wengi walioko kule wengi wao wako kule kwa sababu ya kukithi matakwa ya watawala au watu waliokaribu na watawala au watu walikwisha tambuliwa kuwa ni walala hoi hawana mtetezi na muono huu ndiyo unakamilisha dhana ya tisha toto ambayo hutumiwa na polishi na serikali .

  Ipo siku watu hawa wote watakuwa na moyo wa lema magereza hayatatosha, askari hawatatosha, risasi hazitatosha wala magari ya maji washa. Polisi mnalijua hilo na kama hamlijui tazameni misri, tunisia, na sasa yanayotokea yemen na syria
   
 2. j

  jigoku JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kaka najua hawakubaliani na wewe wote wale ni sehemu ya matatizo ya nchi hii nami nakuunga mkono nimekuwa nikisema sana hapa jukwaani,unachosema mimi tayari nimeshaindaa familia yangu juu ya hli,maana naaminilitatokea na kama CCM wataendelea kudhani wana mbinu,wana akili sana,wana jeshi kubwa wana magereza mengi,wana silaha za kila aina na mpaka jeshi,amini amini nawaambieni hayo yote hayatafua dafu,labda kama wataamua nchi kuifanya jangwa sawa,lakini ukumbuke hawa ni binadamu hata wao wenye silaha watakinzana tu.mimi najua hilo jambo lipo tu linakuja,mimi binafsi nalisubiri kwa hamu bila kujali matokeo yake kwani hakuna mwenye kulipinga hili kama sio CCM kukubali kuacha udhalimu wao ndani ya hii nchi.na kinachowafanya waogope mabadiliko ni hofu yao ya kushitakiwa kwa makosa waliotutendea watanzania
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wewe huna familia bwana kula kulala wewe. Halafu wewe unachekesha sana yaani vita kisa eti Lema kajipeleka gerezani, hata kama wangeenda wote wakiwemo Mboye na SLaa hakuna kitu kama hicho. watanzania si wa kupelekwa kihivyo
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Could be wise unaongezea kule kwa mada ya Lema maana unayo yasema si mageni tungali endelea kule kule kaka .Wewe hujatoka shule za kata lakini inakuwaje unaonekana ulipitia shule hizo kwa tabia hii ?
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa. Unampamba Lema wakati tayari anaumia huko. Kama kweli unachungu kiasi hicho ungemuunga mkono na wewe uende gerezani. Usitudanganye kaka , nchi yetu ni amani. Nenda nchi za jirani ukae wiki moja urudi utasimulia uliyoyaona namna ambavyo haki za binadamu zinakiukwa . Tusiongee hapa kishabiki mambo yakishaharibika mnaondoka kwenda nchini mwenu tunajua ww si raia wa nchii sasa unataka mambo yaharibike ukimbilie kwenu huku watoto, wazee na akina mama wa Tanzania wakibaki wanateseka.
   
 6. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nadhani hujui maana ya amani wewe! Wananchi wanaokunywa maji wana amani? Wananchi wanaolala na njaa wana amani?
   
 7. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kweli wewe ni caputi kabisa, ni nchi gani unaongelea na unataka kuifananisha na viongozi wa Tanzania. Wewe ndio tunakushangaa, kwani walibya waliondoka wakamwacha Gadaffi wakati maneno ya Gadaffi yalikuwa kama hayo hayo ya kwako. Sasa tunakusubiri wewe uanze kukimbia, ukimbilie huko kwenye amani inayokufaa. Vitisho vyenu vya kuwatishia watanzania ndio vinaaga bye bye. Mh Lema anaroho ya ajabu sana, anadhamira ambayo ni wanasiasa wachache wanaweza kuwa nayo. Kitendo cha kuwakamata kamata na kuwanyanyasa wanaarusha eti kwa itikadi ya vyama na kutopenda kukosolewa huo ni kukandamiza demokrasia. Hata kama walifanya maandamano kikatiba ni haki yao kwa ajili ya kujenga eneo lao la Arusha. Polisi wangekuwa na utaratibu wa kufanya kazi kwa kushiriana na wanaarusha sio kukomoana. Polisi wangekuwa wanafanya kazi yao kwa haki ninadhani wanaarusha wasingekuwa na matatizo.
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Alichokifanya ni changamoto kwa Jeshi la poliis hususani IGP Mwema kuangalia utendaji wa Polisi arusha na as far as dhana ya polisi jamii is concerned. Ni ujumbe kwa Tanzania nzima juu ya tabia ya Polisi kujifanya miungu watu katika kubambikia watu makosa kwa kitisho cha jela na kuvuta mpunga
   
 9. IGUDUNG'WA

  IGUDUNG'WA JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 1,998
  Likes Received: 887
  Trophy Points: 280
  sir GOD ailinde TZ atuepushe na wadhalimu wa madaraka
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Masaburi kazi yake ni kukalia!
  Usiya misuse na kutumia kufikiri!
   
 11. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Heko LEMA!
  Nyayoooooo!
   
 12. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Wang'ayo, elewa unachokiandika humu JUKWAANI. Watu wamechoka na upumbavu na uonevu wa CCM, Kumbuka historia ya Tanganyika na hata Zanzibar yaliyotokea ndiyo yaliyotegemewa. Tanganyika Mwl. JK Nyerere aliacha ualimu na kuangukia kwenye siasa na kauli mbiu yake alikuwa UHURU NA KAZI, akapata misukosuko hadi kufikia kuwekwa kizuizini. Ndipo alipotumia lugha ya kuwadanganya wakoloni kuwa msipo tuachia nchi yetu (TANGANYIKA) tutawashitaki kwa Mungu. Kwa upande wa Zanzibar waarabu waligoma ndo maana mapinduzi yakatoke.

  Nimekupitisha kwenye kile kinachoitwa nchi yako, sasa kumbuka aliyeanzisha mapinduzi ya Tunisia alikuwa ni nani! pia nenda misri na kwingineko. Sasa mpambano ni Tanganyika yetu kubaki huru kutoka kwenye mikono ya mafisadi wanaojivua GAMBA, na kama na wewe umetumwa kutudanganya wa-JF umekwama....................... ​
   
 13. Josephine

  Josephine Verified User

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Woooooooooooo,jaribuni basi hata sasa kitaeleweka tu,watu wenyewe nchi imeshawashinda bora muipe jeshi tujue moja hatuna serikali.
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145


  Mpaka kama wang'ayo atakuwa hajaelewa ntamshangaa sana yeye na wenzake wano kurupuka nae wanadhani mapinduzi ni leo basi kesho yamekuwa lazima kupitia hali hii kwenye milima na mabonde ndio tufike tambarare na kwenye kivuli na kula matunda ya Uhuru kamili yeye hapo alipo anadhani ndio kapata Uhuru wala hafikili Celina Kombani alitaka kupitisha mswaada wa Katiba tena na Wang'ayo alitaka kutengwa hasihusishwe kujadili au kutoa maoni yake kwenye katiba yetu ambayo imejaaa nguvu ya Rais kila kipengele Rais yeye ni anateua kila kamati

  Vuguvugu lote hilii ni kupinga kwa kunyang'anywa dhuruma yetu ya Kikatiba na uhuru wetu wakujiamulia kisheria ila serikali yenyewe yataka kutu force tukubali itakvyo kwa matakwa yao hao viongozi
   
 15. M

  Mzee wa Posho Senior Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upuuuzi mtupu ngonjera tu,pelekeni huko ujinga wenu na Mbunge wenu kichaa
   
 16. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hehehe Yesu alijitoa tukombolewe hakika aliteswa sana na alielekea kukata tamaa ila sidhani kama kuna mwanadamu atakayeweza hilo la ukombozi kwa watanzania hapo ni maslahi tu!
  ukombozi ni sisi wenyewe kuanzia ngazi ya familia zetu kukataa kuonewa na kuunganisha nguvu ila siyo wakujitoa kwa maslahi ya cheo na fedha na biashara
   
Loading...