1 Wakorintho 6
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.
Yoshua Bin Sira: 31:25 31, 40:20
25) Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa kileo (pombe), yaani mvinyo,
Imewaangamiza wengi.
26) Tanuru hujaribu kazi ya mhunzi, na mvinyo mioyo ya watu, katika ugomvi wa wenye kiburi.
27) Kwa wanadamu mvinyo ni kama maji ya uzima, ukinywa kwa kiasi. Je, anao uzima gani mtu asiye na mvinyo? Nayo imeumbwa ili kuwafurahisha wanadamu.
28) Mvinyo ni furaha ya moyo na changamko ya roho, ikinywewa kwa wakati wake na ya kutosha.
29) Lakini kunywa mno ni uchungu wa roho, na fedheha, na ugomvi.
30) Kileo humzidishia mpumbavu mitego ya kumletea hasara; hupunguza nguvu, na zaidi huleta jeraha.
31) Usimkaripie jirani yako kwenye karamu ya mvinyo, wala usimdhihaki anapocheka, wala usimwambie neno la shutumu, wala usimnyenye kwa kutaka alipe deni.
40:20 - Kunywa mvinyo na kuimba kunachangamsha moyo, na upendano wa rafiki hupita yote.
Isaya 5:22
Ole wao walio hodari wa kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo.
Mithali 20:1, 23:29-32, 31:4-5,6,7
Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
Ni nani apigaye Yowe? Ni nani aliaye Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo, waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
Usiitazame mvinyo (pombe) iwapo ni nyekundu, iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
Mwisho wake huuma kama nyoka, huchoma kama ----.
Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme
Wala haifai wakuu waseme Ki wapi kileo?
Wasije wakanywa na kuisahau sheria, na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea, kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
Anywe akasahau umaskini wake, asiikumbuke tena taabu yake.
Waamuzi 9:13
Huo mzabibu nao ukaiambia, Je, niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayongeyonge juu ya miti?
Zaburi 104:15
Na divai imfurahishe mtu moyo wake; aungaze uso wake kwa mafuta, na mkate umburudishe mtu roho yake.
Mhuburi 10:19
Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, na divai huyafurahisha maisha, na fedha huleta jawabu la mambo yote.
----------------------