Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.
Sidhani kama unasema kweli - yawezekana si mwananachma kwa maana ya kuwa na kadi lakini kwa post zako ni wazi u mpenzi wa CCM. Unaumia unapoona chama chako kipenzi kinapata lawama lakini hujiulizi kwa nini lawama hizo zisiwe halali yao. CCM imepewa dhamana ya kulinda na kusimamia maslahi ya taifa, sasa hayo maslahi yanapohujumiwa Exaud J. Makyao unataka tumtafute mchawi nje ya CCM, kwa nini ?
Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?
Taifa limepiga kambi kwenye bonde la kashfa na umasikini na CCM kikaomba ridhaa ya wananchi kulikwamua taifa na wakapewa. Miaka karibu hamsini baadaye bado tumejaa tele humo humo na hakuna dalili ya kuhama. Wakati hao waliopewa dhamana wanakula mabilioni kulinda nyadhifa zao, masikini Watanzanaia wanazidi kudidimia, Exaud J. Makyao hilo halioni - anauliza kwa nini CCM inalaumiwa !
Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?
Raisi na makamu wake ni CCM, Mawaziri wote wa jamhuri ni CCM, Wakuu wa mikoa wote ni CCM, Wakuu wa wilaya zote ni CCM, Wakuu wa idara na taasisi zote nyeti za serikali ni CCM, Wawakilishi wa wananchi kwenye baraza la taifa (Bunge) zaidi ya asilimia 80% yao ni CCM - sasa ndugu yangu Exaud J. Makyao unataka tumlaumu nani ?
Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .
Unachanganya mambo hapa, tunayolilia ni wao kutimiza wajibu, ndivyo inavyotakiwa na hapa hawana haki kudai sifa kwa kuwa wanatimiza wajibu. Kwa kuwa wanakusanya kodi kama watajenga barabara huo ni wajibu - ndio maana waliomba kura. Kufanya hivyo si hatimiliki ya CCM kuhusu utawala bora -
good has never been enough where better is possible. Lakini wakiboronga kama wanavyoendelea kufanya je, Exaud J. Makyao unatwambia tusiwalaumu kweli ?
Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.
Bahati mbaya ni kuwa ni itikadi moja tu ndiyo imekuwa madarakani na kila siku wanajizatiti kunga'ng'ania madarakani. Wamefunga milango yote ya kuingiza hewa safi na wako tayari sote tufie humo humo kwenye uozo. Exaud J. Makyao yawezekana hii hewa chafu imekuathiri kiasi cha kushindwa kutambua kuwa huko nje ya CCM kuna hewa safi. Balaa ilioje kuwa watu wa aina yako mko wengi na itachukua zaidi ya mapinduzi kuwazindua usingizini.
Ustaarabu unatwambia kwamba kama wajibu unakushinda, kubali ukae pembeni, mwachie mwingine ajaribu. Lakini hivi sasa tunashuhudia CCM isivyokuwa tayari kupisha wengine na wanatumia hadi nguvu isiyo ya kawaida kung'ang'ania huku uwezo hawana. Exaud J. Makyao, haya huyaoni ? Matokeo yake kila kukicha wanazidi kuharibu huku ustaarabu wa kuwajibika hawana. Kalaghabaho !