Lema 'aichana' Idara ya Usalama wa Taifa

Status
Not open for further replies.
Katika hatua hiyo Lema aliyataja majina ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao wapo kwenye mkakati wa kuhujumiwa wakati wowote na vyombo vya usalama kuwa Ephata Nanyaro ambaye tayari amehojiwa, Joseph Kredo Katibu.
Wengine ni Emanuel Kombe ambaye naye amehojiwa, Hilary Mkonya Mhazina wa Chama, Odelo Odelo Mwenyekiti wa BAVICHA, Kamnde tayari amefikishwa mahakamani kwa
tuhuma za kukutwa na silaha aina ya SMG na Bastola,Glory Shio Mwenyekiti wa BAWACHA, Happy Charles, Sarungi, na wengine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arusha Ephata Nanyaro kwa upande wake aklibainisha kuwa tayari ameandika maelezo polisi akikanusha kuhusika na kikao cha kupanga njama za kumuua Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo.
“Nimehojiwa kwa zaidi ya Saa 7 tena ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO) akiwa na maofisa kutoka Dar es Salaam makao makuu ya Polisi.
“Katika maelezo yangu bado nilikana sina ugomvi na Gaudence, sijahusika na madai ya kupanga kumuua niliwaambia sintamtambua kamwe kwa nafasi aliyonayo,” alisema Nanyaro na kuongeza:
“Tunaushahidi katika kuhojiwa kwangu kwamba Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanahusika kwani wameonyesha uwazi wa kuwatisha viongozi wa CHADEMA.
“Martine Luther King mwanaharakati wa Kimarekani aliwahi kusema; “Kama hakuna jambo lolote binadamu yupo tayari kufa kwalo huyo binadamu hastahili kuishi”. CHADEMA tuna amini uchaguzi wa Meya Arusha ulikuwa ni batili hilo tutaendelea kuliamini mpaka mwisho,” alidai Nanyaro.

hilo nimeamini, hata mimi hayo yalinikuta japo siyo kuhojiwa bali vitisho kutoka kwa moja wa usalama wa taifa, akaniambia kwa kitendo changu cha kuendelea kuwahamasisha vijana kupokea kadi za chadema anaweza kunihamisha ninapoishi, kwa kuwa ni nyumba za serikali.
hizo silaha alikuwa anazimiliki kihalali? na kama sio kwanini asifuatiliwe kama mwananchi mwingine yeyote?
 
Lema marekebisho kidogo, hao wanaitwa Usalama wa Serikali si Usalama wa Taifa!

Ni Agent wa Usalama wa Taifa, ambao wanashughulikia usalama wa Serikali na viongozi wa Serikali, wana Mkurugenzi wao pia nadhani ni idara inayojitegemea kama Polisi. Nadhani ni sehemu ya Usalama wa Taifa kama vile Polisi, JWTZ nk.


Wanaofahamu zaidi wafafanue. Hayo ni mawazo yangu kwa kuangalia muundo na kazi wanazofanya hao jamaa na jina la idara yenyewe.
Kazi za usalama wa Taifa ni hizi hapa.
View attachment 36417
 
unajua kuna vitu vingine ni uchochezi wa hali ya juu just kwamba chadema kaongea basi ni ukweli tutafakari maneno ya mtu mwennye kuchochea hata kama usalama wa taifa wanahujumu if u speak then open up kabisaaa wataje tujue who n who ,bcz usalama wa taifa wapo kwa ajili ya usalama wa nchi na ni kitengo kikubwa sana ambacho kimekuwa hapo kabla ya lema na hata kama wao chadema wakishika nchi they will still be there for nchi so angalia lema isije kuwa unarusha mawe wakati upo kwenye nyumba ya vioo sijui wewe ukirudishiwa utasema wanakuhujumu if u have been to a places or doing some stuff n u started to leta uchochezi ili watu wafanye nguvu ya umma there is no such thingz ,give us a break,,,,,
 
Hata hiyo act imekaa, kimaslahi ya uongozi kuliko umma. Inatoa mianya ya abuse ya TISS. It needs review. Soma ya CIA
 
Sheria inayounda chombo chetu cha TISS ni sharti iendane na wakati; muundo mzima na kazi zake ni za MAZINGIRA YA CHAMA KIMOJA wakati shughuli zake kiuhalisia ni katika mazingira ya vyama vingi.

Huu ndio ukweli unaoleta mgongano wa kila mara dhidi ya SAUTI HURU ambao huko nyuma walichukuliwa kuwa ni MAADUI wakati leo hii ni wanao nafasi stahiki isiyostahili kubanwabanwa kwa kukisaidia tu chama kinachotawala kwa kipindi husika.
 
Lema ni shujaa wetu. USALAMA WA TAIFA si wakuwaamini hata kidogo, POLISI nao ndo zaidi. Siku si nyingi ukweli utadhihiri. WANATAKIWA KUELEWA KUWA, HIVYO NI VYOMBO VISIVYOFUNGAMANA NA SIASA ZA VYAMA, KWA KUFANYA HIVYO WANAPANDA MBEGU YA UBAGUZI KWA RAIA.
 
