Local disk (C) haionekani kwenye Laptop yangu naomba msaada

vlazarowosky

Senior Member
Nov 9, 2014
172
282
Habari za asubuhi wote.

Naombeni msaada kwa anayejua nawezaje kutatua hili tatizo, ANISAIDIE!

Laptop yangu haitaki kuwaka mpaka iweze kutumika. (Power inaingia vizuri, Tatizo ni booting) Ikifika mahali fulani kabla haijawaka, inaleta zile option za ku-restart normally au ku-restart kwa kutumia option ya recommended.

Nikichukua option ya ku-restart normally, inarudi hapo hapo, na nikichukua option ya ku-restart ambayo iko recommended, nafika mpaka pale kwenye system restore ila inashindwa kuendelea sababu inashindwa kuipata drive C ambayo ndo ina O.S.

Ni jinsi gani NAWEZA vipata vitu vilivyopo humu kwenye drive C?? Ni vya muhimu sana.

Nimeitoa hiyo hard disk na kujaribu kuitumia kama external hard disk ktk laptop nyingine, ila ni partitions zingine zinazoonekana na kufunguka. Drive C ktk my computer haionekani, ila kwenye computer management inaonekana.

Inaonyesha pia kuwa inaweza kuwa formatted. Inaonyesha rangi ya dark blue, kuwa ni primary partition na kuonyesha disk size tu (150 GB), zaidi ya hapo haionyeshi kitu kama drives zingine zinavyoonyesha drive letter, file format (NTFS) etc.

Nimejaribu ku-istall upya O.S kwa ajili ya ku-repair tu, sio new installation ila inashindwa kuiona drive C hivyo zoezi linagoma. O.S nitumiayo ni Windows 7 altimate, 32 bit.

Tatizo lilianza wakati naifanyia partition drive C, ghafla ilikuja ile blue screen na baada ya hapo ndo haya matatizo.

Pamoja na maelezo yote hapo juu, lengo langu kuu ni kutaka kupata vitu nilivyoweka humo ndani. Ni vya muhimu. Siwezi i-format. Kama kuna mdau anajua, tafadharini.

ASANTENI.
 
tumia mini tool partition wizard inayoweza kuboot, download toka site yao then fuata maelekezo iweke kwenye flash au burn kwenye cd halafu boot computer na hio software. adress yao hii hapa
Bootable Partition Manger | MiniTool Partition Wizard Bootable Edition

ukishaboot itafunguka kama software tu utaona drives zako na mafile kama utaka kuyahamisha au kuifufua utaangalia mwenyewe, ila always local disk c inatakiwa iwe active iwe na neno boot system kwa mbele, huwenda ulivyoifanyia partition umeiondoloea haki ya kuboot na kuipa partition nyengine isiokuwa na os

bootable-main-interface.jpg
 
Unaweza pia kutumia live cd ya ubuntu au linux yoyote ku acces the whole computer
 
Unaweza pia kutumia live cd ya ubuntu au linux yoyote ku acces the whole computer
Au kwa msaada zaidi jaribu kurepare boot kupitia comnd line kutoka katika instalation disk ya windo unayoitumia.

Maelekezo:
1. Boot katika instalition disk/usb uliyonayo
2. Dont instal window. Click repare
3. Nenda kwenye advance system repare.
4. Chagua repare through comand line
5. Then tupia code
Bootrec (press enter)
Bootrec/fix boot (press enter)
Bootrec/fix mbr (press enter)
Exit (press enter)

Baada ya hapo reboot normaly i hope itasolve hiyo issue brother
 
Asante sana. Nimefanikiwa kuifufua local disk (C), kwa kutumia hiyo software. Sasa hivi mambo shwaaaaariiii sana!!
Longo live JF.
 
Unaweza pia kutumia live cd ya ubuntu au linux yoyote ku acces the whole computer
Au kwa msaada zaidi jaribu kurepare boot kupitia comnd line kutoka katika instalation disk ya windo unayoitumia.

Maelekezo:
1. Boot katika instalition disk/usb uliyonayo
2. Dont instal window. Click repare
3. Nenda kwenye advance system repare.
4. Chagua repare through comand line
5. Then tupia code
Bootrec (press enter)
Bootrec/fix boot (press enter)
Bootrec/fix mbr (press enter)
Exit (press enter)

Baada ya hapo reboot normaly i hope itasolve hiyo issue brother

Asante sana kwa mchango na msaada wako, nimefanikiwa kwa kutumia hiyo njia ya mkwawa hapo juu.
 
Back
Top Bottom