Lameck Airo anahujumu Halmashauri ya Rorya, achunguzwe

Lameck Airo anahujumu Halmashauri ya Rorya, achunguzwe

Nairobian

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
873
Reaction score
2,282
Mbunge wa Rorya, Lameck Airo akishirikiana na Namba tatu, Ochele, pamoja na Ongujo wamegeuza halmashauri ya Rorya kama shamba lao. Wanachukua tenda zote, kwa ajili ya makampuni yao. Lameck Airo amechukua tender ya kutengeneza barabara zote wilayani ambako magrader yake ndio inayofanya kazi za barabara bila kujificha. Aliyejaribu kuzungumzia hili swala alitishiwa maisha na Ongujo ambaye ni mshirika wa Lameck.

TAKUKURU na taasisi zingine ndani ya chama na serikali, hii ni ukiukwaji wa maadili ya utumishi. Iweje mbunge ajipe tender kwenye halmashauri?

Lameck na namba tatu wameiua CCM jimboni Rorya kutokana na tabia zao za kibabe. Katika vijiji karibia 52, CCM imeambulia vijiji viwili tu na CDM kuchukua nyingine. Matusi yao kwa wananchi imevuka mipaka. Kinana, chukueni hatua, vinginevyo hamna chenu Rorya. Chunguzeni hii ya Airo kujipa tender kwenye halmashauri.
 
Attachments

  • 20150511_140703.jpg
    20150511_140703.jpg
    619.8 KB · Views: 671
Sasa Kama wajaluo mmelala kwa nn asitake advantage? Na huyo no3 Ni mdudu gani
 
Nakumbuka sana mlivyokua mkimsema Professor Sarungi kwamba hana uchungu na Rorya eti kwakua mkewe ni mzungu.
Bila shaka mtamkumbuka soon......
 
Imekuaje tena mnatendwa hadi na mazuzu??
Mliambiwa chagueni kiongozi muelewa, msomi atakayewasilisha mambo yenu kwa utaratibu na msisitizo unaostahili....mkawa wabishi sana....
Eti mnamtaka mfanyabiashara asiyekuwa na elimu kubwa......ndo mtaweza kumdhibiti...
Umaskini wa akili ni kama laana vile...mtaangaika sana kumtafuta mchawi wenu kumbe ni vichwa vyenu wenyewe...!!

Sasa yawapasa mvune mlichokipanda....Mlipanda kwa shangwe na vigelegele yawapasa mvune kwa shangwe vile vile.....
Uchaguzi Mkuu ujao tena chagueni mazuzu wengine wawatende hadi mjue kunyoosha Kiswahili...

#SHAMEonRORYA
 
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]Almashauri = Ndio nini?[/FONT]
 
Hii hoja ni dhaifu, hiyo picha haitoshi kuthibitisha kuwa tenda amechukua yeye, inawezekana aliyechukua tenda amekodi mitambo yake na yeye ni mfanya biashara kwa nini asifanye hivyo, ulipaswa uweke nakala ya mkataba wa kampuni ya lakairo na halmashauri ndo utushawishi katika hilo, acha wivu
 
Na vipi kuhusu maadili ya uongozi kujipatia tenda kwa kutumia nafasi yake ilhali akihusika moja kwa moja kwenye bodi ya uzabuni. Je hili unaliona kama ni wivu?
 
Hii hoja ni dhaifu, hiyo picha haitoshi kuthibitisha kuwa tenda amechukua yeye, inawezekana aliyechukua tenda amekodi mitambo yake na yeye ni mfanya biashara kwa nini asifanye hivyo, ulipaswa uweke nakala ya mkataba wa kampuni ya lakairo na halmashauri ndo utushawishi katika hilo, acha wivu

Mkuu ile Halmashauri sidhani kama kuna uwezekano wa kupata hizo nakala.... I doubt kama kuna mikataba ya maandishi make 95% ya viongozi wa Halmashauri kusoma kwao mwiko!!

Naungana na wewe kuwa waache wivu..... Kwa kuwa walipokea pesa zake nyingi analazimika kuzirejesha chap chap!!
 
Mkuu ile Halmashauri sidhani kama kuna uwezekano wa kupata hizo nakala.... I doubt kama kuna mikataba ya maandishi make 95% ya viongozi wa Halmashauri kusoma kwao mwiko!!

Naungana na wewe kuwa waache wivu....Walipokuwa wanapokea pesa za

Fuguka mkuu,
Mbona umepatwa na kigugumizi!?
 
Si mlimpa kura za kishindo mkasema kwa vile Ni tajiri atawasaidia, kwa taarifa pesa ya tajiri haiendi Bure, sasa anajilia vyake shauri zenu nyie akina omera
 
Nairobian

Tumesema mara kibao kuwa airo aligombea ubunge kwa sb tu ya ufisadi na kulinda ufisadi na biashara zake basi,ukiangalia mambo yote yanayofanywa na serikali yeye anaandika jima lake la cairo,la kairo yaani kila kitu kinachofanywa na halmashauri ya rorya yeye anasema na kutangaza kuwa ni la cairo......tenda zote za halmashauri anatumia makampuni yake kibao kushinda tenda jizo kifisadi.....wito wangu kwa wana rorya yawa "Nyi kwar Nyanam Ng'ani ono,walwaare ombulu"
 
Last edited by a moderator:
Si mlimpa kura za kishindo mkasema kwa vile Ni tajiri atawasaidia, kwa taarifa pesa ya tajiri haiendi Bure, sasa anajilia vyake shauri zenu nyie akina omera

Inasikitisha kweli. Huyu namba 3, mwenyekiti ccm wilaya anatishia watu hovyo
 
Jambo la msingi pigs chino chama chake this time.na ukabila muache mbwa nyie
 
Jambo la msingi pigs chino chama chake this time.na ukabila muache mbwa nyie

Ukabila unaingiaje hapo sasa?Halafu kuwa na adabu japo kidogo, unawezaje kutukana watu wote wa Rorya na kuwaita mbwa?Anyway, busara yako imejidhihirisha wazi katika hilo
 
Kwanza historia ya lameck airo kabla haja wa mbunge mlikumbuka ni vitu gani alikuwa anafanya! Na aliupata ubunge lazima aendeleze rafu.
Ovaaa
 
Pesa ndio mambo yote, wenye elimu Tanzania hawana Chao. Hapa ni pesa na kujuana tu. Tunao maprofesa wengi lakini ni watumwa wa wanasiasa!
Halmashauri ya Rorya Airo kaikamata kwa sababu ya pesa zake. Airo ni darasa la saba kielimu lakini ni kama profesa kifedha. Ananyenyekewa na watendaji wa Halmashauri kwa kuwa wanaamini watanufaika.
Nchi hii kinachotafutwa ni pesa elimu ina maana ulaya/America!
 
Back
Top Bottom