Kizuri ni kujua mazingira, nasaba na haiba ya wakazi wa majimbo hayo kwa kila mmoja.Lema anawakilisha jimbo la Arusha mjini ambalo lina wakazi wake wana mchanganyiko lakini wenyeji walio wengi ni Waarusha,Wamelu,Masai,Wachaga na hao wote kiahaiba wanajulikana ni aina ya watu walio wazi kiasilia na wasio taka mzaa na ubabishaji au kupindisha maneno, Wakazi hao wa Arusha ni wafuasi wa kutambua Koleo ni koleao na kijiko ni kijiko,na hivyo si sawa kusema koleo ni kijiko kikubwa.
Wakati huo mnyika ni mwakilishi wa jimbo la Ubungo ambalo wakazi wake ni mchanganyiko wa makabila tofauti tofauti na wenyeji wake wengi ni wazaramo na mchanganyiko wa makabila ya pwani kama wakwere nk,ambayo kihaiba ni watu wa kuchukulia utatuzi wa matatizo kwa misingi ya maongezi ya muda hata kama yatakuwa na kero kubwa kwao na hasara yoyote wao imani kubwa kuwa mtapata suluhu muda ukifika.
Kwa picha hiyo utaona kila mmoja anaongoza jimbo likiwa na utamaduni tofauti wa wenyeji wake wakiwa na mtizamo tofauti wa kiamapokeo na utatuzi wa matatizo yao.
Msimuonee Lema angalieni jamii,na tamaduni,Nyerere na uwezo wake wote wa kuwajenga watanzania bado alipofika kwa ndugu zake wakurya ilikuwa ni kazi kuwaelimisha na kuwafikishia ujumbe,na mpaka ameondoka bado mkoa ule kauacha akiwa hana jibu kamili ni watu wa aina gani.