Umechemka. Kilicholeta ushindi Arusha SIO Lema peke yake, bali sera madhubuti za CHADEMA.
Vitisho na ubabe wa CCM wakivinja sheria kwa kuwaumiza raia wasio na hatia kupitia kikosi chake cha kijeshi, Green Guards, ndio kimewafanya Watanzania kuiona CCM kuwa imefilisika.
CHAADEMA ni chama makini, elewa hilo, na kina viongozi makini, elewa hilo. Ndio, viongozi hao ni mtaji, lakini sio msingi wa CHADEMA kukubalika.
Hebu waulize vijana wa Arusha kuhusu ahadi hewa za CCM kuhusu ajira, usikie watakachokueleza.
Fanya utafiti, usikurupuke na kubwabwaja maneno yasiyoeleweka na yasiyo na mashiko. Fanya utafiti, jenga hoja. Inaonekana, kijana, uelewa wako wa masuala ya siasa na maendeleo na nini wanachokitaka watu ni mdogo sana. Sipendi malumbano, lakini nina mashaka na upeo wako. Au wewe ni mmoja wa wale waliofundishwa na walimu wa "VodaFasta"? Kama ni hivyo, basi sikulaumu. Lakini kama sivyo, hebu rekebisha kauli yako, unajidhalilisha.
CHADEMA ina viongozi wengi wanaokubalika huko Arusha, si Lema peke yake. Ushindi wa kishindo wa wagombea wa CHADEMA unadhihirisha kwamba kila mgombea alikuwa anakubalika, na ni mtu makini. Au umesahau alichojaribu kufanya Mwigulu Mchemba kwa kamanda wetu Mpinga? Mbinu chafu ya kumhadaa kwamba ametumwa na Rais, akijitoa na kuhamia CCM atapewa U-DC, huoni kwamba alikuwa tishio kwa CCM?
Hebu fanya upembuzi kidogo kijana, sio kuja hapa na hoja mfu. Fanya utafiti.
Kumbuka: No research, no right to speak.
Kama huelewi maana ya dhana hii, waulize waliokuzidi umri. Kwamba una nafasi ya kupost unachotaka ndani humu (poleni Mods, sasa naelewa kazi kubwa mliyonayo), haimaanishi unaweza kupost ----- wowote unaotaka.
Think, before you speak/write.
Kila la heri. CHADEMA tuko makini, na ni timu kabambe, ni kikosi kazi cha maendeleo. Si chama cha mtu mmoja mmoja. Unampa credit isiyostahili Lema, wakati kazi hii kubwa hakuifanya peke yake?