LeBron James asaini mkataba mpya, kulipwa Bilioni 9 kwa mwezi

Ikitokea Giannis akaenda Dallas itakuwa noma mzee, watatisha. Huku Luka, huku KP, huku Greek Freak!

Nachompendea Mark Cuban ni vile anawapenda wachezaji wake na timu kwa ujumla. I think ni one of the best owners.

Brooklyn wanaweza kusumbua kwa East, issue ni kama KD atarudi kwenye ubora maana injuries za namna ile zinakuwa ni mara chache kurudi kwa 100%. Hoping pia kwamba Kyrie hatasumbua kwenye Leadership.
Mavericks Wana muda mrefu sana hawajafika hata WCF nafikiri wakipata mtu wakusaidiana na Luka pale ukiongeza na uchu walionao, watafanya wonders, supporting cast muhimu Sana tumeona LeBron alivyorahisisishiwa kazi baada ya AD kutua Lakers.

Baada ya Lakers kuchukua ubingwa siku chache baadae nilionaTweet ya Charles Barkley, ana mwambia KD ili ajijengee heshima kama LeBron, itabidi achukue ring akiwa nje GSW.

Nafikiri hiyo inaweza ikawa ni chachu kwa KD kurejea kwenye kiwango chake haraka na kujaribu kutafuta hiyo heshima anayosema Charles.
 
Kitendo cha hawa majaa kuwa mafree agents ndio kinaumiza hizi team zingine...James Harden nae angejiondokea tu pale rockets atafute chama lingine la fainali sababu pale anapambana sana ila wanaishia kutolewa daily...
Rockets hawana kipya Cha kumpa Harden na Harden Hana kipya cha kuongeza pale Rockets. Yeye angeondoka tu. Na asipojiongeza atajikuta anatundika daluga bila ring yoyote.

Jamaa yake Russell ameshtuka, sasa hivi anazurura tu, Leo Yuko Washington kaenda kujaribu upepo na B.Beal, ameona akiendelea kukaa Oklahoma ataishia kuvuna hela tu na triple-double, ubingwa atauskia kwenye bomba tu
 
kusema Za ukweli me sielewa kwanini Leonard alienda Clippers me naona kama kaflop hivi
Kawhi kwanza naskia haishi Los Angeles anaishi San Diego, na muda mwingi mazoezi anafanya mwenyewe hafanyi na wenzie.

Dizaini Kama vile ameji-isolate, nafikiri ni kutokana na haiba yake the dude is grogeous in nature. Na hii imepelekea wenzake kuanza kulalamika wanamuona Kama vile anapewa special treatment.

Timu ikishakuwa hivi ni ngumu Sana kuwa na ile fighting spirit ya ubingwa.
 
Nyota wa Kikapu nchini Marekani LeBron James amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na Los Angeles Lakers, mkataba wenye thamani ya ($85 million) ambao utamuweka kwenye timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2022-2023.

Kwa mujibu wa ESPN, mkataba huu mpya unamuonesha LeBron James akilipwa kiasi kikubwa cha fedha kwa dakika hadi miaka miwili;

Kwa dakika 1 atakuwa akilipwa ($82) sawa na TSH. 190,158

Kwa Saa 1 atalipwa ($4,891) sawa na TSH. Milioni 11

Kwa Siku 1 atalipwa ($117,397) sawa na TSH. Milioni 272

Kwa Mwezi Mmoja atalipwa ($3.57M) sawa na TSH. Bilioni 9

Kwa Miaka 2 ya mkataba wake atalipwa ($85.7M) ambazo ni sawa na TSH. Bilioni 197
Kodi ushatoa hapo
 
Kawhi kwanza naskia haishi Los Angeles anaishi San Diego, na muda mwingi mazoezi anafanya mwenyewe hafanyi na wenzie.

Dizaini Kama vile ameji-isolate, nafikiri ni kutokana na haiba yake the dude is grogeous in nature. Na hii imepelekea wenzake kuanza kulalamika wanamuona Kama vile anapewa special treatment.

Timu ikishakuwa hivi ni ngumu Sana kuwa na ile fighting spirit ya ubingwa.

