Law School ni jipu

kwa uzoefu niliyokuwa nao ndo nmegunduwa kuwa low schools kweli kuna matatizo, na matatizo hayo ya law schools yanabebwa mpaka kwa wanafunzi waliofanikiwa kumaliza chuo wakapata cheti. Nimesoma law semester 2 , semester 1 mpaka tukagoma kumkataa mwalimu wa law, alikuwa na shida hata mwalimu mwingine naye alikuwa ni shida pia.
 
Nimesoma malalamiko ya wanafunzi wa Law School katika gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki siku ya jumanne na kustushwa sana na habari zile. Kati ya maombi 5,000 au sita ya kujiunga na shule ni maombi 500 tu yanayoweza kujiunga na chuo na kati ya hao ni 70 pekee wanaoweza kupata cheti kwa mwaka.

Kwa maoni yangu kati ya fani nyingi wanazosomea vijana hii ndio fani nyepesi kujiajiri lakini inapowekewa vikwazo vya jinsi hii inafaa tujiulize ni nini hasa lengo kuhusu mustakabali wa serikali na ajira za vijana iwapo utawapiga pini hata wale ambao hawatasumbua kupigia kelele ajira za serikalini na mashirika yake.

Pia fani ya sheria inahitajika sana katika kusaidia haki itendeke katikati ya jamii kwa wenye tuhuma au uhitaji mwingine kupata uhudumu wa mawakili na vilevile kuongeza na kuimarisha taasisis za utoaji haki kama vile mahakama, nk. sasa wachache wanapoamua kuibana fani ili wanufaika wawe wachache sidhani kama hiyo ni nia ya kufikia lengo jema.

Vyuo vya elimu ya juu vimeruhusiwa kisheria kuwa vingi, wahitimu ni wengi pia hivyo kuwabana warande mitaani kwa zaidi ya miaka saba au nane wakisubiri kujiunga Law school na miaka mingine kama hiyo kupa cheti cha uwakili ni jambo la kusikitisha na kushangaza sana.

Hebu serikali ilipatie ufumbuzi hili kwa kupanua Law School na/ama kuruhusu watu binafsi kusajili shule kama hiyo kuondoa tatizo hili na pia iwadhibiti hao wanaotaka kuhodhi fani ya sheria na kuifanya ya wateule; mbona hapo mwanzo haikuwa hivyo na mawakili wote wazoefu walioko sokoni na majaji ni bora sana na hawakuwa wakipitia Law School? Hii shule ni mzengwe wa kubana na kukomoa vijana wetu waliosomeshwa kwa gharama kubwa? hivi Taifa letu limeendelea kiasi hiki kuweza kupuuza nguvu kazi ya maana kama hii?

Law School of Tanzania is simply an extension of UDSM COLLEGE OF LAW,
Its shrouded by caboodle of swindlers who work very hard in disgracing legal education in the country.
I remember in early 2005 Professor Mukoyogo wanted the law school program itinerant: Meaning that the Bar Exam would be moving from College to College henceforth all worthy students would be enrolled as advocates.

I understood his stance, perhaps this could have been the best approach to churn up the best upcoming lawyers in the country.
The Kenyan Council of Legal Education is trying to work this out.
 
Mtu mwenye akili hatoi mapovu kama haya; hao majaji na mawakili wazoefu waliopo sasa walipita Law School? mapovu yako haya yanatoa solution ya hoja iliyotolewa au ni hoja mpya? Leta ufumbuzi wa tatizo kama unao; watu wasome miaka minne watoke na first class vyuoni chini ya uangalizi wa professor ndio unaona wanalilia kubebwa? maelfu yote hayo ya first class ni feki? jibu hoja acha kuongea pumba
Alternative ya Law School ilikuwa ni kufanya Petition kwa CJ moja kwa moja ambapo screening ilikuwa ni ile ile! Acha kulilia goal post iongezwe upana bali fanya mazoezi ili ufunge magol!
 
Ukimtoa Peter Maina, Ringo na Shivji hivi kuna lawyer gani amefanya mambo makubwa kimataifa kwa kipindi hiki?
Nitajie hata watano tu?

Ni aheri hata ungemtaja Dr Rugemeleza alijetolea kushirikiana na Mkono kushinda ile kesi ya DAWASCO ambayo serikali ilishinda. Unaachaje kumtaja prof Luoga kwenye kuisaidia serikali katika sheria za kodi?
 
