Nimefufua laptop yangu kwa kutumia Ubuntu

Nimefufua laptop yangu kwa kutumia Ubuntu

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,932
Wiki chache zilizopita laptop yangu ilishindwa kufungua windows 8.1 baada ya laptop yenyewe kufanya update. Niljaribu kila njia kuifufua lakini ikashindikana. Kibaya zaidi ni kuwa laptop hiyo nilipoinunua haikuja na CD ya Windows na vilevile sikuweza kushusha windows ningine kutoka mtandaoni. Kama nilitaka kuendelea kutumia Microsoft Windows, ilibidi ninunue na kushusha nyingine kutoka kwenye mtandao, na mimi sikuwa tayari kufanya hivyo.

Baada ya kufanya utafiti nikaamua kuweka Ubuntu kwenye laptop yangu. Nilifanikiwa kufanya hivyo na mpaka sasa ndio naitumia katika laptop yangu. Faida za kutumia Ubuntu ni kuwa inapatikana bure tofauti na Microsoft Windows, na unaweza kutumia hata katika kompyuta za zamani kama zile zilizokua zinatumia Windows XP ambayo Microsoft kwa sasa hawatoi huduma. Nimefanikiwa kufufua laptop yangu iliyokuwa inatumiaWin XP kwa kuweka Ubuntu.

Kwa wale ambao wangependa kujua zaidi kuhusu Ubuntu watembelee hapa The leading OS for PC, tablet, phone and cloud | Ubuntu na wale ambao wanataka kuishusha kutoka mtandaoni inapatikana hapa Download Ubuntu Desktop | Download | Ubuntu
 
Security yake ikoje Ubuntu when it comes to virus?
Is it the same as Mac OS?
 
All in all hauwezi mconvince mtu aache windows atumie Ubuntu labda kama wewe ni wale users wa kutumia tu browser,skype na office softwares...

Pamoja kwamba Ubuntu ina Wine kwa ajili ya ku run windows s/w na hata kama hai freeze freeze kila mara na kwa mambo ya security anti virus haiitajiki kivile bado watu watazidi kuipenda Windows OS kwa sababu ya urahisi wa kuitumia...
 
labda niweke kama OS ya pili au kwa ajili ya kujifunza siwezi acha kutumia windows then nikahamia ubuntu
 
labda niweke kama OS ya pili au kwa ajili ya kujifunza siwezi acha kutumia windows then nikahamia ubuntu

Ni hiari yako kutumia Windows na hiyo pia inawezekana. Nangojea Windows 9 itoke niiweke sambamba na Ubuntu.
 
hiyo niliweka...kama OS...Ya pili ..
Niliitumia sikuona raha yake...kivile..ingawa..kuna faida...zake...kama hiyo ya free in virus...
 
Now using ubuntu na taratibu nshaanza kuimaster libre office ipo kama ms office tu na GIMP ipo kama photoshop tu so im enjoying with ubuntu..
 
Ubuntu ni kwa watu wanaotaka kuelewa how computer really works behind the scenes na mostly inatumiwa na madeveloper/Programmers kwasababu kwenye linux OS tunacheza na command lines tu na iko very secure. Windows ni kwa watu wakawaida tu wanaotaka kubrowse internet na wenye uelewa kidogo wa computer. Windows is very vulnerable na ndio maana cybery criminals, botnets wanatarget window uses mostly.
 
Ila pia kuna DoS attacks huwa zinapigwa kwenye linux servers
 
bwana Dingiswayo next time angalia kwenye laptop yako chini huwa key za windows zinaekwa kule unatafuta tu windows sawa iliokuja na laptop mfano home premium unaeka na key zako kazi imeisha huna haja ya kununua nyengine kwani ulivyonunua computer tayari umenunua na windows pamoja.

ubuntu ni kama mchele mmoja kwenye gunia la linux, kuna os nyingi za linux nzuri zinazozovutia ila tatizo la linux ni driver na software. mimi nimeshajaribu os tatu za linux ubuntu, zorin na pinguy.

hawa pinguy ni rahisi sana kutumia na vitu vingi vipo pre installed. pia muonekano wake ni kama windows na mac wazae mtoto hivyo hutapata shida kuitumia.ila setup yake ni kubwa inabidi uwe na gb za kutosha

zorin yenyewe ni nzuri kwa pc za zamani na ipo kama windows minimum requirement ya ram ni 128mb tu.
 
Last edited by a moderator:
Ubuntu ni kwa watu wanaotaka kuelewa how computer really works behind the scenes na mostly inatumiwa na madeveloper/Programmers kwasababu kwenye linux OS tunacheza na command lines tu na iko very secure. Windows ni kwa watu wakawaida tu wanaotaka kubrowse internet na wenye uelewa kidogo wa computer. Windows is very vulnerable na ndio maana cybery criminals, botnets wanatarget window uses mostly.

mh. Ngumu kumeza. MAPISHI MENGI....
 
Mkuu Uliyepost Una uhakika ulielewa Vizuri Microsoft waliposema wamesitisha suport for windows XP?
 
Ubuntu ni kwa watu wanaotaka kuelewa how computer really works behind the scenes na mostly inatumiwa na madeveloper/Programmers kwasababu kwenye linux OS tunacheza na command lines tu na iko very secure. Windows ni kwa watu wakawaida tu wanaotaka kubrowse internet na wenye uelewa kidogo wa computer. Windows is very vulnerable na ndio maana cybery criminals, botnets wanatarget window uses mostly.

You are very right buddy!!!
 
Wanasema ni virus free, au sio rahisi kwa mtu kutengeneza virus ikadumu katika jamii ya Linux.

Can you install two OS simultaneously? lets say Ubuntu na Windows?
Kama jibu ndiyo hapo juu vipi kuhusu utendaji wake computer pindi utakapo install OS mbili kwa pamoja?
 
Can you install two OS simultaneously? lets say Ubuntu na Windows?
Kama jibu ndiyo hapo juu vipi kuhusu utendaji wake computer pindi utakapo install OS mbili kwa pamoja?

Inawezekana na utendaji ni ule ule maana si kuwa unapowasha basi OS zote mbili zinawaka kwa pamoja. la hasha, unachofanya wakati ukiwasha ni kuchagua os ipi iwashe mashine.
 
Back
Top Bottom