Ladies, why?...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ladies, why?...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Jun 27, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Ni jana ndoa ya bro wangu ilikufa kabisa.

  Chanzo cha kifo cha ndoa hiyo ni baada ya bro kumfungulia mkewe biashara na kumkabidhi ili ajipatie mahitaji yake sio mpaka mumewe ampe.

  Lakini cha ajabu mkewe ameendelea kutoa shida zake kwa bro, bro akimuuliza mwanamke anajibu hela za dukani ni zake mke na yeye kama mume anatakiwa amhudumie tu!

  Swala hili lilizusha ugomvi ulopelekea ndoa kuvunjika au kufa . . .

  Kesi za namna hii ni nyingi sana,mwanamke anahitaji haki sawa, sijui hizo haki sawa anazitafsiri namna gani. Unakuta mwanamke ni mwajiriwa au ni mjasiriamali, mshahara au hela ya biashara haionekani nyumbani, akitakiwa wagawane matumizi ya nyumbani anang'aka, anasema hayo ni majukumu ya mume! Kwanini?

  Wengine inafikia mpaka gharama za vocha, saloon, nguo wanadai kwa mume wakati wana kipato, ukiwauliza wanasema mi mke wa mtu bana, biashara au kazi yangu ni yangu haihusiani na ndoa/mahusiano yangu!Sasa najiuliza hicho kipato ni cha nini?. . . . . .

  Wanawake wengine wanasaka vidume wenye hela wakati wao wanajimudu sijui ili iweje!

  Kuna mzee mmoja, mkewe ni mwajiriwa serikalini na yule mzee ni mfanyabiashara, imebidi kutumia ubabe, mkewe akipata mshahara lazima aulete nyumbani na utanunulia mahitaji ya nyumbani mpaka uishe wote siku hiyo! Namkubali sana huyu mzee.

  Wakati mwingine ni bora wanawake wasiwe na kazi au kipato kwa usalama wa familia. Labda mnaweza kuniambia hizo hela mnatafuta za nini?
   
 2. m

  mamajack JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  huyo hakua mke, alikuwa mjasiriamali!

  ni tabia tu za watu wajinga ambao wana mifumo ya kiswahili.

  mpe pole mwaya kaka yako.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Kama sio mke basi asilimia kubwa ya wanawake siku hizi hawafai!
   
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Eiyer,changu changu chako chetu ndo wimbo wa taifa katika ndoa zetu nyingi.
  Mwambie kaka yako arudishe moyo,hayuko peke yake katika hili. Mwanamke ukichunguza matumizi yake utakuta anatumia pesa nyingi ( bila mme kujua) katika kuwatunza wazazi na nduguze,hiyo ndo hali halisi.
  Btw kinababa kwa nini tulalamikie hili wakati sisi ndo kichwa cha nyumba?
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Hayo sio matumizi sahihi,anatakiwa anaweka mshahara wake mezani na mimi naweka wangu mezani,tunagawa matumizi bana.Kama sisi ni kichwa wakae nyumbani!
   
 6. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Ndo maana watu tunaobisha hodi kuingia huko ndoani mioyo yetu iko na mashaka sana!
   
 7. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  nina hakika hiyo sio sababu ya ndoa kuvunjika,ya ndani ya kuta za nyumba wakiwa wenyewe kaka yako hatakuambia!
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Bishanga, come to think of it, hivi ni wanaume wangapi wanawatumiaga wakwe zao hela? Tena mwanamke anatumiwa kipato chake na mwanaume na nduguze kuliko ndugu zake wa damu!

  Haya umemalizia vyema. Kichwa cha nyumba afu unataka ugawane majukumu pasupasu na mkeo? Nae akirudi saa saba usiku usiulize!
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Usiogope,ingia ukapambane na independenti ladiz!
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ni vizuri kupanga maisha pamoja.. pia kushirikiana kwa kila kitu...tatizo wababa wengine ni wabinafsi ..utasikia mwanamke anasema mume wangu anajenga nyumba ingine mbezi huko ....as if haimuhusu.....but kabla ya kujenga huyu baba angemwambia tu mkewe tujenge nyumba mbezi tunaitaji amount fulani nina hii ebu jazia hii tuweke msingi dear....!!
  sasaunakuta wanaume wengi wanajifanyisha vidume ndani wanadai hawataki kupelekeshwa au kuhudumiwa na mwanamke..anajitwika majukumu yooote mwisho wa siku unakuta hela ya mwanamke ipo idle ....sasa hapo ndo hata mwanamke anakuwa jeuri na kuhonga viserengeti boys.....
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Inaonekana wewe unajua yaliyomo kuliko wenye ndoa,hebu niambie hayo mengineyo!
   
 12. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  usinielewe vibaya,ni kwamba wanaume na wanawake,ndoa zinapovunjika,ni vigumu wewe wa nje kujua nini kinachovunja ndoa!haya tunayoambiwa nje huwa ni kuweka mambo sawa tu kwa ndugu!
   
 13. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160

  Hawa independent ladies wana challenge!! Usiombe ukutane na mbeijing amambaye kalishwa sumu za Independence halafu zikamkubali...
  Ni kweli inafikia sehemu mwanaume anaona bora aoe aliyeishia darasa la saba halafu toka amalize shule akawa anajiandaa kuwa mke/mama wa nyumbani!
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Dada king'ast gud mrng,hivi kumbe unapooa unakua umeoa ukoo mzima na wanakua ni wake zako inkludingi wakweeeeh,so there your rensponsibillitieee!I didnti no thisi!!Kichwa cha nyumba when it comes your income!Ladies bana!
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  How do you knw kwamba hili sio lililovunja ndoa hii?
   
 16. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Eiyer nakuhakikishia ukiendelea na hizi mada za kwuadadavua kina mama/dada utaishia kumpoteza Kaunga

  kwani whats happening?:A S confused:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Uchafu hausafishwi na uchafu!
   
 18. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  nimekosea kutumia neno nina hakika ningetumia nadhani,naomba usiandike katika hansard!
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hahaha, baby braza! Kumbe mke anapohudumia mamako na babako, dada zako na wapwa zako wanapokuja inakuwa aliolewa na ukoo eeh? Nkuki kwa nguruwe! Wewe hudumia nduguzo woote na mkeo, yeye atahandle nduguze. Maisha yanakuwa pamba motooo, fyagiliaa waaah waah!

  Ila ukitaka mkeo akuheshimu mdogo wangu, fanya majukumu yako. La sivyo atakuona marioo! Na tatizoi lenu mkisaidiwa majukumu mnajisahau na kupata excess ya za kuhonga! Jipangie baba, uhonge ngapi, unywe ngapi, ugawe kwa mashosti ngapi! Hapa labda ujisemeleshe 'tunahitaji tiles za 4M mamaa' ndo ntakunjua account yangu!
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,977
  Likes Received: 23,679
  Trophy Points: 280
  Dogo nimekukubali,

  Kila siku lazima ushuke na uzi wenye kisa kipya.

  Hongera kwa ubunifu and keep it up!!
   
Loading...