Land Rover Discovery 4 off road capabilities.

Land Rover Discovery 4 off road capabilities.

mkuu, kwenye
1.handling
2.comfortability
3.braking
4.technology

landcruiser haiwezi kulingana na range rover hata kidogo,range rover iko far far ahead....ukija kwenye off-road ndio kidogo kutakuwa na debate.

kama mumeendesha european car yoyote ndio utajua tofauti ya handling na brake za euro makes vs japanese...

Mkuu kama umesoma vizuri nlisema the almighty Ranger rover is the best SUV so far ,ila kwa hayo matoleo mengine ya land rover kama 110,discovery Mimi na opt for a land cruiser
 
nimetaja jeshi la polisi kwasababu ni waharibifu,zile defender wanazo zaidi ya miaka kumi lakini bado zipo zinadunda ingekuwa gari nyingine za kijingajinga zisingekuwepo leo hii...walikuwa na hyundai kibao sasa hivi hazifiki hata kumi,walikuwa na benz g wagon,vw combi,golf zote wameua...sasa hivi wana toyota hilux[ndo ninazozisema hapa],zipe miaka mitano uone zitakuwa wapi..hizo hardtop zenyewe mpya lakini sasa hivi utafikiri zina miaka kumi kinachoziokoa ni spare zipo mpaka manzese.

angalia defender za jeshi zina hali gani halafu uliza ni za lini,au defender za ffu...btw nina mtu wangu wa karibu ana defender nzuri tu hio habari ya ac na vumbi naisikia kwako na hio gari inatumika kijijini tu ikija mjini inakaa siku mbili inarudi bush.

Sijasema kwamba defender ni gari mbaya Hapana, ila nimejaribu kuelezea sababu za Serikali kuachana nazo na kununua Toyota Land cruiser, na sababu hasa ni kwamba zinawasumbua na zina gharama kubwa ukilinganisha na toyota kumbuka Land Rover zilikuwa zinatumiwa kwa sababu ya mabakia ya Ukoloni wa Uingereza na ndiyo maana kila mahali kuanzia Kenya, Uganda zipo ila sasa hivi hata Kenya pia nilikuwa juzi huko wameacha kuzinunua tena na wanatumia Toyota Land Cruiser au Nissan Patrol na sababu kubwa ni kwamba Land Rover hawatoi tena ile version kama ya 109/110 ambayo ilitengenezwa maalumu kwa Afrika sasa hivi kuna hii new model nimeshaitumia sana Td 5 na iko juu ya mawe ingawaje ni mpya kabisa dereva wa Serikali walienda huko Mikoani wakaingia kwenye maji electronics zikafa na wanashindwa kuzirepair, kuhusu vumbi kuingia ni mwenyewe nilisafiri nayo Td5 na tulipata shida sana na ac kwa hasa kwa watu waliokaa nyuma na pia kuna openings nyingi zinazopitisha vumbi kuanzia kwenye milango hasa wa nyuma na chini!

Hivyo ukisikia watu wanasifu Land Rover ni zile za zamani 109, 119 mpaka defender za mwanzo kama miaka 10 iliyopita lkn hizi za toleo la mwisho kwa serikali yetu wamezishindwa na ndio maana idara nyingi wameacha kuzinunua!

Kuhusu ubora wa Toyota, jeshi la Polisi TZ hawajawahi kutumia Toyota land cruiser ndiyo mara ya kwanza ila nijuavyo JWTZ walikuwa na Nissan Patrol pick up ambazo mpaka leo baadhi bado zipo na zina miaka ishirini sasa tangu enzi ya Salim A.Salim lkn nijuavyo ndiyo gari inayotumiwa kwenye vita huko middle east kuanzia ISIS mpaka Libya kote hivyo kuna sababu hata UN hawanunui defender huku Afrika angalia gari zote zinazonunuliwa na UN ambazo zinatumika kwenye mazingira magumu ni Toyota Land Cruiser na labda cha kushangaza zaidi Waingereza wenyewe huwa wanatoa msaada wa magari ya kutumika hapa Tanzania kwenye miradi wanayoifadhili na hawatoi defender huwa wanatoa Toyota land cruiser hasa Hard Top!

Hivyo sijahoji ubora wa Land Rover kwa ujumla wake inawezekana ni moja kati ya gari bora Duniani kushinda Land Cruiser lkn kwa Tanzania zinawasumbua serikali kwenye gharama na ndio maana wameziacha sasa labda hatujui kuzitumia hilo sifahamu!
 
Kaka hiyo sio defender. . . .Tatizo nililonotice ni kuyumba nyuma kama haina mzigo ambapo kama itafungwa stabilizer bar inatulia (nilivyosikia). . Labda na za zamani zilikuwa too noisy (Puma wamekata kelele kabisa) kuliko Land Cruiser. . Otherwise defender 200tdi na sasa Puma . . . .Ni punda wa kazi big time mpeleke kokote hatokuangusha. .. .

Kwa sisi wenye kazi nyingi za offroad tutaangalia uwezekano.
Ila kwasasa nadhani discovery 4 itakata kiu yangu.
 
Back
Top Bottom