Lema 'aichana' Idara ya Usalama wa Taifa

Status
Not open for further replies.

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Messages
981
Points
500

n00b

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2008
981 500
MBUNGE wa Jimbo la Arusha Godbless Lema CHADEMA) ameionya na kuitaka Idara ya Usalama wa Taifa nchini kujifunza kutoka kwa Kiongozi wa Libya Muammar Gadaffi.

Mbali na kuinyoshea vidole Idara hiyo Lema pia amewataka Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoani hapa kutambua kuwa kazi yao si kukitetea Chama cha Mapinduzi (CCM) bali ni kutetea maslahi ya taifa.

"Kama Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanafikiri wao wana nguvu sana wanapaswa kujua kwamba wanajidanganya. Kama wanataka kujua nguvu zao zina uwezo kiasi gani, wasafiri kwenda kuiuliza Idara ya Kijasusi ya Libya kama ilimsaidia Gadaffi asipinduliwe kwenye nchi aliyoingoza kwa miaka zaidi ya 40," alidai Lema.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini Arusha Lema alidai taarifa za Kiintelijensia walizonazo zimedhibitishia pasipo shaka kuwa Idara ya Usalama wa Taifa mkoani Arusha inatumika kwenye mgogoro wa Meya.


Godbless Lema akiongea na waandishi

Alidai kuwa mtu anayetuhumiwa kuongoza mpango huo mchafu unaolenga kuwaangamiza viongozi wa kisiasa wa CHADEMA ni Msaidizi wa Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Arusha.

Endelea >>> FikraPevu | Lema 'aichana' idara ya Usalama wa Taifa
 

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,982
Points
1,500

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,982 1,500
Lema ni kamanda wa ukweli, hababaiki wala hamumunyi maneno kama JK. Huyu Jamaa anafaa kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
 

Mumwi

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2011
Messages
592
Points
170

Mumwi

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2011
592 170
Mungu atusaidie Tanzania.
Tanzania ulikuwa na amani lakini tunaona kidogo kidogo umeanza kuishiwa na amani je Tanzania unatupeleka wapi?
 

Feedback

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
7,995
Points
1,500

Feedback

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
7,995 1,500
"Kuanzia Jumatatu tutaendesha ‘movement' ambayo hawajawahi kuiona na wakiendelea hivi pengine ukombozi wa nchi unaweza kuanzia Arusha," alidai.
Hii statement si ya kupuuzia wana Arusha wanawaaminia mkilianzisha sisi wa Mwanza tutaitikia haraka sana.
 

Henry Kilewo

Verified Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
898
Points
250

Henry Kilewo

Verified Member
Joined Feb 9, 2010
898 250
Mb wa Arusha Mjini Godbless Lema leo amefanya kikao na waandishi wa habari na kulaani kitendo cha polisi kushirikiana na usalama wa Taifa huku akimtaja Bwana Mombo afisa msaidizi usalama wa taifa mkoa kuhusika ktk njama za kuwafungulia kesi wanachama wa chadema na huku lengo kuu na mkakati ukiwa ni yeye.

Hivi karibuni jeshi la polisi mkoani arusha limewahoji viongozi wa chadema , Bwana Emanuel Kombe katibu mwenezi na Ephata Nanyaro mwenyekiti wa wilaya Arusha mjini kwa tuhuma za kupanga mauaji dhidi ya meya feki wa arusha , cha kushangaza ni kwamba watu hao wanaodai kuwa walihusika kwenye vikao hivyo ndio hao waliofanya maandamano kumpinga nanyaro na mb lema siku ya tarehe 6/8/2011 wakimshutumu mh lema kwa msimamo wake dhidi ya kutokubaliana na muafaka wa na leo wanasema walikuwa na kikao na mh lema na nanyaro tarehe 11/8/2011 cha kupanga mahuaji dhidi ya meya wa kichina.

Hebu fikirieni inawezekana vipi ukapanga mipango ya aina hii na adui yako , lakini hata hivyo Mh lema amesema yuko tiyari hata kupoteza\maisha yake kwa ajili ya kutetea umma wa watanzania , na kuomba serikali imchunguze bwana Mombo kwani ni afisa usalama anayeishi maisha ya anasa sana.
 