Daaah noma sana aisee
 
NBA DRAFT 2009 ROUND PICK 1

1. Griffin
2. Ndugu yetu
3. James harden
7. Curry

Hawa kina 1, 3, 7 walitakiwa wawe kwene headline na ndugu yetu sababu wanakichafua mpaka leo na watu mpaka wamekuwa maMVP, huyu ndugu najua kilichomponza, badala ya kugombania wanawake na kija jay Z ye anakuja kugombana na Ally kiba wanangombea mheshimiwa wa kisarawe, wenzake kina Ibaka wanakula kina kerry hilson ye anakuja kwa kina hamisa mobeto ? Ndugu yetu alipata bahati akaichezea..tungekuwa tunamwongelea yeye saivi...
 
Watafute shooter mwingine?
Sio kwamba kila mchezaji kwenye high-ranked NBA team anauwezo wa kushoot... Kushoot si ndio kufunga goli kwenye kikapu? Sasa unataka kuniambia timu huwa inamtegemea mchezaji mmoja tu kwenye kufunga? Kweli?
Yes watafute shooter mwingine, yes kwenye hizo high-ranked team kila mchezaji anaweza kushoot na akafunga lakini si kila mchezaji ni mahiri wa kushoot.

Ngoja labda nikwambie kitu kimoja, timu Kama Golden State warriors ni three-pointer over-relient team, yaani ni timu inayotegemea zaidi kupata matokeo kwa kupitia three-points shooting. Na hiyo inahitaji uwe na mashooters mahiri Sana angalau watatu wenye uwezo unalingana au kukaribiana, na si kila mchezaji NBA ana umahiri huo.

Ndio maana tumeona GSW walivyo wakiteseka sana baada ya kuwakosa shooters wake mahiri waliokuwa wanaibeba timu.

ilifika mahali mpaka wakajaribu kuwatumia biggies wakati aina yao ya uchezaji wala hata haitaji Sana kutumia biggies.

Kwa maelezo haya nafikiri tumeelewana.
 
Unamwelewa Klay Thompson?

Pengo lake kwenye shooting hakuna anayeweza kuliziba kwa sasa NBA!
31 points in a single quarter.
6 back to back three-pointer

Jombaa sidhani Kama amemfuatilia kwa ukaribu hasa yule Klay wa 2016. Enzi splash brothers wana zi-splash NBA teams mpaka unaogopa.
 
Yes watafute shooter mwingine, yes kwenye hizo high-ranked team kila mchezaji anaweza kushoot na akafunga lakini si kila mchezaji ni mahiri wa kushoot.

Ngoja labda nikwambie kitu kimoja, timu Kama Golden State warriors ni three-pointer over-relient team, yaani ni timu inayotegemea zaidi kupata matokeo kwa kupitia three-points shooting. Na hiyo inahitaji uwe na mashooters mahiri Sana angalau watatu wenye uwezo unalingana au kukaribiana, na si kila mchezaji NBA ana umahiri huo.

Ndio maana tumeona GSW walivyo wakiteseka sana baada ya kuwakosa shooters wake mahiri waliokuwa wanaibeba timu.

ilifika mahali mpaka wakajaribu kuwatumia biggies wakati aina yao ya uchezaji wala hata haitaji Sana kutumia biggies.

Kwa maelezo haya nafikiri tumeelewana.

GSWs imeshapotea, tutabaki tunaizungumza kwamba iliwahi kutisha na kuvunja records. It was real sweet to watch them competing with the King.

Both Curry and Klay are no longer who they used to be. Sioni yeyote kati yao akiwa na impact kama ya LBJ at their age.

Sasa hivi baada ya Lakers, nadhani tutashuhudia miamba mipya, the likes of Dallas, Phills, NOP, Bucks (if Giannis stays), Boston Celtics, Utah Jazz na Denver.
 
NBA DRAFT 2009 ROUND PICK 1

1. Griffin
2. Ndugu yetu
3. James harden
7. Curry

Hawa kina 1, 3, 7 walitakiwa wawe kwene headline na ndugu yetu sababu wanakichafua mpaka leo na watu mpaka wamekuwa maMVP, huyu ndugu najua kilichomponza, badala ya kugombania wanawake na kija jay Z ye anakuja kugombana na Ally kiba wanangombea mheshimiwa wa kisarawe, wenzake kina Ibaka wanakula kina kerry hilson ye anakuja kwa kina hamisa mobeto ? Ndugu yetu alipata bahati akaichezea..tungekuwa tunamwongelea yeye saivi...
Nafikiri hata yeye mwenyewe akimuangalia mchizi wake James Harden na ile contract ya Adidas ya $200m huwa inamuuma Sana na ukizingatia James Harden aliwahi kumwambia ana tamani sana angekuwa na Height Kama yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom