Lema alamba posho kikao cha madiwani Arusha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema alamba posho kikao cha madiwani Arusha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FIDIVIN, Sep 27, 2011.

 1. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kusaini na kuchukua posho ya kikao cha Baraza la Madiwani mwishoni mwa wiki, lakini akatetea uamuzi huo akisema alikwenda kuzima njama za kufukuzana.

  Lema na madiwani wenzake watatu wa Chadema, walishiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha, kinyume cha msimamo wao wa kutohudhuria vikao hivyo.

  Mapema mwaka jana, Lema na madiwani wote wa Chadema wa Jiji la Arusha waliweka msimamo wa kutomtambua Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo na kutohudhuria vikao vyote vya Baraza la Madiwani kwa madai kuwa Meya huyo hakuchaguliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na kuhudhuria vikao ni kumtambua.

  Lakini Ijumaa iliyopita, Lema na madiwani Isaya Doita (Ngarenaro), Crispin Tarimo (Sekei) na Sabina Francis (Viti Maalumu), walihudhuria kikao hicho na kupokea posho kwa malipo ya kuhudhuria kikao.

  Lema alikiri alisaini posho hiyo yeye na wenzake na kudai kulikuwa na njama za kutaka kuwafukuza madiwani wa Chadema kwa kukosa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila ya kuwa na taarifa yoyote na kwa mujibu wa sheria na kanuni wangetimuliwa.

  Alisema kwa kufanya hivyo siyo kama wamebadilisha msimamo wao wa kutomtambua Meya Lyimo na Naibu wake, Estomii Mallah, isipokuwa ilibidi wafanye hivyo kutegua mtego wao wa madai ya kufukuzwa madiwani.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Chang'a alisema madiwani wa Chadema walipewa posho baada ya kuhudhuria kikao hicho na wala hakukuwa na njama za kutaka kuwafukuza kama alivyodai Lema.

  Source: Habari Leo
   
 2. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mtajiju......Hata UDSM vijana wamepata akili za mgomo siku hizi,wanagoma siku mbili ya tatu darasani,siku2 ya3 class mpaka kieleweke,Safi kamanda,najua wanataka anzisha majungu hapa,akili kichwani maana wakifukuzwa hao madiwani wao si ndio watajiona wako sahihi!!!Twende kazi hakuna kulala mpaka mieleweke....
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  is it within the law for Lema to signed up for posho ? if it is not, call the authority to pick him up and stop complaining.
   
 4. b

  ben genious Senior Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri ndiyo lilikuwa lengo lao kuwatimua, kama watu wamehudhuria kwa nini mkurugenzi alalamike kwenye vyombo vya habari je alitaka wasiudhurie?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani hao habari leo bure kabisa ishu ni kudhuria kikao au posho?????
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Viongozi wengi wa Chadema wamevutiwa kwenye siasa na pesa za posho ila wengi wao ni wanafiki na waongo tu. Mtu kama Zitto alishawahi kuhongwa VX na RA lakini anajifanya eti yupo mstari wa mbele kupinga posho za vikao! Huyu Lema naye ana historia ya wizi wa Magari kwahiyo siwezi kumshangaa kama ameamua kuiba na kuchukua posho za vikao za madiwani. Haya ni mambo ambayo niliyatarajia kabisa kwahiyo siwezi kushangaa.
   
 7. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Mbona hutuelezi wewe umehongwa nini? Na hao magamba wanaoacha fani zao na kugombea uongozi wanafuata nini? Msipende kuufanya uongozi wa nchi yetu kuwa exclusive kwa magamba tu! We need change and PEOPLE'S POWER will prevail!!
   
 8. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Swala kubwa hapo ni lema kuhudhuria kikao au kulamba posho????!!!!
   
 9. O

  Omr JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Njaa mbaya, kelele nyingi lakini mgao ukipita wao ndio wa kwanza kutanguliza bakuli. Lema ni jambazi sasa mlitegemea nini kutoka kwake? Kama aliweza kuua watu kwaajili ya pesa sasa unataka aziachie za bila jasho.
   
 10. e

  ebrah JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  teh teh mtachonga sssssana, lakini kumbukeni uzuri wa wana chadema tumebarikiwa akili na ufaham!
  sema yote kete tumewanyima antunasonga kwa nguvu ya uma! peeeeeples!
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  mungu akusamehe, haujui ulitendalo. Unaweza kudhibitisha ujambazi wa Lema?
   
 12. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama hamtambui meya nadhani ni vizuri asingehudhuria vikao, akifukuzwa ubunge poa tu, lakini amesimamia anachokiamini na ambacho chama chake kinaamini. The same goes to CDM MPs.... wasingeitambua serikali ya JK.Anything else is BS.
   
 13. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Kweli eeh hata mkisema walivutwa na pesa au nini wana cdm ni wajuvi wa mambo chadema ipo tangu 1992 hatuja kulupuka kuipenda hata kama lema alikuwa jambazi mbona jambazi wenzie kina Alex masawe,Zombe,francis nyari mmewaacha huru au sababu huwa wanafadhili kampeni
   
 14. S

  Straight JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mbona na wewe unachukua Posho kwa Nape ili ushinde humu JF
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160  Mwitaaaaaa!

  Umeishiwa kabisa hoja! Imewauma sana maana hilo ni bao la kisigino. Mlitegemea kupeleka hoja ya kuwafukuza lakini wameizima. Sasa mmebaki mnazungumzia posho na propaganda.

  Pole sana, mpambano bado unaendelea na tutatumia mbinu zote hadi kieleweke!
   
 16. S

  Straight JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na kweli njaa mbaya, si unaona unavyolopoka kwa ku2mia masaburi, jikaze ndugu Nape anahesabu idadi ya post...
   
 17. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Yani wewe ukiona thread inamuhusu Lema tu, lazima utie kalamu. Lema fanya mpango umuoe huyu Mwita25. Anakupenda sana.
   
 18. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Duh! Kweli mafisadi wameanza kazi yao humu ndani. Nimesema tangu jana ya kwamba humu hata mkiingia na gia ya kupandia milima hakika tutawatambua tu. Humu tumo wa2 na akili ze2 timamu wa kutambua nani huyu na ni nani yule. Wewe uliandika thread hii kawaambie ya kwmb huko hapaingiliki kihivyo ulivyokuja wewe. Hii ni karne ya 21 bila shaka magamba mtateseka sana.
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Swali la msingi la kujiuliza hivi ni haramu diwani kuchukua posho aliyohudhuria kikao? Pia pana logic kusema kuwa hao madiwano wangefukuzwa kama wasingehudhuria kikao hicho maana kingekuwa kikao cha tatu kutohudhuria bila sababu ya msingi!
   
 20. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni haramu sana kwasababu haiwezekani umkatae meya halafu hapohapo uhudhurie vikao. Hizi njaa zitawaua magwanda
   
Loading...