Lema alamba posho kikao cha madiwani Arusha!

Nyie msicheze na kitu inatwa hela, pesa, fedha!! Fedha fedheha jamani!! Posho ni mtego mbaya sana. Posho zitatugawa!!

Mbona Mods wameiondoa hii kwenye jukwaa la siasa? Jukwaa la siasa ndio mahala pake hii thread. Posho ni siasa na siasa ni posho!!
 
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kusaini na kuchukua posho ya kikao cha Baraza la Madiwani mwishoni mwa wiki, lakini akatetea uamuzi huo akisema alikwenda kuzima
njama za kufukuzana.

Lema na madiwani wenzake watatu wa Chadema, walishiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha, kinyume cha msimamo wao wa kutohudhuria vikao hivyo.

Mapema mwaka jana, Lema na madiwani wote wa Chadema wa Jiji la Arusha waliweka msimamo wa kutomtambua Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo na kutohudhuria vikao vyote vya Baraza la Madiwani kwa madai kuwa Meya huyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na kuhudhuria vikao ni kumtambua.

Lakini Ijumaa iliyopita, Lema na madiwani Isaya Doita (Ngarenaro), Crispin Tarimo (Sekei) na Sabina Francis (Viti Maalumu), walihudhuria kikao hicho na kupokea posho kwa malipo ya kuhudhuria kikao.

Lema alikiri alisaini posho hiyo yeye na wenzake na kudai kulikuwa na njama za kutaka kuwafukuza madiwani wa Chadema kwa kukosa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila ya kuwa na taarifa yoyote na kwa mujibu wa sheria na kanuni wangetimuliwa.

Alisema kwa kufanya hivyo siyo kama wamebadilisha msimamo wao wa kutomtambua Meya
Lyimo na Naibu wake, Estomii Mallah, isipokuwa ilibidi wafanye hivyo kutegua mtego wao wa madai ya kufukuzwa madiwani.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Chang’a alisema madiwani wa Chadema walipewa posho baada ya kuhudhuria kikao hicho na wala hakukuwa na njama za kutaka kuwafukuza kama alivyodai Lema.
Source: Habari Leo
Kumbe wewe hujui kuwa huyu jamaa ni mchaga. siiku alipotoka tu tumboni mwa mama hakulia mapka sarafu ilipodondoshwa chini. Zile kelele zake ni mpaka asikie SLAA ameunguruma istoshe ameshajua sasa ukweli wa CHADEMA peza zinadhibitiwa na FREEMANSONY bwana sasa yeye alale njaa?
 
Ni haramu sana kwasababu haiwezekani umkatae meya halafu hapohapo uhudhurie vikao. Hizi njaa zitawaua magwanda



Njaa itakuua wewe unayetumika! Tena unatumiwa vibaya hadi unajisahau kwamba ni njaa tu ndio inakuweka hapa. Sijui leo jf ikifungwa au Bwana wenu Nape akitimuliwa utachumia wapi tumbo lako maana una njaa kali sana. Hujifunzi kwa mwenzio TH. Sijui kafia wapi? Tumia akili mtoto, acha kutumia masaburi! Kijana mdogo unakuwa kama mzee wa enzi za ujima!? Period...!
 
Kumbe wewe hujui kuwa huyu jamaa ni mchaga. siiku alipotoka tu tumboni mwa mama hakulia mapka sarafu ilipodondoshwa chini. Zile kelele zake ni mpaka asikie SLAA ameunguruma istoshe ameshajua sasa ukweli wa CHADEMA peza zinadhibitiwa na FREEMANSONY bwana sasa yeye alale njaa?

Baada ya siasa za udini kugonga mwamba mmeamua kurudi kwenye siasa za ukabila.
Upuuzi mtupu!?
 
Ni haramu sana kwasababu haiwezekani umkatae meya halafu hapohapo uhudhurie vikao. Hizi njaa zitawaua magwanda

Hivi wewe Mwita25 mbona naonaga kama unawashwa na masaburi yako sana? Si umtafute Lema bila shaka atakumalizia tatizo lako lote. Maana cjawahi kuacha kupitia humu nikaona hoja zinazomsema MH. Lema halafu wewe na masaburi yako unakaa na kusema pumba tu. Mtazamo wangu WEWE msearch Lema alipo bila shaka atakugusa vema! Uwe mwelewa kilaza wee hii ni karne nyingine.
 
nifafanulieni wakuu, kuuza gongo ni halali, kuinywa ndiyo haramu!!
 
Hii thread safi sana.
Source: Habari Leo
Mchangiaji mkubwa: Omr/Mwita 25/Ritz/Nduka/Rejao.
Asanteni.
 
is it within the law for Lema to signed up for posho ? if it is not, call the authority to pick him up and stop complaining.

SWEET WORDS FROM THEIR MOUTH ARE NOT COMING FROM THEIR HEART. IF YOU ARE AUTHORITY THEN PICK THEM THIS IS THEIR SIN:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom