Lema airahisishia CHADEMA ushindi wa Udiwani Arusha


N

nassiry

Senior Member
Joined
May 7, 2013
Messages
182
Likes
0
Points
0
Age
41
N

nassiry

Senior Member
Joined May 7, 2013
182 0 0
Baadhi ya picha zikionyesha maelfu ya watu wakimsikiliza Jembe la Arusha kamanda Mpambanaji Mh G Lema akiiondoa CCM kwenye historia ya siasa Arusha na amefanikiwa kwa asilimia 93%
 

Attachments:

N

nassiry

Senior Member
Joined
May 7, 2013
Messages
182
Likes
0
Points
0
Age
41
N

nassiry

Senior Member
Joined May 7, 2013
182 0 0
Hawa ni watu wasiopewa hela bali hutoa hela kichangi harakati tofauti na ccm wanavyowapa pesa lakini hata wakija hawafikii ribi ya hawa
 
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,337
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,337 339 180
Hawa ni watu wasiopewa hela bali hutoa hela kichangi harakati tofauti na ccm wanavyowapa pesa lakini hata wakija hawafikii ribi ya hawa
Mkuu nenda kwenye heading nisaidie sijawahi kusikia mkoa au mji wa atusha.
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Soma hii hapa chini kwa makini


GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, kwa mara ya kwanza anakumbana na upinzani mkali jimboni kwake kutoka Chama cha Wananchi (CUF), FAHAMU limeelezwa.


Kwa sababu ya upinzani huo, Lema ameamua kusamehe vikao 40 vya bunge hatua itakayomkosesha kipato kinachokaribia Sh. Mil. 9 kinachotokana na posho ya kuhudhuria vikao hivyo kila siku.


Mbunge huyo anayewakilisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameamua kusamehe mapato yote hayo kwa lengo moja tu: Kukabiliana na ushindani mkali wakati huu ambapo kata kadhaa za ndani ya jimbo lake zimo katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kutokana na chama chake kufukuza madiwani wao.


Kata hizo ni miongoni mwa kata kadhaa nchini kote zinazoendesha uchaguzi mdogo uliopangwa kufanyika Juni 16, mwaka huu kujaza nafasi zilizoachwa baada ya madiwani wake kufa au kujiuzulu.


Kulingana na taarifa zilizopatikana na gazeti hili, Lema amechukua uamuzi huo mgumu baada ya kuamini pasina shaka kuwa ikitokea Chadema kupoteza kata hizo, mzigo wa lawama na shutuma utamuangukia yeye.


Kwa upande mwingine, kushindwa kwa chama hicho katika uchaguzi wa kata hizo, kutakuwa na maana ya hali ngumu ya kisiasa kumkabili yeye binafsi kama kiongozi wa ngazi ya juu pamoja na chama chake kuelekea uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.


"Mimi ni kiongozi wa uhamasishaji na nimeacha vikao vya bunge kwa ajili ya watu, ni fedha kama milioni 9 katika vikao 40 vya bunge.... natumia nguvu yangu ili ku-make sure (kuhakikisha) nashinda," anasema Lema


Kata zinazokabiliwa na ushindani mkubwa jimboni Arusha Mjini, ni Elerai, Themi na Kaloleni na kuna kila dalili kuwa ushindani huo unakuja kutokana na Chama cha Wananchi (CUF) kusimamisha wagombea wanaokubalika kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.


Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya wanachama wa Chadema na viongozi ndani ya jimbo na mkoa, wanaelezwa kuwa wanawaunga mkono wagombea wa CUF katika kile baadhi yao wanachokieleza kuwa "hatua ya kulipiza kisasi baada ya madiwani wa kata hizo kufukuzwa na Chadema."


Tofauti na Uchaguzi Mkuu 2010 Lema katika majukwaa amekuwa akitumia muda mwingi kuishambulia CUF akimwaga shutuma na mashambulizi yake kupitia kituo cha Redio Five.


Hivi karibuni, amesikika hewani akilituhumu Jeshi la Polisi kwa alichodai kushindwa kuwachukulia hatua wanachama wa CUF anaodai kuwa walilishambulia gari la Katibu Mwenezi wa Chadema Arusha.


"Gari la matangazo la katibu mwenezi ndio lilirushiwa jiwe, ilikuwa maeneo ya Msikiti wa Ijumaa, mhalifu anajulikana. Sisi tumeshachukua hatua ya kwenda polisi na hatua nyingine zinaendelea," alisema Lema.


Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma na Haki za Binaadamu wa CUF, Abdul Kambaya ameliambia FAHAMU kwamba chama hicho kimetambua udhaifu wa wapinzani wao wakubwa (Chadema) kwani kimegawanyika makundi mawili.


"Tumetambua udhaifu mkubwa wa Chadema hapa Arusha, hawa hawapo pamoja kutokana na kushindwa kuelewana. Wanacheza pamoja lakini kila mmoja anawaza lake na ndio maana Lema anashindwa kuondoka hapa kwenda bungeni," alisema Kambaya ambaye amepiga kambi jijini Arusha kuongoza kampeni za CUF.


Wakati Kambaya akisema hivyo, Lema alisema "hisia zangu ni kwamba CUF ni watu waliozidiwa, CUF kipo Arusha lakini kina watu wachache sana kama vile hakuna. Nakumbuka katika Uchaguzi Mkuu mimi nilipata kura 6,000 na wao walipata kura 400 kwa hiyo CUF haipo Arusha."


Wakati Lema anajigamba kuwa CUF haipo jimboni Arusha, amekuwa akitumia mbinu ya kukipakazia CUF kuwa ni CCM B Zanzibar huku akiwashambulia wale madiwani waliosimamishwa na Chadema.


Ingawa anawashambulia madiwani wao wa zamani, hali inayoonekana katika kampeni inathibitisha kuwa Lema anamlenga zaidi John Bayo, mgombea udiwani kupitia CUF katika Kata ya Elerai.


Taarifa kutoka Chadema zinaeleza chama hicho kimegawika makundi mawili kutokana na kundi moja kujiona wanyonge na kundi jingine kujipa mamlaka mkoani Arusha.


Hali hiyo imesababisha chama hicho kupungua mvuto kwa watu na kurahisisha kampeni ya CUF kupenya kisawasawa ndani ya nyoyo za wakazi wa kata hizo zinazogombaniwa.


Mwandishi wa FAHAMU aliyeko jijini Arusha ameshuhudia mara kadhaa baadhi ya viongozi wa Chadema wakimgeuka hadharani Lema na kupanda kwenye majukwaa ya CUF kuwanadi wagombea wa chama hicho ambacho kina siasa za kistaarabu majukwaani na mitaani.


Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema wanaoinadi CUF ni Katibu Mwenezi wa Kata ya Olorien, Prosper Mfinanga na Mwenyekiti wa Kata ya Terati, Gerald Majengo.


Mara kadhaa viongozi hao wamekutwa wakimtuhumu Lema kwa madai kuwa anawagawa wanachama. Vituo vya redio vya mkoani Arusha vimesikika mara nyingi vikirusha tuhuma hizo.


Mjini Arusha, baadhi ya wanachama wa Chadema waliwahi kufikisha malalamiko yao kwa Katibu Mkuu wao, Dk. Willibrod Slaa yanayohusu matumizi mabaya ya michango inayotolewa na Chadema katika kampeni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).


Viongozi hao wanalalamika kuwa Lema anatumia raslimali za chama kwa ajili ya maslahi binafsi.


Tuhuma hizo zilimfikia Dk. Slaa na mwaka jana wakati alipozungumza na gazeti hili, alithibitisha kuzipata na akawataka wanachama hao kumpelekea ushahidi.


Wanachama hao walichukizwa na msimamo wa Dk. Slaa na hivyo kuongeza mpasuko unaokidhoofisha chama hicho kwa kuamini kuwa Dk. Slaa na viongozi wenzake waandamizi walioko Makao Makuu Dar es Salaam wanambeba Lema.


Wao walisema walichokitarajia baada ya kutoa malalamiko dhidi ya Lema, ni chama kuendesha uchunguzi wa tuhuma walizozitowa dhidi ya yake.


Taarifa zilizowekwa kwenye orodha ya madai ya wanachama hao na kuzifikisha kwa Dk. Slaa zilieleza kuwa, Lema bila ya woga amekuwa akifanya ufisadi, ubabe, vitisho na hata matumizi ya nguvu kukabiliana na wanachama na kwamba kutokana na hali hiyo, baadhi ya viongozi na wanachama wameamua kumgeuka.


Katika andiko lao kwa Dk. Slaa, makamanda hao waliitaka Kamati Kuu ya Chadema kufanya uchunguzi wa haraka na wa kina wakiorodhesha tuhuma kadhaa ikiwamo ya kutafuna fedha za wajane na yatima.


"Tunaiomba Kamati Kuu kufuatilia kwa makini yafuatayo kwa ajili ya ustawi wa chama…huyu Bwana (Lema) aliomba kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wananchi, akapewa.


"Je bado kipo?, bado malengo yake ni kujengwa hospitali na kimeandikishwa kwa jina la nani?" walihoji makamanda hao katika barua yao Kumb. Na. 01/CDM/AR ya Novemba 05, mwaka jana, iliyosainiwa na Majengo kama Mwenyekiti na Mfinanga kama Katibu kwa niaba ya wenzao zaidi ya 20.


Alipoulizwa na FAHAMU kuhusu tuhuma hizo ambazo zinadaiwa kukivuruga chama na kutoaminika kwa baadi ya viongozi na wanachama, Lema alionesha kukasirishwa.


"Mimi nilijua tu lazima utaniuliza hilo swali, nyinyi mmekuwa mkiandika habari za kutengeneza..., kuna kipindi mlikuwa mkiandika lakini tukawacha tu kwasababu hamkuwa na wasomaji wengi.


"This time (muda huu) sitawaacha, nitawapeleka mahakamani, nionye tu kwamba, kuna wakati tutakuwa very serious (makini sana) na gazeti lenu kutokana na story (habari) zenu," alisema Lema alipohojiwa mwishoni mwa wiki.


Lema alishikiliwa wajibu wake kujibu tuhuma na siyo kulalamika na hatimaye alisema, "sikiliza kamanda, mimi natumia pesa kutoka katika akaunti yangu kwa kutoa misaada pamoja na kukiimarisha chama, na kama chama kina mbinu zake, mimi si mtunza fedha nitafujaje fedha za chama."


Majengo ambaye ni mmoja wa viongozi waliosaini waraka wa malalamiko dhidi ya Lema, aliliambia gazeti hili jana kuwa malalamiko hayo waliyapeleka makao makuu ambao wakubwa waliyapuuza.


"Tulifikisha malalamiko hayo wenyewe Dar es Salaam lakini wakubwa hawakuchukua hatua yoyote, wanalindana. Tuliwaeleza Lema amekuwa akisema yeye uongozi wake ni wa familia na matumizi mengine mabaya.


"Nakumbuka kuna trekta lililotolewa kwa ajili ya chama halijulikani lilipo, kuna kiwanja cha hekari tano kilitolewa lakini hakielezwi hati yake imeandikwa jina gani. Napanda majukwaa ya CUF kueleza ukweli huu," alisema.


Kuhusu Lema kuchangia fedha kutoka kwenye akaunti yake, Mwenyekiti wa Chadema M


Source: gazeti la FAHAMU[/QUOTE]
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Mkuu nenda kwenye heading nisaidie sijawahi kusikia mkoa au mji wa atusha.
Hawa ni wale vijana wetu wa form four wa mwaka huu amao ni bahati mbaya mkuu
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Hawa ni watu wasiopewa hela bali hutoa hela kichangi harakati tofauti na ccm wanavyowapa pesa lakini hata wakija hawafikii ribi ya hawa
Huwa wanachangia saccos ya chadema au vp mkuu? Halafu ribi ndio mdudu gani huyo?
 
L

lupe

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
5,659
Likes
5
Points
0
L

lupe

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
5,659 5 0
Fahamu ni gazeti la udaku ka ccmB .
 
Ranks

Ranks

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
2,597
Likes
866
Points
280
Ranks

Ranks

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
2,597 866 280
Huo ni ujuha kwa CUF mahtuti mpendwa wa ccm mfu kuamini kwa kutumia makapi ya CHADEMA itaimarika.,A -town ni ya ma-people.
 
UmkhontoweSizwe

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,660
Likes
813
Points
280
UmkhontoweSizwe

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,660 813 280
Mkuu, FAHAMU ni gazeti au blog? Sijawahi kabisa kusikia hii kitu?
 
L

lupe

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
5,659
Likes
5
Points
0
L

lupe

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
5,659 5 0
Mkuu, FAHAMU ni gazeti au blog? Sijawahi kabisa kusikia hii kitu?
Mkuu fahamu ni gazeti la ccm"B" aka CUF, ni gazeti la uwongo na upotoshaji kama gazeti la uhuru! Ni kama clouds fm nayo ni radio ya upotoshaji inayorumiwa na ccm.
 
L

lupe

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
5,659
Likes
5
Points
0
L

lupe

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
5,659 5 0
Hawa ni watu wasiopewa hela bali hutoa hela kichangi harakati tofauti na ccm wanavyowapa pesa lakini hata wakija hawafikii ribi ya hawa
Mku ni kweli kabisa!
 
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
8,614
Likes
409
Points
180
Age
37
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2012
8,614 409 180
Cuf nayo inajipigia propaganda Arusha,hii ni kichekesho.
 
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
2,524
Likes
6
Points
135
L

Lilambo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
2,524 6 135
Lema ashafisadi trekta na shamba ekari tano. Hao madiwani watafuat nyayo za mbunge, hata hawafai kwanza. Washazuiwa kuhudhuria vikao vya maendeleo watawezaje kuleta maendeleo. Yan msimamo wa chadema uwaumize wanaArusha? Hiyo haiwezekani cdm mmejikoroga.
 
M

mgoli magombe

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
121
Likes
6
Points
35
Age
34
M

mgoli magombe

Senior Member
Joined Apr 20, 2013
121 6 35
Kwa umati huu mnzinzi (mchemba )rudi tu bungeniu utaaibika kama ulivyotorokaga arumeru mashariki.
 
Makala Jr

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Messages
3,396
Likes
19
Points
135
Makala Jr

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2011
3,396 19 135
Ngoja tusubiri wananchi wa Arusha wafanye mamuuzi maana hizi ngonjera za waliberali sizielewi!
 

Forum statistics

Threads 1,273,879
Members 490,535
Posts 30,494,902