Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,793
- 165,531
Huyu mwili wake ulisambaratishwa kikatili na bomu la machozi na si kitu chenye nkali.Huyu Marehemu aliuawa kikatili,hakuna hata kiongozi wa serikali aliyeonysha kujali wala kutoa hata kauli ya faraja japo kwa wafiwa."Alichomwa na kitu chenye ncha kali".Kuonyesha walidhamiria mkuu wa usalama wa Raia wa mkoa ule akapandishwa cheo!!
Wanatakiwa waibike mchana kweupeeee na familia zao wahusika wote.
Miongoni mwa watu waliouwawa kikatili ni mwandishi Daudi Mwangosi.Naamini kilio chake hakikuwa kama kilio cha samaki na sasa Mungu amejibu.
Kuna watu walipopata madaraka walijisahau na kudhani hii nchi ni mali yao na kwamba watatawala watakavyo huku wakisahau kuna siku watatoka madarakani na kubaki raia wa kawaida tu.
Aibu waipatayo leo hii ni matokeo ya waliyoyatenda walipokuwa madarakani.
mkuu mwacheni Marehemu Mwangosi apumzike kwa amani huko aliko. Tuendeleze siasa bila kuleta majonzi kwa familia za marehemu.
mkuu mwacheni Marehemu Mwangosi apumzike kwa amani huko aliko. Tuendeleze siasa bila kuleta majonzi kwa familia za marehemu.
RIP Mgimwa, RIP Mvungi, RIP Chachage, RIP Kolimba, RIP Sokoine, RIP JKN, RIP Mwangosi, RIP KARUME, RIP Kombe, RIP Ballow .... CCM must go ...
Wakina nani?Damu ya Chacha wangwe itawatafuna hata kizazi cha 7...
Halafu yule askari aliyemfanya hivyo hajulikani alipo!! Alipelekwa mahakamani kama Mara 2 baadae kesi ikafa mpaka Leo!! Hii ndiyo Tanzania, CCM inatuadaa wakati wa kampeni tunawapa kura ila wakishapa huongozi wanakuwa madicteta!!