salimkabora
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 2,441
- 652
Nimesoma malalamiko ya wanafunzi wa Law School katika gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki siku ya jumanne na kustushwa sana na habari zile. Kati ya maombi 5,000 au sita ya kujiunga na shule ni maombi 500 tu yanayoweza kujiunga na chuo na kati ya hao ni 70 pekee wanaoweza kupata cheti kwa mwaka.
Kwa maoni yangu kati ya fani nyingi wanazosomea vijana hii ndio fani nyepesi kujiajiri lakini inapowekewa vikwazo vya jinsi hii inafaa tujiulize ni nini hasa lengo kuhusu mustakabali wa serikali na ajira za vijana iwapo utawapiga pini hata wale ambao hawatasumbua kupigia kelele ajira za serikalini na mashirika yake.
Pia fani ya sheria inahitajika sana katika kusaidia haki itendeke katikati ya jamii kwa wenye tuhuma au uhitaji mwingine kupata uhudumu wa mawakili na vilevile kuongeza na kuimarisha taasisis za utoaji haki kama vile mahakama, nk. sasa wachache wanapoamua kuibana fani ili wanufaika wawe wachache sidhani kama hiyo ni nia ya kufikia lengo jema.
Vyuo vya elimu ya juu vimeruhusiwa kisheria kuwa vingi, wahitimu ni wengi pia hivyo kuwabana warande mitaani kwa zaidi ya miaka saba au nane wakisubiri kujiunga Law school na miaka mingine kama hiyo kupa cheti cha uwakili ni jambo la kusikitisha na kushangaza sana.
Hebu serikali ilipatie ufumbuzi hili kwa kupanua Law School na/ama kuruhusu watu binafsi kusajili shule kama hiyo kuondoa tatizo hili na pia iwadhibiti hao wanaotaka kuhodhi fani ya sheria na kuifanya ya wateule; mbona hapo mwanzo haikuwa hivyo na mawakili wote wazoefu walioko sokoni na majaji ni bora sana na hawakuwa wakipitia Law School? Hii shule ni mzengwe wa kubana na kukomoa vijana wetu waliosomeshwa kwa gharama kubwa? hivi Taifa letu limeendelea kiasi hiki kuweza kupuuza nguvu kazi ya maana kama hii?