Mumwi

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2011
Messages
592
Points
170

Mumwi

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2011
592 170
Nafikiri Arusha siku moja itakuwa Banghazi ya Tanzania maana chadema inatafutiwa kila sababu ili iangushwe lakini hawataweza maana watu Wa Arusha sasa hivi wako tayari kwa lolote.
Niliona siku ya mkutano Wa chadema ulifanyika mwezi uliopita.
Ombi langu kwa usalama Wa taifa wasitumiwe na vyama kutuharibia nchi.
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,743
Points
0

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,743 0
Ukiisoma hii habar unabak unashangaa,mauaji ya nyamongo hatujasikia polis wala afisa wa usalama wa taifa toka makao makuu,mambo ya kipuuz kama haya wanahangaika,nadhan maofisa wa serikal wanaitumia chadema kama chanzo chao cha POSHO,kwasababu wanajua lazima watatakiwa kusafiri kujifanya wanakifuatilia
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
11,036
Points
1,250

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
11,036 1,250
Hakika hata nami naamini UKOMBOZI utaanzia hapa Arusha na siyo kwingine na tukae na 2subirie. Kwanini Watanzania tuwe kwenye hali hii? Na wakati maslahi yote muhimu yapo? Tusubiri na tuone mwisho wa hawa mafisadi ni wapi. Ukombozi ni SASA!
 

Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Messages
217
Points
0

Tetere Enjiwa

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2011
217 0
Natilia sana mashaka umakini wa huyu mheshimiwa, hasa pale anapotaka kulinganisha TZ na Libya au waTZ na walibya nadhani atakuwa anafanya makosa makubwa sana kama si kujidangaya. Niangalizo tu.
 

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,777
Points
2,000

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,777 2,000
CCM na serikali yake wanapaswa kuwa proactive na kuanza kuchukua hatua madhubuti za kuleta mabadiliko makubwa ya kijamii, vinginevyo wakiendelea kusubirisubiri watajikuta wamechelewa kama madikiteta wa Tunisia, Misri na Libya. Mabadiliko lazima yaje, tena yanakuja kama mafuriko ya maji, CCm wakijifanya kichwangumu yatawakumba bila huruma.
 

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,982
Points
1,500

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,982 1,500
Katika hatua hiyo Lema aliyataja majina ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao wapo kwenye mkakati wa kuhujumiwa wakati wowote na vyombo vya usalama kuwa Ephata Nanyaro ambaye tayari amehojiwa, Joseph Kredo Katibu.
Wengine ni Emanuel Kombe ambaye naye amehojiwa, Hilary Mkonya Mhazina wa Chama, Odelo Odelo Mwenyekiti wa BAVICHA, Kamnde tayari amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya SMG na Bastola,Glory Shio Mwenyekiti wa BAWACHA, Happy Charles, Sarungi, na wengine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arusha Ephata Nanyaro kwa upande wake aklibainisha kuwa tayari ameandika maelezo polisi akikanusha kuhusika na kikao cha kupanga njama za kumuua Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo.
"Nimehojiwa kwa zaidi ya Saa 7 tena ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO) akiwa na maofisa kutoka Dar es Salaam makao makuu ya Polisi.
"Katika maelezo yangu bado nilikana sina ugomvi na Gaudence, sijahusika na madai ya kupanga kumuua niliwaambia sintamtambua kamwe kwa nafasi aliyonayo," alisema Nanyaro na kuongeza:
"Tunaushahidi katika kuhojiwa kwangu kwamba Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanahusika kwani wameonyesha uwazi wa kuwatisha viongozi wa CHADEMA.
"Martine Luther King mwanaharakati wa Kimarekani aliwahi kusema; "Kama hakuna jambo lolote binadamu yupo tayari kufa kwalo huyo binadamu hastahili kuishi". CHADEMA tuna amini uchaguzi wa Meya Arusha ulikuwa ni batili hilo tutaendelea kuliamini mpaka mwisho," alidai Nanyaro.

hilo nimeamini, hata mimi hayo yalinikuta japo siyo kuhojiwa bali vitisho kutoka kwa moja wa usalama wa taifa, akaniambia kwa kitendo changu cha kuendelea kuwahamasisha vijana kupokea kadi za chadema anaweza kunihamisha ninapoishi, kwa kuwa ni nyumba za serikali.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,353,237
Members 518,297
Posts 33,075,459
Top