Sweden yalaani mauaji ya Mwangosi;Yasema kumuua mwandishi ni kujichafua:CHADEMA wahoji kamera ya Mwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sweden yalaani mauaji ya Mwangosi;Yasema kumuua mwandishi ni kujichafua:CHADEMA wahoji kamera ya Mwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  IJUMAA, SEPTEMBA 07, 2012 05:34 NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


  *Yasema kumuua mwandishi ni kujichafua
  *Polisi wazidi kushutumiwa kila kona
  *Jukwaa la Katiba, UTPC wazidi kucharuka
  *Vyama vya siasa vyapanga kumwona Pinda

  BALOZI wa Sweden nchini Tanzania, Lennarth Hjelaker, ameungana na mamilioni ya Watanzania, kulaani tukio la kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

  Amesema kuwa, kitendo cha mwandishi huo kuuawa akiwa kazini, kimeleta taswira mbaya kwa uhuru wa habari nchini.Hjelaker aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

  Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana, umewakutanisha viongozi wa vyama vyote vya waandishi wa habari nchini na unatarajia kuhitimishwa leo.

  “Natoa salamu zangu za rambirambi kwa waandishi wote wa habari, ndugu na familia ya Marehemu Daudi Mwangosi na pia naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu,” alisema balozi huyo kwa kifupi.

  Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walitoa tamko linaloonyesha msimamo wao juu ya kifo cha Mwangosi.

  Wakati akilaani mauaji hayo, Balozi Hjelaker ambaye hakuzungumza sana, alisema kwamba, Serikali ya Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo.

  Umoja wa waandishi walonga

  Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), umeitaka serikali kuwasimamisha kazi askari wote walioshiriki operesheni haramu iliyosababisha kifo cha Daudi Mwangosi.

  Rais wa UTPC, Kenneth Simbaya, alitoa tamko hilo Dar es Salaam jana mbele ya viongozi wa klabu zote za waandishi wa habari nchini.

  “Tunataka askari hawa wasimamishwe kazi kupisha kipindi hiki cha uchunguzi, lakini pia tunataka uchunguzi ukikamilika, Serikali iutangazie umma na kupisha sheria ichukue mkondo wake kwa wale waliohusika na kifo cha mwandishi mwenzetu,” alisema Simbaya.

  Alisema wakati huu wa uchunguzi, Serikali inatakiwa kumpa chochote ilichonacho mjane na watoto wa marehemu, ili waweze kujikimu.

  “Katika mkutano huu, tumeridhia kushirikiana na taasisi nyingine za haki za binadamu, uwakili na utetezi, ili kubaini namna bora ya kuishitaki Serikali hasa kama tutaona mwenendo wa suala hili hauleti tija,” alisema Simbaya.

  Alisema kwamba, Serikali na Jeshi la Polisi, vitoe utaratibu ambao utawawezesha wanahabari nchini kufanya kazi zao bila hofu wala dharau, lakini pia kutoa elimu kwa wanajeshi kuhusiana na jukumu lao katika taifa zima.

  “Mauaji ya Mwangosi ni ya makusudi na hasa kwa kuwa alikuwa chini ya mikono ya askari polisi, Mwangosi alifia mikononi mwa polisi, mauaji yake ni ya kikatili, kionevu, kinyama na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

  Mauaji haya yamelifedhehesha taifa ambalo wakati wote tangu mwaka 1961, limejipatia sifa ya kuwa na utulivu kiasi cha kupachikwa jina la Kisiwa cha Amani.

  “Mimi nilishiriki mazishi ya mwenzetu huyu, inasikitisha sana, marehemu alikuwa mtu mzima mwenye afya njema, lakini jeneza lake lilikuwa kama la mtoto mdogo, kwa sasa Jeshi la Polisi siyo rafiki tena wa wanahabari, tunaomba tamko hili lingetuelekeza kususia shughuli za Jeshi la Polisi hadi upelelezi utakapokamilika na kuiona haki inatendeka,” alisema Simbaya.


