Lazima ujue si wewe tu

Lazima ujue si wewe tu

Joined
Aug 8, 2013
Posts
29
Reaction score
16
Habari ndugu zangu wote , najua mko poa kabisa na hata wenye changamoto pia niwaambie kuwa tuko pamoja sababu ndo maisha yalivyo ila tu tutafute njia ya kujitoa huko kwenye matatizo kama zipo ndani ya uwezo wetu .

Kuna baadhi ya vitu vinavyo endelea katika jamii ambavyo si vigeni saana nikiwa na maana kama hakija kukuta wewe basi umewahi kushuhudia au kusikia limetokea sehemu .


Rafiki yangu mmoja alinisimulia stori fupi kuhusu maisha yake ( Aliishi vizuri na wazazi wake waliokua na uwezo kiasi alikua mdogo lakini wazazi wake walisaidia ndugu wengine pia katika masomo yao wakafanikiwa maisha wazazi wake walifariki akiwa bado yuko shule hivyo kupelekea hali kua ngumu zaidi akawa anajiweka karibu na wale waliosaidiwa na wazazi wake lakini walimnyanya paa na kumsema akafeli na kushindwa kuendelea na masomo , wakamwambia hayupo serious na mambo yake ndio maana ameshindwa shule bila kutafakari kua kuna vitu havipo sawa katika akili yake iliyo pelekea kushindwa lakini akakubali lawama , akaanza upya maisha ya kufanya kazi angalau apate chakula kutokana na elimu yake ndogo ambayo alishindwa kusoma , wakasema muda unaenda utafanya kazi za ajabu hadi lini tafuta kazi nzuri ! Alishangaa sana wapo waliokua wanamshangaa anavaa vibaya eti anawaaibisha kwa jamii wana sahau hana kipato kizuri na labda wazazi wake wasinge wasaidia wao wangeweka akiba nayeye angesoma vizuri ili naye apate hsyo wanayo yataka wao )
Mimi nikamwambia dunia hii ndio ilivyo leo watakucheka lakini labda watakuja kujua baadae kua shida hakuna aiombae , cha msingi ni kukaza na kupambana kwa hali yoyote ile fanya bila kukata tamaa ili ufikie malengo .

Nimemwambia kuna watu sasa hivi yupo anatafuta figo , mwingine anataka mtoto tu ila kapewa kila kitu na mungu , mwingine haolewi ila ni mzuri anapesa zake lakini ndo hivyo wanaume hawamuoni , mwingine karisishwa uchawi na wazazi na hawezi kujitoa atakufa .

Wewe si wa kwanza katika dunia hii pambana hadi mwisho anakwambia ni mchafu sababu yeye anapendeza .
Anaye kuambia mgumba kwa sababu yeye anazaa .
Anaye kuambia masikini sababu yeye tajiri usiogope piga kazi tafuta njia ya kujitoa kama inawezekana !
 
Safi sana
Cha muhimu endelea kumpa suport

Lakini na ww hutakuwa mtu wa kwanza kusalitiwa na mtu uliye simama naye wakati wa shida endapo kama jamaa atasahau fadhila zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom