Kivipi mazingira yanaharibika?? Yaan majeneza yanaharibu mazingira?? Wakati hapo Una shelves za mbao sofa seti za mbao...
Kukata mti utengeneze jeneza tu ushaharibu mazingira.
Hata land use tu ni uharibifu wa mazingira. Ukishazikwa wewe ndiyo umeziba eneo hilo lisitumike tena.
Tumetaka kuunganisha barabara ya Maliki Upanga chini na juu, imekuwa kazi sana kwa sababu hapo katikati kulikuwa na makaburi ya Tambaza.
Ikabidi watu wafukue makaburi na kuyahamisha kwa tabu sana. Ndipo kile kipande cha kutoka United Nations Road, hapa Muhimbili Primary School, kuja hapa juu Mindu Stree kikawekwa.
Ingekuwa hatujajifunga kwenye kuzika, tusingekuwa na matatizo kama hayo.
Kuna siku nilikuwa napiga mahesabu, kama watu wakiwa wanakufa kwa rate hii ya leo na wanazikwa tu, in 100 years tutatumia eneo kama la nchi nzima ya Gambia kwa makaburi tu.
Sasa watu wenye kufikiri mbele sana wanafikiria, what about in a thousand years? What will the economic cost be?
Even worse, zamani watu walikuwa wanazika ina biodegradable way, hawajengei. Siku hizi watu wanajengea mausoleum, wanaweka concrete kabisa. Nilikuwa natania nikasema jinsi watu wanavyosilibiwa simenti, ikiwa siku ya parapanda watu watafufuka kutoka makaburini, wengine watashindwa kufufuka kwa sababu ya makaburi yalivyosilibiwa simenti.
Najua mengine ni mambo ya utamaduni na kila mtu ana haki ya kuzika kivyake, lakini, kadiri tunavyoongezeka na ku face matatizo ya mazingira, land use etc, inaonekana ni vizuri zaidi kutafuta alternative.