  Jukwaa la Katiba
  Katika hali ya kuonyesha kutoridhishwa na mauaji ya Mwangosi, Jukwaa la Katiba Tanzania, limesema Serikali inatakiwa kuitunza familia ya marehemu Mwangosi.

  Pamoja na hayo jukwaa hilo limesema kitendo cha mwandishi huyo kuuawa akiwa kazini, kimetia doa mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya unaoendelea kwa sasa.

  Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana, kwamba kutokana na kifo cha mwandishi huyo, kamwe Jeshi la Polisi haliwezi kujinasua katika suala la kutunza familia ya marehemu.

  “Tunapenda kutoa rai kwa Serikali itangaze rasmi, kwamba itachukua jukumu la kutunza, kusomesha, kulisha na kuhudumia familia aliyoiacha Daudi Mwangosi kuanzia sasa, kwa muda wa miaka 20 baada ya watoto wa marehemu kuanza kujitegemea.

  “Itakuwa ni fedheha kuiona familia aliyoianzisha marehemu Mwangosi ikisambaratika, kwa sababu kichwa cha nyumba hiyo kimesambaratishwa na bomu la polisi, ambalo kodi ya marehemu ilichangia kulinunua.

  “Kama ilivyokwishaelezwa na wengi, kifo cha mwandishi huyo ni cha kwanza cha aina yake katika tasnia ya habari nchini na kinatishia si tu uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa habari, bali pia kifo hiki na vingine vya siku za karibuni, vinauweka mchakato wa Katiba Mpya njia panda.

  “Vitendo vya mauaji ya raia vinazidi kushamiri siku hadi siku, wapo wananchi wanaouawa na watu wanaoitwa wenye hasira kali kwa tuhuma za uhalifu, ingawa haki ya kuishi inayowekwa na kulindwa na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanza kuingia dosari Tanzania.

  “Roho za Watanzania zinazidi kupotea kutokana na udhaifu mkubwa unaosababishwa na rushwa na mambo mengine ya ukosefu wa maadili katika vyombo vya usimamizi wa haki.

  “Jeshi la Polisi linalotumia risasi za moto, mabomu ya kivita, maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi dhidi ya raia ambao hawajabeba hata fimbo za kuchungia mifugo, ni jeshi lisilojiamini na linaloonyesha woga wa ajabu.

  “Kwa hadhira kama za Nyololo (Mufindi), Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam na nyinginezo za miezi ya hivi karibuni, Jeshi la Polisi, lingeweza kuwatuliza wananchi kwa kutumia filimbi tu.

  “Matumizi ya nguvu na kumwagia maji ya kuwasha hata wazee wastaafu wanaodai haki zao, inaweza kuwa ndiyo laana inayopelekea polisi kusikia furaha kuua kila mara.

  “Mikusanyiko mingi ambayo imepelekea mauaji wakati polisi wakijaribu kutawanya watu ni matukio yaliyolenga kupata majibu ya kisiasa na siyo ya kipolisi.

  “Tabia inayozidi kushamiri ya Jeshi la Polisi kutaka kujibu au kuzima hoja za kisiasa au kiuchumi kwa mtutu wa bunduki, mabomu, maji ya kuwasha na virungu ni tabia ya jeshi kutaka kuingilia kazi isiyo yake na ndio maana inawashinda. Kama polisi wangekuwa ni wataalamu wa siasa, wangegundua kuwa wanachokifanya ni kuahirisha matatizo na si kuyatatua.

  “Jeshi la Polisi na vyombo vyenye dhamana ya ulinzi, lazima vijitambue upya kuwa vina wajibu wa kulinda raia, mipaka na mali zao na siyo vinginevyo,” alisema Kibamba na kuongeza.

  “Athari za matukio ya mauaji na fujo zinazosababishwa na Jeshi la Polisi kutawanya waandamanaji au mikusanyiko mingine ni kubwa sana katika kuathiri vibaya hamasa ya wananchi kwenye mchakato wa Katiba.

  “Kwa mwenendo wa sasa, Jeshi la Polisi litakuja kupiga mabomu na kuua hata wananchi watakapokuwa katika mabaraza ya Katiba wakijadili na kupinga baadhi ya vipengele vitakavyoingizwa katika rasimu ya Katiba.

