dropingcoco
Senior Member
- Jun 21, 2008
- 124
- 11
nafikiri zitakuwa na matatizo ya kawaida kama products zingine.....siyo kila chinese product ni mbaya.......angalia unakonunua product. usitarajie ununue HDTV itumike miaka 10 i'll be outfashioned. wabongo do wachakachuaji
Hisense ni kampuni kubwa ya kimataifa ya vifaa nya umeme na elektroniki nchini China. Ni kampuni inayomilikiwa na serikali ya China.Msaada wenu wadau, kuna hizi lcd tv za startimes naziona zipo kwenye promo, kwa yeyote ambaye anaujua utendaji wake atujulishe, zinasemekana zina Hisense technology, kwa anayejua pia hisense ni nini atuelimishe, at least na sisi wengine tujidai na flat screen za bei rahisi
HDTV maana yake ni: High Definition Television.mkuu msaada hapo kwenye red please
HDTV maana yake ni: High Definition Television.
Unakaribishwa...!salam aleykum.....asante kwa kunijulisha haya....hii teknolojia wengine inatumix
Bei zake zinaendana sambamba na zile zingine zenye majina tayari.
zipo kwenye promo, 42" inauzwa 700,000 na 32" I think 500,000
Yap, mwisho trh 31 mwezi huu.
Wakuu nishaurini, nikanunue?
HDTV = High Definition Television.
Ubora wa picha kwa TV ya namna hiyo ni mara 5 zaidi ya TV za Kariakoo.
Kama ni soka, basi utaona kila kitu kama vile uko uwanjani.
Actually size wanazouza kwa promo ya sasa ni 32" kwa 700,000/= na si 42", pia 26" kwa 500,000/=.
Mtu angeniuliza nimshauri anunue au la... ningejibu:
- Zina kingamuzi (decoder) ya Startimes hivyo hauhitaji kununua decoder kwa ajili ya Digital TV. Zina option pia ya kuweka kadi za DSTV hivyo hulazimiki kununua decoder ya DSTV, utahitaji Dish tu. Ila kwa masafa ya Startimes huhitaji dish, antennae ya kawaida inatosha (Huwa wanauza pia kwa gharama nafuu nadhani around 50,000 au 30,000).
- Zina uwezo wa kuunganishwa na computer zikatumika kama screen. Kwa kawaida hazina resolution kubwa sana kiasi kwamba uzitumie kwenye kompyuta kwa kazi za typing. Ila kwa kutazama movie, video editing supa dupa.
- Zina connections nyingi (Nyingi sana ukilinganisha na TV nyingi utazokuta dukani):
- USB, nimeambiwa unaweza kuunga external hard disk, kama ina videos au audios basi we ni kuziplay tu, full kujiachia (Ila sijathibitisha hili) ila ni kweli zina USB.
- Zina connection ya S-Video kwa ajili ya Deki za DVD au kompyuta au Camera au kifaa chochote chenye uwezo wa S-Video. S-Video huwa na picha bora zaidi kuliko VGA (Ukiitumia kama screen ya kompyuta).
- Zina HDMI Connection kwa ajili ya Deki za DVD au kompyuta etc zenye connection hii, baadhi ya laptop za kisasa zina HDMI. HDMI ina ubora wa picha kuliko S-Video na VGA.
- Zina Audio output kwa ajili ya subwoofer etc.
- Ni HD Ready, kwa ubora wa picha kuliko screen za kawaida.
- Screen yake ni Gloss kiasi kwamba kiasi kwamba inaonesha picha vizuri hata kama kuna mwanga wa jua. Haififii.
- Ni nyeusi kwa rangi.
- Zimetengenezwa na kampuni ya Hisense ya China. Hisense inatengeneza bidhaa nzuri na bora.
"Kwanini hujanunua hadi sasa?"
Kama kuna swali nakaribisha. Nitajitahidi kujibu kwa lugha rahisi.
asante mkuu kwa kutuelewesha vizuri kabisa.....swali lilikuwa niulize kama nitaweza kutumia dstv lakini umeshajibu , ila niulize....kwa hiyo sitahitajika kununua decoder ya dstv? nimesikia hizo zina inbuilt decoder zao how come dstv iingie hapo?
Hisense ni kampuni kubwa na ipo mpaka USA.Msaada wenu wadau, kuna hizi lcd tv za startimes naziona zipo kwenye promo, kwa yeyote ambaye anaujua utendaji wake atujulishe, zinasemekana zina Hisense technology, kwa anayejua pia hisense ni nini atuelimishe, at least na sisi wengine tujidai na flat screen za bei rahisi
Hisense ni kampuni kubwa na ipo mpaka USA.
Hisense USA - Top Rated - Consumer Electronics and Home Appliances. Ukiona kampuni imekubalika mpaka USA ujue lazima ina quality products kwani jamaa hawawezi ingiza bidhaa za hovyo.
Pia jaribu soma hapa Don't Fall Into These HDTV Buying Traps - Yahoo! Shopping upate mwanga kidogo jinsi ya kuchagua hivi vitu.