masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,410
- 14,119
ARV , bado hujajibu duku duku au swali langu.Mkuu gari ya model ya mwaka 1993 sio kwamba ilianza kutembea hapa bongo mwaka 1993. Huo ni mwaka wa kutengenezwa ukifuatilia unaweza kuta iliingia hapa bongo mwaka 2003 tena ikiwa na kilometa hata 20000 tuu.
Hata hizi Verrosa mnazozikimbilia sasa hapa bongo ni model ya 2002, lakini inafika hapa na Km.25000 tuu.
Hiyo gari iwe imetembea bongo au huko huko Japan bado kutembea Km 120,000 ina maana likiuwa limepaki miaka mingi tu na lilikuwa halitumiki.
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa magari, hata Japan gari lilotembea chini ya Km 100,000 ni ghali sana, tena sana hasa kwa 4WD.
Sasa kama lilifika hapa na km 20,000 mimi na-doubt(hebu google Goonet.com ujionee hata gari lako)
Niliachia njiani tu, kama gari lako linatembea km 20 kwa mwezi au wastani wa chini ya km 1 kwa siku basi gari lina matatizo.
Aidha ukubali tu fundi kasogeza nyuma odometer.
Last edited by a moderator: