Lawrence Masha na Miriam - Kashfa

Mambo ya ndani ya ndoa ya Masha hatuyajui, kama yeye na mkewe wana makubalinao flani hatujui, lakini ninawajua wananchi wengi hapa Darsalama, wanaoishi maisha ya open ndoa, na kuishi pamoja kwa ajili tu ya watoto wao, kuna wengine mashoiga na wana wake na watoto,

Masha ni mtu mzima na mwenye akili timamu na msomi pia aliyebobea na ni mwanasheria mzuri sana kati ya wachache sana tulio nao bongo, eti at this time and moment of his life tunaweza kumfundisha what is right na what is wrong? Tena waziri wa mambo ya ndani? Eti wewe mkuu unamjua vizuri mkewe?

Eti ni makosa kwa M-Tanzania kwenda Rosegarden kwa sababu tu ya kazi yake? Kwa sababu amesema nani? Kama hizi habari ni za ukweli na ni njema sana mbona waliozileta hawakuzileta kwa majina yao hasa wanayoheshimika nayo humu forum? Hivi kwa nini mnapenda kujifanya wajanja wakati ni wajinga? Hivi ni kwa nini mnapenda kuwafanya watu hapa forum kuwa ni wajinga sana na ninyi tu ndio wenye akili? Wewe unaamini kuwa una hoja hapa kwa nini unatuzunguka na majina kwa nini usisimame na jina lako hasa unalotumia hapa? Wanaleta udaku hapa halafu wanakimbia na kuangalia kwa pembeni huo ndio ujanja?

Wakuu again ninaomba mtuambie Masha ametumia hela ngapi za serikali kuhudumia huyu kimada? Msitupotezee muda hapa, kama kuwa na kimada ni vibaya sana basi tubadili katiba badala ya kujaribu kuharibu majina ya viongozi humu kwa sababu za wivu na chuki zisizokwisha!

Kaka maswala mengine haina haja ya kujiingiza. Hili la Masha unalijua kabisa na hata hali yake kindoa unaitambua na nini sababu na hata athari za hali hyo unazijua. Sasa ukiwa kama mtanzania unaoumizwa na uozo wa viongozi wetu na kama rafiki wa karibu wa Masha ni bora ukajinyamazia ukainua simu na kumwambia kwa upole tu....Kaka hii sio jitahidi kubadilika.....lakini sio kujaribu kuhalalisha uozo huu wa kimaadili ambao unajua wazi hasara zake kitaifa na kifamilia pia.

Kumbuka tukiwa kama vijana tunapaswa kusimamia Tanzania tuitakayo na sio hii tunayorithishwa na wazee wetu iliyojaa uozo kiasi hiki ambapo tunalzimika kujidanya kuwa uozo wa kimaadili wa viongozi wetu hauna uhusiano na uozo wa kiuongozi kwa taifa letu.

Uongozi bila ya uthabiti wa maadili binafsi sio uongozi bora tunaopigia kelele hapa kila kukicha.....

Onyesha urafiki wa kweli kwa Masha kwa kumwambia wazi kuwa anaharibu kwake binafsi, kwa familia yake lakini zaidi kwa ndoto za watanzania walio wengi walizonazo juu ya viongozi wa kizazi kipya kama yeye.

Bila ya kushughulikia ufisadi wa kimaadili kamwe hatuwezi kushughulikia ufisadi wa kiutendaji, kifalsafa na zaidi ufisadi wa kiuchumi....

Kama kiongozi anaweza kutoithamini familia yake na kama anaweza kumsaliti anayelala naye kitanda kimoja hivi unategemea nini kwa mamilioni ya watanzania anaowapita huku kajifungia ndani ya AC ya gari la mamilioni? Kama anaweza kusaliti kiapo chake cha kuheshimu ndoa yake kwa mungu anayemwamini tangia utotoni mwake hivi atashindwa vipi kusaliti kiapo alicohotoa mbele ya Rais asiye na imani naye, Spika asiyekubaliana naye ama hata mamilioni ya watanzania asio wajua?

Tanzanianjema
 
bwana mdogo tangu mchonga hadi mugwana wana mabibi wa nje hiyo ni sera ya serikali yako nyerere alikuwa mtu wa mabibi tu,unasikia na misifa kemukemu mnamwaga

Hilo halina maana kuwa ufuska sio tatizo kwa taifa letu......ni tatizo kubwa mno na kama mtu ana interest na public office ni muhimu kulitambua hilo na kulifanyia kazi ili kupunguza uozo tulionao sasa.....

Tanzanianjema
 
haya mabo huwa hayana nafasi kwenye nchi zetu kila mtu ana boriti lake kwa hiyo tuachane an kibanzi cha masha.

Anapokuwa kiongozi wa kijamii ama kisiasa hicho hakiwi tena kibanzi chake pekee bali cha jamii nzima. Hata kama tunavijiboriti vyetu, kushindwa kujitoa hakuna maana tuhalalishe uozo wa kimaadili. Kama ulivyo uozo mwingine, Ufuska (zaidi wa viongozi wetu)ni tatizo kwa nchi yetu na hatupaswi kuendelea kurasimisha uozo huu.

Kitaendelea kuwa kibanzi chake pale tu atakapojivua jukumu la kuwaongoza watanzania katika kuelekea kwenye Tanzania tunayoitamani na sio kutupeleka pabaya zaidi ambako wazee wetu ambao wengi walifanya makosa kama yake wametufikisha....

Tanzanianjema
 
Watu bwana, hakika tunafikira zilizo tofautiana mno.
wengine ati tunamsema Masha, ilhali nasi tumo pamoja naye, wengine tunamtetea utafikiri ayafanyayo ni sahihi
Yangu macho.......
 
tanzania njema, sidhani kwasababu jina lako liko hivo nikuwa tanzania ndo ilivyo njema, kashfa ni kashfa, hao ndo viongozi waliosema kuwa vitu kama bay watch night visionyeshwe kwenye tv wakati wao wanaongoza kwa tabia zilizooza(sorry to say that) it is the truth. na maadili ni maadili tu, mda upi wanaoupata kushinda na hao vimada,familia, ndugu, marafiki, unajua wanapata wapi mda wa kuudumia taifa, au ukiwa kiongozi unapata 35 hours a day unlike us who get 24 hours a day? au hawalali? mh? utu uzima ungekua uungwana(kama the late jkn) tungekua mbali sana nchi yet, au kwa vile we nitajiri? je unajali maskini, je unajali familia za hao wasichana ambao watpewa tu magari na magonjwa juu, je tuna solve tatizo? ulikuepo wakati mke wake na huyo mheshimiwa( hivi nani anawaita waheshimiwa?) walivokubaliana juu ya open relationship...je aliwa include watoto kwenye hilo jambo? haujui watoto are the most affected ones? it all comes to being selfish, kutoridhika kunaleta ufisadi- they are simple psychology which relate to each other....
 
ushauri wa bure kwa ndugu yangu Lau:political future yako ni angavu,you are smart and knowledgable,lakini wallah hili la wanawake kisiasa litakumaliza.nasikia kuna wakati unakaa level 8 kempinski uko mbwi na kufanya mambo ambayo hayastahili.wanaokusema humu si wote wanakuchukia,wengine wanakupenda na wangependa ufanikiwe.to start with achana na makundi ya Rose Garden yatakuharibia,tulia kama Ngeleja utafika mbali.
Bishanga, inaonekana ushauri wako haukuzaa matunda kwa wahusika hawa wawili, haswa huyo wa kwanza!
 
Last edited by a moderator:
ushauri wa bure kwa ndugu yangu Lau:political future yako ni angavu,you are smart and knowledgable,lakini wallah hili la wanawake kisiasa litakumaliza.nasikia kuna wakati unakaa level 8 kempinski uko mbwi na kufanya mambo ambayo hayastahili.wanaokusema humu si wote wanakuchukia,wengine wanakupenda na wangependa ufanikiwe.to start with achana na makundi ya Rose Garden yatakuharibia,tulia kama Ngeleja utafika mbali.
Ngeleja hakua ametulia, wewe humjui tu.... kama kipimo ni rose garden sawa, lakini kama ni kupora wake then huyo uliemtaja yuko juu ya lau:alien:
 
Jamani kuwa mpenzi wa pembeni wa kumpooza siku moja moja siyo tatizo,pia ni mpenzi wake wa siku nyingi.
Mwacheni afanyekazi zake hela alikuwa nayo hata kabla ya kuwa waziri. Tusimwonee wivu. cha msingi anafanyakazi bila tatizo.
Mwanaume gani anaweza KUSIMAMA na kusema hajawahi kucheat hata siku moja either kwa mkewe au girlfriend wake?

Mfano mdogo sana: Fikiria unapopata girlfriend mpya kabla hujamwamcha uliyenae huwa hu-cheat???????????

kumbeee?
 
This's the kind of jamii forums I was introduced to....THE REAL GREAT THINKING, SMART ANALYSIS, USABLE TOPIC, GREAT,SMART THREADS... na siyo hii ya siku hizi. I MISS THE OLD JF!, ahhhhhhhhhhhhh!
 
Back
Top Bottom