Lema ahofia Mwenendo wa Mbowe na CCM

Lema ahofia Mwenendo wa Mbowe na CCM

Mimi nahofia juu ya uelewa wako,hapo mbona Lema anahofu na CCM na hila zao wala sio Mbowe?ndio maana kamuombea kwa Mungu ili aweze kuziona hizi hila
Ingekuwa ana hofu na CCM kufuata msimamo wa Chadema Lema Wala asingemuuliza Mbowe kama yanayotokea bungeni hayana baraka za CCM
 
Mkuu
Kuna makubaliano FULANI hivi Mbowe anafanya na CCM ambayo katumwa na ofisi kubwa ambayo ccm inawajibika kwao!!!
Wasiwe na shaka! MBOWE anajua Taasisi anayoitumikia ambayo hata wafuasi WENGI wa CHAMA hawajui!!!

Hakuna anachokijua yule ni msanii tu kama unabisha rejea kuanguka kwakwe kwenye ngazi na kusema alipigwa na Watu wasio julikana,kumtangaza Lowassa kuwa mgombea urais kupitia chadema na kumwaga Wlibroad silaaa.
 
Mbowe ashajua Njia ya Violence na vitisho kamwee haitasaidiaa kituuu...!! Wameanza kukubali mchakato wa katiba mpyaaa nice move.... Mbowe asianze kutupia mawe mbwa wanaobweka pembeni aendelee kusonga mbelee! Kina mdee watatolewa tu ila Serikali haitaki kuonekana imeshurutishwa na chadema na chadema nao kelele hawaachi hawajui ndo wanazidi kuharibuu...

sasa wakati ACT walipoanza na njia kama hiyo kwanini mulikua munawatupia matusi? Au ndio kunya anye kuku tu akinya Bata kahara?
 
Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Godbles Lema,ameanza kuwa na wasiwasi juu ya uaminifu wa Mwenyekiti wake wa Taifa Freeman Mbowe na Chama Cha Mapinduzi(CCM),kuwa unaweza kumpofusha kiongozi wake huyo asione hila yoyote kutoka kwao.

Lema ameonyesha hofu hiyo kupitia Ukurasa wake wa Twitter,leo Juni 23 ambapo ameandika na kumuasa Mbowe juu ya ukaribu wake na CCM hasa wakati huu ambao sakata la wabunge 19 wa Chama hicho likiwa linazungumzwa katika mazingira tofauti.

Katika kuonyesha hofu yake hiyo kupitia Twitter Lema ameweka picha inayomuonyesha Mbowe,Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Mstaafu Abdul Rahman Kinana

Katika picha hiyo ambayo Mbowe ameweka mikono yake mbele mithili ya mtoto anayeomba msaada kwa Mzee wake Lema ameandika

"Mwenyekiti nimefanya kazi na wewe kwa muda Mrefu.Naujua moyo wako juu ya nchi,najua Nia yako.Ninakiri kuwa umejitoa kwa ajili ya Tanzania.Tunapokuwa kwenye mazungumzo ya Tanzania Bora muombe Mungu akuonyeshe hila"

Kisha akauliza swali kuwa

"Unafikiri Spika anaweza kuvunja sheria Bila baraka za CCM?"

Kauli hiyo ya Lema imebebwa kwa uzito mkubwa na wachangiaji mbali mbali ikizingatiwa kuwa ni mkosoaji na mtu mwenye maono ambayo mara kadhaa yamekuwa yakijidhihirisha.

Miongoni mwa waliomuunga Lema Mkono juu ya hofu yake hiyo ya Mwenendo wa Mwenyekiti ni pamoja na mwanaharakati wa mitandaoni Mdude Chadema ambaye aliishauri badala ya kutumia neno CCM Lema angepaswa atumie neno Samia.
Mbowe hawaze kubadirika, hii “strategical change”, yupo palepale, anaweka soft power kwanza, akiibuka hapo watashindwa kumdaka. Hamuna kitu kilichomdhoofisha Mbowe kama kumwingiza Lowasa kugombea Urais kupitia chadema mwaka 2015.

Hii faulo iliwapaisha CCM sana
 
Am also so worried about this so called Chadema Chairman. Time will tell but am kind of smelling a Rat type of a thing.
 
Back
Top Bottom