Labour kuzowa viti 410, Conservative yaambulia 131 tu

Labour kuzowa viti 410, Conservative yaambulia 131 tu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Utabiri baada ya kura kupigwa nchini Uingereza unaonesha kuwa chama cha Labour kimeibuka na ushindi wa kishindo, huku kiongozi wake, Keir Starmer akielekea kuchukuwa nafasi ya Rishi Sunak kama waziri mkuu mpya.

Matokeo yaliyopitiwa na mashirika mbalimbali ya habari yanaashiria kuwa chama cha Labour kinachofuata siasa za mrengo wa kati kushoto kimepata viti 410 kati ya 650 bungeni, huku wahafidhina wa mrengo wa kulia, Conservative, wakimudu kukusanya viti 131 tu, kiwango cha chini kabisa kwa chama hicho kwa zaidi ya miaka 100 sasa.

"Kwa kila aliyeipigia kampeni Labour kwenye uchaguzi huu, kwa kila aliyetupigia kura na kukiamini chama chetu cha Labour kilichobadilika, ahsanteni." Aliandika Starmer kwenye mitandao ya kijamii.

Naibu wake, Angela Rayner, aliliambia shirika la utangazaji la BBC kwamba wametiwa moyo sana na matokeo, lakini asingeweza kusema zaidi mpaka pale matokeo yote yawe yamekusanywa na kutangazwa rasmi.

Katika kile kinachoonekana kama inuko jengine la wafuasi wa siasa za mrengo wa kati, chama cha Liberal Democrat kinatazamiwa kupata viti 61, na kukiondosha chama cha Wazalendo wa Scotland, SNP, kwenye nafasi ya tatu bungeni. SNP kinaelekea kupata viti 10 tu.

Nigel Farage akusanya viti 10
Kwa upande mwengine, chama kinachopinga wahamiaji cha Reform UK kinachoongozwa na mwanasiasa mwenye utata, Nigel Farage, kimepata viti 13, huku chama cha wazalendo wa Wales kikiwa na viti vinne na walinzi wa mazingira, the Greens, wakiwa na viti viwili.

Kwa ushindi huu, Labour iko mbele kwa viti 170, ikiwa ni mara ya mbili ya ushindi wa Conservative kwenye uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2019 uliokuwa umetawalliwa na ajenda ya Uingereza kujitowa kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit.

Kiongozi wa zamani wa Conservative, William Hague, ameiambia Times Radio kwamba matokeo yanayoendelea kukusanywa yatakuwa janga la kihistoria kwa chama chake, ambacho kwa matokeo yake ya mwisho mabaya yalikuwa viti 156 mwaka 1906.

Lakini profesa wa siasa kwenye Chuo Kikuu cha London, Tim Bale, anasema matokeo haya si mabaya kama vile ambavyo ilitazamiwa yawe, na kwamba sasa chama hicho kilichotandwa na vita ndani vya kiitikadi, kinapaswa kuchaguwa muelekeo kinaotaka kuuchukuwa.

Kura kutoka vituo 40,000 kote nchini Uingereza zilianza kuhisabiwa mara tu baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa na kuendelea hadi usiku wa manane, huku matokeo rasmi yakitazamiwa asubuhi ya Ijumaa (Julai 5).
 
Unamaanisha kwamba sasa Uingereza itaiunga mkono Russia au unaropoka tu.
Namaanisha Zelensky anarudi kwenye kazi yake aipendayo ya usanii wa kuigiza.

Hujui kusoma, unakurupuka tu kama swala mbugani.
 
Namaanisha Zelensky anarudi kwenye kazi yake aipendayo ya usanii wa kuigiza.

Hujui kusoma, unakurupuka tu kama swala mbugani.
Haujajibu swali, unamaanisha kwamba sasa Uingereza itaiunga mkono Russia au unaropoka tu.
 
Haujajibu swali, unamaanisha kwamba sasa Uingereza itaiunga mkono Russia au unaropoka tu.
Siasa ya nje inabaki vile vile. Ni afadhali Sunik kuliko huyo jamaa kuhusu Mambo ya Russia na Israel
Russia haina haja ya kuungwa mkono, kwa sababu haijawahi kuacha kukubalika.

Viongozi wapya wa Ulaya wamegundua kwamba kuendelea kumchokonoa dubu ni sawa na kujitegea tanzi wenyewe.

Hivi sasa mataifa yote ya Ulaya na viongozi wao ndipo wametahamaki na kuanza kumwelewa Victor Orban, ndiyo maana kawekwa kuwa msuluhishi.

Ingekuwa wakati ule SMO ikianza, wangeshamla kichwa, angewekewa vikwazo na wala asingeruhusiwa kumtembelea Putin.

Sijui unaelewa hata? Najua mambo haya ni magumu sana kwako kwa sasa. Ila jikaze tu; hakuna namna.
 
Wapinzani wameshinda Uingereza sasa ni zamu yetu Tanzania.🤞✌️
 
Siasa ya nje inabaki vile vile. Ni afadhali Sunik kuliko huyo jamaa kuhusu Mambo ya Russia na Israel
akishaingia Trump tu ishu ya urusi ukraine itakua haina nguvu,, watapeleka nguvu Israel,,,,na huyo uingereza hawezi kuendelea Ukraine kama baba yake akibadili maamuzi
 
Wapinzani wameshinda Uingereza sasa ni zamu yetu Tanzania.🤞✌️
Ni vizuri kuota ndoto. Lakini zikipitiliza ni hatari kiafya.

CDM hakuna viongozi, japo kuna wafuasi. CDM ina wababaishaji wa siasa wakati Sisiemu yenyewe ina walafi na viongozi wenye maono kiduchu.

Sisiemu itaendelea kubaki hatamuni kwa muda mrefu sana.

Siku CDM ikijifunza kutenganisha maslahi binafsi na mustakabali mpana wa taifa, hakika chama kitakuwa kimepiga hatua kubwa sana ya mabadiliko.
 
Back
Top Bottom