LeBron James asaini mkataba mpya, kulipwa Bilioni 9 kwa mwezi

Airmanula

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
3,741
5,288
Nyota wa Kikapu nchini Marekani LeBron James amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na Los Angeles Lakers, mkataba wenye thamani ya ($85 million) ambao utamuweka kwenye timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2022-2023.

Kwa mujibu wa ESPN, mkataba huu mpya unamuonesha LeBron James akilipwa kiasi kikubwa cha fedha kwa dakika hadi miaka miwili;

Kwa dakika 1 atakuwa akilipwa ($82) sawa na TSH. 190,158

Kwa Saa 1 atalipwa ($4,891) sawa na TSH. Milioni 11

Kwa Siku 1 atalipwa ($117,397) sawa na TSH. Milioni 272

Kwa Mwezi Mmoja atalipwa ($3.57M) sawa na TSH. Bilioni 9

Kwa Miaka 2 ya mkataba wake atalipwa ($85.7M) ambazo ni sawa na TSH. Bilioni 197
 
Nyota wa Kikapu nchini Marekani LeBron James amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na Los Angeles Lakers, mkataba wenye thamani ya ($85 million) ambao utamuweka kwenye timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2022-2023...
Mlaumu mshua kwa kupata school fees. Angekosa school fees leo Tanzania ingejua kipaji chako. Plutnumz ana shine kwa sababu ya kipaji tu.
 
Hizi akili hizi,kwahiyo ukikosa Elimu,unakuwa na kipaji?mfano Diamond,Masanja mkandamizaji,hawana Elimu ya juu,lakini wanapesa sana,wewe unataka kutuambia waliokosa Elimu,wanakuwa na vipaji/hela,sasa wale vijana machinga waliojaa stendi za mabasi,wanauza pipi,au wale wanaofanya kilimo Cha nyanya,au vijana wa bodaboda,hawana Elimu,sasa mbona hawatumii vipaji vyao kutengeneza pesa?waachane na tabu za dunia.?
Harmonize kabla hajakutana na Mond mbona hakuwa na kitu?au kipaji kilitokea baada ya kuperekwa studio?pesa ikatumika kumjenga
 
Kipaji akiokotwi kama cheti kiazi weweee. Kipaji kinavumbuliwa, kinalelewa ndio unapata star (Musician/ Athletes / Actors/ Actress). Wenzetu wana academy kwa ajili ya kugundua talents za watoto. Hawawekezi kwenye Elimu ya dunia tu kama njia ya kumtoa mtu. Usidhani hao akina Lionel Messi wameingia Barcelona baada ya kumaliza chuo tu. Messi yupo Barcelona tokea akiwa na miaka 13. Ndio utajua aliwekeza wapi zaidi na wapi pana mlipa. Kupitia mpira kwa week anaingiza zaidi ya TZS 750m

Nimetoa mfano wa Platnumz kwa sababu huwa hafichi support aliyoipata kutoka kwa Bi Sandra wakati ana hustle kutoka.
 
Hapo kabla alikuwa analipwa ngapi?
Nyota wa Kikapu nchini Marekani LeBron James amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na Los Angeles Lakers, mkataba wenye thamani ya ($85 million) ambao utamuweka kwenye timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2022-2023.

Kwa mujibu wa ESPN, mkataba huu mpya unamuonesha LeBron James akilipwa kiasi kikubwa cha fedha kwa dakika hadi miaka miwili;

Kwa dakika 1 atakuwa akilipwa ($82) sawa na TSH. 190,158

Kwa Saa 1 atalipwa ($4,891) sawa na TSH. Milioni 11

Kwa Siku 1 atalipwa ($117,397) sawa na TSH. Milioni 272

Kwa Mwezi Mmoja atalipwa ($3.57M) sawa na TSH. Bilioni 9

Kwa Miaka 2 ya mkataba wake atalipwa ($85.7M) ambazo ni sawa na TSH. Bilioni 197
 
Mkataba mpya wa LeBron unaanza msimu wa 2021/22 na kuisha 2022/23.

Msimu huu wa 2020/21 anaendelea na mkataba wake wa nyuma.

Hivyo jamaa bado wako pamoja kwa kiasi kama hakuna atakeyekuwa traded.
Pia Kama hapatakuwepo na serious injury kwa yeyote tutegemee kuona dominance itakayosumbua Kanda zote mbili.
 
Let's hope so, maana mpaka dakika hii hatujui kama Giannis atasaini extension au la.

Maana asiposaini, ujue anatimka msimu ujao. Akidondokea Dallas au Miami inaweza kubadili upepo.
 
Nafikiri GSW Kama watamkosa Harden Basi watamfuata Giannis, na Giannis lazima aondoke maana ana uchu sana wa kucheza fainali, na kule Milwaukee ameshaona hakuna cha ziada amejaribu kadri ya uwezo wake akaishia ECF tu.

Golden State wanataka kurudi msimu huu na kumkosa Klay kwa msimu mzima itawalazimu wasajili mchezaji wa Kariba ya ubingwa.

Lakini pamoja na hivyo kwa mtazamo wangu bado Lakers itabaki kuwa timu sumbufu na kuliko zote.
 
Sina uhakika kama Giannis atataka kwenda GSW, wengi naona wanafikiria Dallas, Miami au Masai - Raptors.

Harden ana miaka 2 Houston ambayo iko guaranteed, alikuwa anaforce trade kwenda Nets, jamaa wamekataa. So, kwenda GSW napo sijui.

Halafu sina uhakika kama GSW wana cap ya kupata mchezaji top.

Naona unamsahau kabisa Kawhi kwenye upinzani.
 
Kuna page ndio niliiyona hiyo speculation ya GSW kumtaka Giannis, sikujua Kama timu zilizo serious ni hizo zingine.

Ila Mimi naona Harden wangemwacha tu akatimka zake Houston, maana sioni Kama ana kitu kipya Cha kuwaongezea. Tumeona ameshindwa kufika fainali akiwa na CP3 tena walikuwa na chemistry nzuri tu, na sasa hivi Napo ameshindwa akiwa na swahiba wake Russell.

Hahaha... Kuhusu Kawhi sioni akileta ushindani wowote seriously kwa huu mpasuko uliopo kwenye timu yake.
FB_IMG_1606951868235.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom