Laptop ikiingia maji... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laptop ikiingia maji...

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by tindikalikali, Dec 22, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Wakuu habari zenu? Mimi ni mmoja wa waathirika wa hizi mvua, na imetokea P2 imelowa upande mmoja. Kuna wanaonambia eti imeshakufa. Jamani hli lina ukweli?
   
 2. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  inategemea. Inaweza ikafa au ikapona. Cha msingi ipeleke kwa wataalamu kabla ya kufanya chochote.
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,162
  Trophy Points: 280
  Usiiwashe kabisa, mpaka ifunguliwe ikaushwe maji yote, kuna uwezekano mkubwa kuwa itafanya kazi ikikaushwa kabisa maji kabla ya kuwashwa.

  Pole na maafa.
   
 4. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,582
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  pia toa battery
   
 5. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  We kweli we ni never give up hiyo battery imekuwa battery za radio kwamba zitavuja
   
 6. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Battery ni muhim kutolewa kwan ikiachwa itaendelea kufanya uhalibifu kwenye circuit.

  Mkuu fanya mpango wa kuisafisha kisha ikaushe.
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  we mtu wa ajabu
   
 8. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kweli yeye anajua Radio tu.

  It once happened to me and I was able to solve the problem by removing the battery as early as possible then dry by blowing the laptop using fan.

  LAPTOP/SIMU E.T.C IKIINGIA MAJI; TOA BETRI MARA MOJA NA JITAHIDI KUIKAUSHA KWA HEWA/BLOWER NA KAMA MAJI NI MENGI SANA LAZIMA IFUNGULIWE NA IKAUSHWE SAWASAWA THEN ITAKUWA OK.

  KAMA ULICHELEWA KUITOA BETRI NI BORA UKAIPELEKA KWA FUNDI KWANI KAWAIDA LAPTOP HUFANYA KAZI HATA KAMA IMEZIMWA SI SHORT CIRCUITING YAWEZA KUWA IMETOKEA.
   
 9. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Toe betri na angalia kama. Kuna kitu kingine chochote unaweza kufungua upande uliotoa betri na ukarudisha kama hilivyo bila kukorofisha kitu chochote.

  Baada hapo chukua blow dryer tumia kukaushia upande ule ulitoa betri kwa mda wa kutoasha inaweza kuwaka.

  Mie yangu iliingia maji na nikafanya hivyo ikawaka kama kawaida. Dogo aIimwagia maji ikiwa on na screen ilinipa warning na nikawahi kuzima.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Asanten wakuu
   
 12. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,582
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  fanya zoezi dogo tu, laptop ikiwa imezimwa chomeka charger/adaptor uone kama haitaendelea kucharge battery! Mfumo wa umeme upo active wakati wote kwenye machine hivyo hata maji yakiingia yanaweza kusababisha short ktk circuit
   
 13. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  toa battery na kama ikiwezekana fungua utoe battery memory kuepusha circuit short
   
 14. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  nimeshangaa kuhusu battery kwa sababu ushauri ninaouona ni wa ''kutoa battery' hivi hamna altenartive nyingine zaidi ya battery. Nitarudi baadae
   
 15. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  bora we yako imeingia maji nusu, Me yangu nimeikuta imekaa kama masaa mawili yaan kama nguo imerowekwa vile...nikainyanyua kisha nikawa naicheki inavyochuruzika mimaji (tena mimaji michafu)...
   
 16. P

  Paul S.S Verified User

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni kama huduma ya kwanza kufanyia kifaa chochote cha kielekriko kikiingia maji.
  Pili mbona amepewa ushauri mwingi wa nini afanye hadi video kawekewa lakini wewe unaona kutoa betrii tu.
  Au ulisha kariri ni redio tu inayotolewa betrii ikiingia maji?
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,162
  Trophy Points: 280
  Ushauri mwingine mzuri ambao umenijia baada ya kuitazama avatar yako ni, itafune uimeze yote laptop na battery yake.
   
Loading...