Ukimtoa Peter Maina, Ringo na Shivji hivi kuna lawyer gani amefanya mambo makubwa kimataifa kwa kipindi hiki?
Nitajie hata watano tu?

Na zaidi ni kuwa Maina kafanya kazi kwenye Human Rights hata Shivji pia. Kuna wengine kama prof Fimbo alifanya mengi kwenye Land law. Pia kuna prof Kanywanyi kafanya mengi kwenye sheria za biashara. Ila pia penda usipende prof Kabudi na Majamba ni vichwa hatari! Extremely intelligent.
 
Ni aheri hata ungemtaja Dr Rugemeleza alijetolea kushirikiana na Mkono kushinda ile kesi ya DAWASCO ambayo serikali ilishinda. Unaachaje kumtaja prof Luoga kwenye kuisaidia serikali katika sheria za kodi?

Nimesema nitajie kazi zao kubwa zianazojulikana kimataifa.
 
Na zaidi ni kuwa Maina kafanya kazi kwenye Human Rights hata Shivji pia. Kuna wengine kama prof Fimbo alifanya mengi kwenye Land law. Pia kuna prof Kanywanyi kafanya mengi kwenye sheria za biashara. Ila pia penda usipende prof Kabudi na Majamba ni vichwa hatari! Extremely intelligent.

Nimesema nitajie maprofesa au madaktari wa sheria watano hapo Mlimani wanaofahamika kimataifa.
Na kazi zao kubwa ambazo zimesaidia dunia.
 
Nimesema nitajie maprofesa au madaktari wa sheria watano hapo Mlimani wanaofahamika kimataifa.
Na kazi zao kubwa ambazo zimesaidia dunia.

Hebu ongea kama unaelewa hivi vitu vizuri. Kuna baadhi ya masomo tena machache ndio yana general application kama human rights, Puplic international law etc hivi unataka Mwalimu wa Probate au Land awe na mchango kwa dunia nzima?
 
5,000 au sita ya kujiunga na shule ni maombi 500 tu yanayoweza kujiunga na chuo na kati ya hao ni 70 pekee wanaoweza kupata cheti kwa mwaka.

.. pass/graduation rate ya 15% ni aibu hata kwa hao wanaowafundisha. Law ni course rahisi mno! Harvard Law School, kwa mfano mwaka jana (2015) walikuwa na graduation rate ya 98%.
 
Hebu ongea kama unaelewa hivi vitu vizuri. Kuna baadhi ya masomo tena machache ndio yana general application kama human rights, Puplic international law etc hivi unataka Mwalimu wa Probate au Land awe na mchango kwa dunia nzima?

Kwanini wasiwe na mchango?
Hivi, hivyo vitabu vya Law of Torts, Probate Law , Civil Procedure Law na hata Constitutional Law unasoma vya Watanzania tu?
 
.. pass/graduation rate ya 15% ni aibu hata kwa hao wanaowafundisha. Law ni course rahisi mno! Harvard Law School, kwa mfano mwaka jana (2015) walikuwa na graduation rate ya 98%.

Pass rate ni zaidi ya 15% ila pia mkuu kuna tofauti kubwa sana kati ya wanafunzi wa hapa na huko ulikotaja.
 
Mtu mwenye akili hatoi mapovu kama haya; hao majaji na mawakili wazoefu waliopo sasa walipita Law School? mapovu yako haya yanatoa solution ya hoja iliyotolewa au ni hoja mpya? Leta ufumbuzi wa tatizo kama unao; watu wasome miaka minne watoke na first class vyuoni chini ya uangalizi wa professor ndio unaona wanalilia kubebwa? maelfu yote hayo ya first class ni feki? jibu hoja acha kuongea pumba
HIYO YA MAELFU YA FIRST CLASS NI KALI NA INATISHA! YANAPATIKANA WAPI HAYO MAELFU NAMI NIKACHUKUE MOJA?! HATA HIVYO WANAFUNZI KUFAULU 70 KATI YA 500 SIYO TATIZO LA CHUO! WANASOMA WATU WAZIMA. SASA MTU MZIMA UFELI HALAFU UTUPIGIE KELELE HAPA! LST INA AWAMU KARIBU TATU KWA MWAKA, BADO NI WANAFUNZI 500 TU HAO?!
 
Kwa hiyo hizo awamu tatu zinahitimu kila moja baada ya miezi minne au?
 
Back
Top Bottom