Anayedhania ya Gaddafi yanatofauti sana na haya afikiri tena. Mwanzo wa vituko vyote vya Gaddaf ulikuwa ulevi wa madaraka na kufikiri dola linaweza kumlinda kwa njia yoyote!

Kazi ya vikosi vyetu ni kusimamia haki na si kutekeleza majukumu kwa malengo ya chama chochote. Watawala kuweni makini na njia mnayochagua taifa letu lipitie.

Naendelea kuamini uhuru wa kweli bado kupatikana.

YANGU NI HAYO.......!
 
Huyu Bwana wa usalama wa taifa anaitwa Mombo nasikia leo kahojiwa na mabosi wake , kwani ni mtu mwenye kiburi na unyanyasaji wa hali ya juu na kazi yake kutishia wafanyabiashara wa madini na kunywa pombe ktk baa moja ya first and left hata hivyo pia ni mtu anayemiliki magari mengi ya kifahari na anayo range rover ambayo kwa taarifa hii gari inasemekana alimdhulumu bwn mmoja anaitwa Hamad mfanya biashara wa magari mjini arusha.
kuna taarifa kutoka Tra ambazo tunazipokea kesho kuhusu ni jinsi gani huyu mtu anatumia cheo chake kuonea wananchi mjini arusha. kaeni mkao kesho tunaweka uozo wote wake hapa mpaka na mtu aliyekuwa anatembea na mke wake huko nyuma anayo mambo mengi yakutueleza
 
usalama wa taifa +polisi+Lema=vita kaeni chonjo waachieni wenyewe walumbaneeee wakichoka watanyamaza!!!
 
Lema ni mbunge wa Tanzania anastahili sifa na kuungwa mkono kwa hayoa anayoyasema, watz tumeonewa kiasi cha kutosha sasa tuchukue madaraka kwa nguvu hawatuwezi kama wameshindwa akina Qadhaff na Mubarak itakuwa hawa wacheza mdundiko?
 
Tanzania hii ina wenyewe, wazalendo wa kweli ambao hatuko tayari kuona inachezewa.
Wana-Arusha tumechoshwa na vitisho na pumba za huyu Mbunge. Thubutu kulianzisha uone jinsi wananchi watakavyoungana na vyombo vya dola kuwaweka sawa. Hatujasahau jinsi wewe na wasanii wenzako mlivyosababisha watu kufa na baadaye kutumia maiti zao kujinadi kisiasa. Hamtapata nafasi nyingine ya kufanya huo ufedhuli.
Tuacheni tuchape kazi tujenge nchi yetu, Hatuna muda wa kupoteza vijiweni kama machalii na masela wako.Ngebe za kisiasa zisubiri 2016.

mkuu hv una umri gani?samahani lakini...
 
hawa jamaa wa Usalama ni wa Taifa au CCM....?
hapa haingii akilini hata kidogo Ofisa usalama asiyekwenda School? school husaidia sana kutafakari katika maisha.
I wish wangezipitia kanuni za uchaguzi, ili wapate kujua ukweli kama malalamiko ya CDM yana mshiko au laa....?
n then wakawape ushauri wakubwa zao.
kutumia public office kwa maslahi ya itikadi za CCM ni ujuha na uhuni usiopaswa kuvumiliwa!
kutumwa kufanya jambo pasipo tumia akili na busara ni Ujinga mkubwa na ni hatari sana!
 
Kazi za usalama wa Taifa ni hizi hapa.
View attachment 36417

Ukisoma hii attached file, hapa ni moja kwa moja Lema kavunja sheria kumtaja agent kwa jina lake na anastahiri kufikwa kwenye vyombo vya sheria. Maana imeandikwa mtu kutoka idara hii anayeweza kutajwa waziwazi ni DG tu. Sasa Lema kama mbunge na mtunga sheria hakulijua hili?
 
Idara imevurungwa na wahuni wachache na kuwa kama mradi wao na wala si kuwa watumishi wa kuangalia usalama na mali nchi hii. hata hivyo nashangaa hii thread imedumu kwani nimengundua tukiongelea hawa spoon feeder wa kikwete thread inafutwa fasta fasta.
 
Nadhani ppo wa arusha ndo watatuambia leo Mh.lema anafanya kazi gani jimboni kwake!
 
Huyu Bwana wa usalama wa taifa anaitwa Mombo nasikia leo kahojiwa na mabosi wake , kwani ni mtu mwenye kiburi na unyanyasaji wa hali ya juu na kazi yake kutishia wafanyabiashara wa madini na kunywa pombe ktk baa moja ya first and left hata hivyo pia ni mtu anayemiliki magari mengi ya kifahari na anayo range rover ambayo kwa taarifa hii gari inasemekana alimdhulumu bwn mmoja anaitwa Hamad mfanya biashara wa magari mjini arusha.
kuna taarifa kutoka Tra ambazo tunazipokea kesho kuhusu ni jinsi gani huyu mtu anatumia cheo chake kuonea wananchi mjini arusha. kaeni mkao kesho tunaweka uozo wote wake hapa mpaka na mtu aliyekuwa anatembea na mke wake huko nyuma anayo mambo mengi yakutueleza

ebwana tunasubiri muendelezo wa hii movie kesho ndugu......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom