Hivi kwanini gari za polisi zinaendelea kuitwa 'difenda' huku nyingi siku hizi zikiwa Landcruiser ?

Hivi kwanini vituo vya mafuta vinaitwa ''sheli' huku tukifahamu kampuni ya Shell haipo nchi ?

Hivi kwanini simu za mkononi vijijini wanaziita 'nokia' hata kama ni kampuni ingine ?

Hivi kwanini watu husema barabara ya Morogoro road hata kama barabara maana yake ni 'road' ?

Hivi kwanini ukitaka kushuka kwenye daladala ambapo hamna kituo useme 'msaada' mbona kupanda wanasimama popote ?

ongezeni zingine.