  “Mikusanyiko, maandamano na shughuli za mikutano ya siasa ni matendo halali na haki ya kila Mtanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ibara ya 8, 20 na 21.

  “Tabia iliyoota mizizi ya polisi kujiona kama wamepewa taarifa ili watoe au kukataa kibali ni uelewa finyu wa Katiba na sheria za nchi,” alisema Kibamba.


  TCD
  Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kimesema kitakwenda kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kujadili mauaji ya raia wasio na hatia kwenye mikutano ya kisiasa.

  Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa TCD, James Mbatia, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya kisiasa nchini.

  Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, alisema Baraza la Utendaji la kituo hicho, limeagizwa kuandaa rasimu ya maadili itakayovibana vyama vya siasa, Serikali na Jeshi la Polisi pindi watakapokiuka maadili hayo.

  “Jana (juzi) wajumbe wa kituo hiki ambacho kinaundwa na vyama sita vyenye uwakilishi bungeni, walikaa na kupitisha azimio la kuonana na Waziri Mkuu, ili kujadiliana juu ya matatizo yanayojitokeza nchini na jana (juzi) saa tisa mchana, nilipeleka barua ya wito wa kuonana naye sasa tunasubiri jibu kutoka kwake.

  “Tukifikia makubaliano, itakuwa kama aina fulani ya mkataba ambao vyama vya siasa, Jeshi la Polisi na Serikali vitasaini ili kukubaliana kuwa atakayekiuka maadili ya rasimu hiyo, achukuliwe hatua na umma wa Watanzania.

  “Kwa sababu pamoja na Tanzania kusaini mikataba ya kimataifa ya usawa wa kibinadamu, bado utekelezaji wake ni mbovu kutokana na mfumo mbovu na uzembe wa watawala.

  Waandishi Tarime nao wachachamaa

  Waandishi wa Habari Wilayani Tarime, Mkoa wa Mara, wamesusia sherehe za Polisi Day, Kanda Maalum ya Tarime Rorya zilizofanyika jana.

  Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walifikia uamuzi huo kama sehemu ya kuungana na wenzao nchini waliokubaliana kutofanya kazi na Jeshi la Polisi.

  Katika utekelezaji wa mgomo huo, waandishi hao waligoma kuitikia wito wa Kamanda wa Polisi, Tarime Rorya, Justus Kamugisha aliyewataka wahudhurie sherehe hizo mjini hapa.

  Pamoja na kususia sherehe hizo, waandishi hao walionyesha kutoridhishwa na tukio la mwaka jana, ambapo waandishi wa habari walikamatwa wakati walipokuwa wakifuatilia mauaji ya watu watano katika Mgodi wa Dhahabu wa Nyamongo.

  CHADEMA wahoji kamera ya Mwangosi

  Mkuu wa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila, alisema chama chake kinataka kujua kamera ya marehemu Mwangosi iko wapi.

  Pia alisema kwamba, kabla Mwangosi hajauawa, alimwambia Kigaila kuwa, ana wasiwasi juu ya uhalali wa askari waliokuwa katika operesheni ya kuwadhibti wafuasi wa CHADEMA dakika chache kabla hajauawa.

  “Marehemu Mwangosi aliniambia ana shaka na askari waliopo eneo hilo na alikuwa ameniahidi kwamba atanionyesha picha za askari asiowafahamu licha ya kufahamiana na askari wengi mkoani hapo.

  “Wakati akiniambia hivyo, baadhi ya polisi walimsikia na huenda hiyo ndiyo ikawa sababu ya kumng’ang’ania na kusababisha kifo chake.

  “Kama kweli polisi hawakuhusika katika tukio hilo, tunataka kujua vifaa vya kazi vya marehemu kama vile kamera, kompyuta ndogo viko wapi.

  “RPC tunataka atueleze kamera ya Mwangosi iko wapi, begi na Laptop viko wapi, na kama vitu hivyo vipo kwa nini wapo kimya, kuna uwezekano picha zilizokuwemo mle ndani ya kamera waliona zitawaumbua ndiyo maana wameficha kamera hiyo,” alisema Kigaila.

  Alisema kuwa, imekuwa ni kawaida kwa chama cha mapinduzi kuwavalisha raia nguo za jeshi na wakapewa vitambulisho vya jeshi na kufanya kazi hiyo, huku baadhi ya askari nao wakituhumiwa kwa kuvalishwa magwanda ya CCM na kufanya kazi ya CCM.

  Naye Hamad Mussa Yussuf, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, alisema wakati Mwangosi anauawa alikuwa jirani naye na kwamba askari aliyejeruhiwa kwa bomu wakati Mwangosi anauawa, alikuwa akimuokoa marehemu, baada ya kuona anapigwa na askari polisi bila sababu.

  “Nilimsikia yule askari akisema mwacheni huyo ni mwandishi, alimfuata Mwangosi na kumkumbatia huku akiwazuia askari wale wasiendelee kumpiga na wakati huo kulikuwa na askari mmoja amemwelekezea bunduki tumboni,” alisema Yussuf.

  Habari hii imeandaliwa na Arodia Peter, Elizabeth Mjatta, Gabriel Mushi, Dar es Salaam, Timoth Itembe (Tarime) na Oliver Richard, Iringa.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Very GOOD START... Nchi za EUROPE zaanza kuishtukia Serikali ya kiulaghai ya CCM; SWEDEN... tunahitaji Nyingine Nyingi hadi

  NAPE na Wenzake wapate Vumbi na kujiuzulu...
   
 3. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shuka ndo linafuliwa na ni usiku wa saa3 sjui nn kitaendelea, na wenzetu wakishikilia msimamo ni huo. Naisubiri marekani ikiamka mjue CCM kushney hata kama wanataka kuwahonga Uranium.
   
 4. m

  majebere JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Africa watu wanakufa kila siku kama mbuzi na hakuna wazungu wanalo lifanya zaidi ya kutoa vineno viwili vitatu halafu imepita.
   
 5. m

  majebere JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Hao wamarekani watakua wamekosa kazi ya kufanya, wasiende syria waje huku kisa mtu mmoja kauwawa wakati nchi zingine wanakufa maelfu. Nyie mnaota ndoto za mchana.
   
 6. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unakumbuka NIGERIA na kuuliwa kwa AMINA kwa mawe? Hii ni demokrasia na uhuru wa habari na ndio funguo ya midomo ya Marekani. Demokrasia hakuana umevunja uchumba na Marekani. Use your common sense!
   
 7. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Heri yako wewe uliyekata tiketi ya kuishi milele
   
 8. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo hili nalo litapita ili muendeleze unyama wenu!!Sawa kila la kheri
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Naona uko kikazi zaidi ehee!!! Endelea si tunakusoma tu.
   
 10. s

  sokoinei JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,835
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama hujui vifo vyote vinahesabiwa unahitaj kusomewa dua.hakuna mwenye ruhusa ya kuua hata kuku ndan ya dunia hii,kunasiku dam zetu zitajibu.waandish mnatakiwa mdai haki zenu ikiwa nipamoja nakulifungulia mwanahalis hakizetu zimekiukwa yani wazir anauwezo wakufungia tv redio yoyote!ee mungu kwanini nilizaliwa tz?inauma kutoa zawad malalio yetu inauma sana but ipo siku
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa mauaji yaliyotokea Waziri wa Mambo ya ndani ni mmoja ya watuhumiwa kwani polisi wako chini yake.Msajili wa vyama yeye huzinduka baada ya tatizo kutokea ni kero kweli.
   
 12. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Nape yeye na chadema tu haoni lingine hata agesalitiwa na mkewe haraka angesema chadema hao! Wakati mwingine mtu apime upepo unaendaje si kuropoka tu
   
 13. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ukombozi wa TZ utatokana na watanzania wenyewe na sio wazungu wanafiki wanaokuja kupora mali zetu
   
 14. Jaji

  Jaji Senior Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo mazito
   
Loading...