Laptop yangu inatatizo sugu kwa siku tatu sasa

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Laptop yangu aina ya DELL Latitude E6410 imenigomea kuwaka toka ijumaa ya week hii.

Nikiiwasha inaandika "Automatic Repair" ila cha ajabu inaganda hapo hapo.Baada ya muda mfupi Screen inakuwa nyeupe then itakaa hivyo hata masaa 6 then itanipa options 3 ,
1.Continue with window 8.1
2.Troubleshoot
3.cancel

Ila nikibonyeza option yoyote kati ya hizo itanirudisha kule kule Kwa "Automatic Repair" then mchezo unakuwa ni mzunguko ule ule.

Nimejaribu kuwaambia marafiki zangu wenye utaalamu zaidi hapa chuoni wakanishauri niweke Window tena,ila sasa napoweka huo window mpya hutumia zaidi ya masaa 5 kuongezeka asilimia moja tu ya kipengelewe cha kwanza wakati wa kupiga window.Ni kipengele kiitwacho "Extracting Window files"

Wakuu nilijitahidi kuvumilia zaidi ya siku moja mpaka Leo naamka asubuhi naambiwa ili fail ikiwa na 59%.

Nikajaribu kuuliza upya kuwa tatizo inaweza kuwa nini .? Nikajibiwa "HDD yako imekufa"

Sasa wakuu kinachonitisha zaidi ni Kuwa wakati napiga window baada ya kuelekezwa na mtaalamu nilikuwa Naona partitions za HDD yangu.So kama HDD mbovu mbona ilikuwa inaonekana kwenye window?

Na kama window uli corapse ilikuwaje nikapewa option number 1 kuwa niendelee na Window 8.1?

Wakuu naamini JamiiForums kuna wataalamu zaidi hivyo nimeleta hili tatizo kwenu kuomba msaada.

Ni hayo tu.
 
hapo inaonekana kama ipo slow sana HDD yako, kama upo comfortable unaweza ukaitoa na kumuomba mtu mwenye external akuazime kasha lake kisha ieke kwenye external hio hdd na kuitest kwenye machine nyengine kama inafanya kazi kama kawaida. jaribu kuhamisha mafile uone speed yake.

sometime kuiformat kunaweza solve tatizo na windows ikaingia, sema data zako zitapotea, au inawezekana ndio inaharibika hivyo hdd yako.
 
Press button F12 mara nyingi , kisha nenda Bios Setup Click Enter, System Configuration, SATA Operation utaona Option 4 Disabled, ATA, AHCI, IRRT. Wewe mark AHCI. Kisha ushuke chini Click Apply. Subiri Seconds 10 Kisha click Exit Button. Itajiwasha na kurudia hali yake. Ukikwama ni PM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom