Ladies, why?...!

Nahisi dada King'asti hujamuelewa kijana anachomaanisha. Naona umeitukia hii topic kwa jazba na kiushabiki zaidi kiasi kwamba nashindwa kuelewa kama ni wewe huyo wa siku zote mwenye ushauri wa maana au la!

Na nduguyo Asprin naye ameamua kuchangia kwa kutaka kukufurahisha zaidi kuliko kusema ukweli kabisa. Mimi kwa muono wangu hata ukirejea kwenye vitabu vitakatifu imempambanua mwanamke bora ni yupi. Ni yule mwenye kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nyumba yake. Soma mithali.

Inapendeza sana wanandoa mkishirikiana kujenga na kuinua uchumi wa nyumba yenu kwa uhuru, uwazi na kushirikiana kwa kupanga kila jambo pamoja. Mkitanguliza upendo wa kweli Kati yenu, kamwe hayo matatizo hayatotokea. Mimi ninamashaka sana na ndoa yako kama inaamani kwa huo msomamo na mtazamo wako

Umeona eeh babu? Muambieni kijana mwanaume hajitambulishi! Kama mkeo anaendesha gari ya 50M usizojua amezitoa wapi na mafuta anatoa wapi, jua imekula kwako! Hujamnunulia hiyo iPhone na hujui anatoa vocha wapi unaweza kupoteza haki ya kuuliza mawasiliano na mahusiano yake!

Tatizo hawa vijana siku hizi wanalalamika manake wanapenda u-slope utasema wanafanya hesabu za ku-integrate! Marioos! Uvunje ndoa kwa sababu mke anadai ununue chumvi?!
 
Umeona eeh! Yaani hata nashindwa kuelewa Eiyer anataka nini, maana nishamwambia l am ready to be full time housewife mradi anitimizie mahitaji yangu yote na ya familia yangu. Sasa nikimpunguzia responsibility kwa kutake care of my extended family bado alalama! Khah!

Ukinisoma vyema hautapata shida kunielewa ma love!
 
gfsonwin,nimechagua kutokujibu swali lako lakini ukichunguza vizuri utapata jibu!
 
I respect you Cacico, I wish King'asti angesoma huu Uzi wako mkuu .

mariages, mariages, mariages! ukiamua kuifanya iwe hell itakuwa kweli, na ukiamua kuifanya heaven itakuwa! the two of u are the once playing that game! but this game called mariage will never give us a winner in terms of dictatorship, there IS ONLY ONE WINNER BECAUSE OF RESPECT AND THATS A HUSBAND!(hapo tupende, tusipende ndivyo MUNGU alivyoumba, daima mwanamke atakuwa chini ya mumewe.) Samahanini kama nitawakwaza fellow women coz kila ndoa na misingi,makubaliano na VISIONS zake! kamwe yangu haitakuwa yako, wala yako haitakuwa yangu! naishi kama mimi na simfuatilishi mtu NEVER!

coming to the point ya kipato cha mwanamke! we are doing alot under carpet ambazo wanaume hawafahamu, eg costs ndogondogo kama sabuni, toothbrush, vyombo,vyakula, vitu vya jikoni kwa ujumla SIJUI KAMA MY HUBBY ANAJUA VINATOKA WAPI, HUWA ANAONA SIKU ZINAKWENDA, am doing everything kuhusu nyumbani, nguo zangu na watoto na zake ni mimi. na yeye ana majukumu makubwa kunizidi eg skulfees, kujenga, service magari na fuel, etc wababa mnaelewa!

THEN WE HAVE A JOINT ACCOUNT! hiyo account iko kwa ajili ya ndugu zake na ndugu zangu! eg msiba umetokea kwetu tunachota laki 5 za mchango nk, msiba umetokea kwao we do the same, mama mkwe nakuja tunachota hapo, mama mkwe naumwa tunachota hapo and vice versa! hii account we share kudeposit kila mwezi and we dont touch it kabisa! so hakuna anayeona anaonewa kwa misingi tuliyokubaliana!
 
I respect you brother. You are very wise man.

Eiyer,
Hapa nasema kutoka chini ya sakafu ya moyo wangu. The same snario, yamenitokea, na hapa nitampa mwenza wangu naye asome thread hii ingawa italeta maneno tena. Mimi ni mfanyakaz wa Serikali, nina cheo kikubwa tu na pato langu si hapa kulinganisha na maisha ya mtanzania wa kawaida. Mwenzangu ni mjasiria mali, mtaji na plan ya biashara yake ni nguvu zangu, yeye katika mtaji hakutoa hata senti moja. Namshukuru, ni mzuri katika kusimamia biashara na anaingiza kipato kikubwa kwa mwezi. TATIZO LILIPO; hela yake ni sawa na ukoma, hakuna anayejua inakwenda wapi, hanunui chochote kile pale nyumbani kuanzia chakula, kulipa bili ya umeme, DSTV, maji,ada za watoto,gharama za matengenezo madogo kwa mafundi na mbaya zaidi miradi yangu hayuko tayari kuisimamia hata kama ana nafasi yuko radhi kuona nawatuma mafundi kununua vifaa vya ujenzi bila kuwasimami na mafundi kama unavyojua ni wachakachuaji wakubwa. Kwa mambo mengine ni mzuri, anajua wajibu wake kama mama, anajua wageni na n.k. Sikuona kugombana naye ni njia sahihi, ila nilimwambia ukweli kwamba kila mwisho wa mwezi alete pato lake na la kwangu tuchanganye then tupange matumizi, hiyo haikuwa rahisi mpaka wazee wa dini waliingilia. kwa sasa tunakwenda vizuri. Wana Jf, msishangae mbona haya ni ya kila siku kwenye maisha ya ndoa?? ila suala la divorce liwe ni hatua ya mwisho baada ya mengine kushindikana.
 
ikoje si kama yako!kumbe imekukera hee!! na wewe kumbe unatolea povu mshahara wa mkeo !shauri zako utalishwa hata wa wenzio

Malaya tu wasioridhika na wale wenye tamaa iliyopitiliza ndiyo wanaweza kuwa na msimamo na mtazamo kama wako. Kama umeolewa nampa pole sana huyo mumeo.
 
Back
Top Bottom