Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Nimechoshwa na tabia ya kuwadhalilisha viongozi wetu hadharani tena kwa lugha za kebehi, eti kisa wamekosea kingereza! Hili ni jambo la ajabu kweli kweli. Nifahamuvyo mimi lugha yoyote ile duniani inao usahihi na upotovu wake kwa wale watumiaji wa hiyo.
Hata hiki kiswahili tunachozungumza kila siku tunakikosea mno!
Cha kushangaza hapa ni pale sisi tunapoona sawa kukosea kiswahili huku tukiwatupia lawama wale wanaoonekana kukosea kingereza!
Mpaka hapo mimi nimeshindwa kuelewa kabisa aina hii ya akili.
Huu ni utumwa wa fikra uliovuka mipaka yake ya kawaida!
Ndugu zangu waingereza walithamini kwanza lugha yao ndiyo maana wewe unaithamini hiyo lugha yao leo!
Pamoja na ukweli huo mchungu hata hivyo kulingana na wakati tulio nao mimi si miongoni mwa wale wanaotaka kiswahili kiwe lugha ya kufundishia katika taasisi yoyote ya elimu iliyopo hapa nchini.
Kwa nini?
Ni vizuri tukaacha kabisa kuishi kwa kudanganya na kudanganyana sasa.
Tukiendelea kukifanya kingereza kuwa bidhaa adimu ambayo haipatikani mitaani kwetu, ndani ya daladala, vijiweni nk. Nawahakikishia leo hii huu ujinga wa kucheka na kuchekana kwasababu ya lugha hautaisha kamwe hapa nchini.
Bali kinyume chake utasambaa kutoka katika mitandao ya kijamii na kuingia bungeni, mahakamani, serikalini na kila sehemu ndani ya mipaka ya nchi hii.
Unajua tatizo ni nini?
Bidhaa imekuwa adimu!
Tukiachana na hilo; nani asiyejua umuhimu wa kingereza katika dunia hii ya utandawazi? Dunia ya leo ni kijiji kidogo tu! Yale maisha ya kuishi ukiwa umejifungia na lugha yako, biashara yako, kazi yako na chochote ulichonacho; yako wapi? Leo hii maisha ni popote, biashara ni popote na ujasiriamari ni popote. Usipojua kingereza utakuwa mgeni wa nani?
Hata Sanaa ambayo hapo kale kidogo haikubagua wasanii katika lugha wanazotumia lakini leo hii inawalipa zaidi wale wanaojua kingereza kuliko wale waliong'ang'ania lugha zao za asili. Watanzania tusikichukulie kingereza kama dalili ya usomi la ila kama nyenzo ya mafanikio katika nyanja yoyote ya kiuchumi bila kujali kama unaongea rafudhi ya kimarekani au kikaribiani.
Mradi umelitimiza kusudi lako tu!
Sasa basi ili kuwafanya raia wa watanzania kuwa sawa na wale wa wazambia, wamalawi, waganda wakenya katika ufahamu wa kingereza, je tunapaswa kufanyaje katika kulifanikisha hili? Kwa upande wangu mimi naomba tuanze kutumia kingereza kama lugha rasmi ya kufundishia kuanzia Shule ya msingi. Ndiyooo! maana watu wengi huishia kuipata elimu hiyo tu!
Lakini pia unaonaje endapo huyu wa sekondari kama angekuwa amesoma masomo hayo kwa kingereza toka Shule ya msingi ingekuwaje kuhusu ufanisi wake? Chonde jamani tusiwalaumu wasomi wetu! Kingereza ni lugha kama kihaya, kichaga au kimakonde. Hata katika lugha zetu hizi mama mtu usipopata watu wa kuongea nao mda mrefu ni lazima urimi wako uwe mzito.
Hii ni kanuni ya asili kwa lugha yoyote!
Ndiyo maana napendekeza kwenu nchi yetu ihakikishe wanafunzi wanaanza na hii lugha tangu shule ya msingi tukifanya hivyo tutakuwa tumetengeneza kundi kubwa la waongea kingereza jambo litakalofanya kigugumizi cha wengi kuondoka. Na hivyo kuondoa uadimu wa hii bidhaa unaofanya wale walionayo kulinga na kujiona ni wasomi.
Uwe ni msomi au la tujifunze kingereza na si kuchekana !!
Kiswahili kibaki kama somo tu na hii haina madhara yoyote.