Lakini hata huyu atanitenda tu.

Lakini hata huyu atanitenda tu.

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
Bila shaka umewahi kukutana na mtu aliyetendwa katika mapenzi.Au ni rafiki yako au ni wewe.Unajitoa kwa moyo wote kumpenda mtu ila yeye hakujali,anafanya yale ambayo mwenyewe angefanyiwa asingevumilia ulivyovumilia.Mungu si athumani umepata mwingine ambaye anakupenda ila kutokana maumivu uliyopata nyuma unamkwepa ili usijiumize au usimuumize.Pengine unafikiria "Lakini huyu nae atanitenda tu" kama una tatizo hilo naomba tutafakari pamoja.
::
KUBALI UKWELI.
Kubali kuwa yule aliyekutenda si huyu aliyepo mbele yako.Usimlaumu aliyekuacha maana aliamua kufanya kwa matashi yake.Ukweli ni kuwa hujui ungetenda namna gani kama ungekuwa yeye.Mpe nafasi aliyepo mbele yako yaweza kuwa nuru mpya maishani mwako!
::
UTENDEE HAKI MOYO.
Uwe tayari kuzungumza na moyo wako.Mweleze wazi aliyepo mbele yako unavyojisikia,mipango yako,sema bila kuficha.Usiogope kumuumiza kumbuka ni vema ajue mapema kuliko kujua kupitia wengine ambao wanaweza kumpa taarifa zisizo sahihi.Usijaribu kuficha makosa yako wala kuyakuza ili uvute huruma yake.Hapo utautendea haki moyo wako.
::
SAMEHE
Jambo lisilopendeza ni ile tabia ya kusema umemsamehe aliyekutenda lakini hutakomea hapo.Uko tayari kulipiza ulivyotendwa.Huko ni kutaka kuonekana mwema lakini pia unataka kuonja utamu wa kulipiza kisasi kwa kumwona mwingine akiteseka.Hilo ni kuamsha majeraha ya zamani.Fungua maisha mapya kwa kuondoa mashaka kuwa huyu nae ni kama wa zamani.
::
JIFUNZE KATIKA UZOEFU
Kadri tunavyojaliwa uhai ndivyo tunavyopata uzoefu mwingi.Huu ni utajiri wa maisha,tunahuzunika,tunajuta,tunashindana,tunatafuta matatizo.Hilo ndilo tatizo uzoefu wetu mwingi unatuachia maumivu kwa sababu wale tuliowapenda sana ndio waliotumiiza sana.Naam tusijitupe mikononi mwa wengine jumla bila hadhari,,
::
USISAHAU A,B,C
Kwa kuwa umepata akupendae basi nakuhimiza usisahau
A=Amua kumkubali.
B=Bila kukumbuka ya zamani.
C=Chukulianeni na kutimiziana mahitaji yenu.
::
Ondoa wazo la hata huyu atanitenda tu! Yafurahie maisha mapya
=
 
Jaundiced views are shaped by real life events and it's hard to ignore them.
 
Hapo kwenye uzoefu, lmao! Its nice when you look at a person and predict his/her next move. This is living and other stories.
 
Back
Top Bottom