Taifa linapo mkosea Mungu

Taifa linapo mkosea Mungu

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,322
Reaction score
3,648
TAIFA LINAPOMKOSEA MUNGU.
Leo 12:15 hrs 17/09/2022

Taifa lolote linapomkosea Mungu,hukumu inakuja juu ya Taifa hilo, Mungu anaondoa neema yake juu ya Taifa hilo (No more grace,no more mercy, no more favour) hukumu inakuja kutokana na matendo yasiyofaa ya Taifa hilo mbele za Mungu, kwa ujumla mambo yanayofanywa na kunenwa mbele za Mungu yakiwa ni machukizo,Tunaona hapa:-
▪️Maneno yenu yakiwa kinyume na Mungu.
▪️Matendo yenu yakiwa kinyume na Mungu
▪️Nyuso zenu zikionesha hatia mbele za Mungu juu ya dhambi zanu bila kutubu.
▪️Dhambi zenu zikiwa wazi wazi kama Sodoma na Gomora,kufanya dhambi bila kificho chochote kile, maisha ya dhambi yakiwa kawaida katika jamii yenu, mmezoea basi hukumu ya Mungu itashuka juu yenu shida na matatizo yatawaandama.

-Hukumu ya Yerusalemu na Yuda

Mungu anaitaarifu nchi ya Yuda kuipiga mapigo matatu,mapigo ya Upungufu wa chakula katika nchi ya Yuda,Upungufu wa Maji, na Upungufu wa Viongozi katika Yuda huu ni unabii katika kitabu cha Isaya 3:1-7

🔸Mungu anaruhusu kuondoka watu wa kila kada walio na msaada kwa taifa la Yuda kama vile:
*Mashujaa wa vita
*Mwamuzi wa Taifa
*Nabii ataetoa unabii juu ya Taifa
*Mpiga ramli
*Mzee (wenye hekima)
*Majemedari wa vita
*Washauri
*Mafundi stadi
*Waganga/matabibu

Unabii huu wa kuondolewa watu muhimu katika taifa la Yuda ulikuja kutimizwa kwenye 2 Wafalme 24:14.

Mungu aliahidi kuruhusu taifa la Yuda kukandamizwa na watesi,kutokana na ukosefu wa viongozi na watu wakuu katika taifa basi katika ngazi za kifamilia watatamani waongozwe na yoyote tu ili mradi taifa liende,lakini bado hata hao watakataa kutokana na uhaba mkubwa wa chakula na shida mbalimbali zinazojitokeza kila siku na kukosa viongozi muhimu wa kuliongoza Taifa hilo.

Ni hukumu kubwa sana kwa Taifa, Jaribu kuwaza nchi kama yetu iondokewe na watu wote muhimu ni pengo kubwa sana kwa taifa na maendeleo yake. Lakini yote haya ni matokeo ya dhambi na uasi wao mbele za Mungu,nae Mungu analipa adhabu Taifa kwa kuondoa maono ya Taifa hilo na watu wa kuliongoza Taifa hilo.

Hasira ya Mungu ilishuka juu ya Yerusalemu na Yuda baada ya kutenda matendo yasiyo mpendeza Mungu,Isaya 3:1-5 Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi akaondoa kutoka Yerusalemu na Yuda kila tegemeo.

Tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la kinywaji, Mungu akaondoa mashujaa na askari ,waamuzi na manabii, waaguzi na wazee, majemedari wa vikosi vya watu hamsini na watu wenye vyeo, washauri, wachawi stadi na walozi hodari, (Mungu ataweka watoto wawatawale) naam, watoto wachanga watawatawala.

Watu watadhulumiana,kila mtu na jirani yake;vijana watawadharau wazee wao, na watu duni watapuuza wakuu wao,haya yalitabiriwa, Yerusalemu na Taifa la Yuda waliambiwa na yakatimia kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha 2 Wafalme 24:14

Maovu yalipelekea Taifa lote kupata hukumu kutoka kuwa Mungu.

-Mungu anaahidi uheri kwa wenye haki wake Isaya 3:10. Ijapokuwa wataonewa na kupitia shida toka kwa wanadamu waovu sababu ya haki yao, bado Mungu anawatia moyo kuwa watalipwa mema, si katika ulimwengu huu tu hata ule ujao, yapo matunda ya matendo yao, Waovu wote wanapewa ole na onyo kuwa watavuna kile walichokipanda Isaya 3:11 apandacho mtu ndicho atakachovuna,Viongozi wasio na uwezo watainuliwa kutawala kwa sababu ya hukumu.

Tutaona watoto na wanawake kulitawala taifa kutokana na maovu,Hii ilikuwa ni ishara ya taifa kulaaniwa katika nyakati hizo na kwa tamaduni za Yerusalemu na Taifa la Yuda, na mwisho walipelekea taifa la Yuda kupotea njia na mwelekeo mbele za Mungu Isaya 3:12. Si kwamba ni mbaya kwa wanawake kuwa viongozi, tunaona Mungu alimwinua Debora kuwa mwamuzi kwenye taifa la Israeli (Waamuzi 4-5) na hata Esta, hoja kuu hapa ni kuwa taifa zima lote kuongozwa na wanawake tu peke yao, haikuwa ishara nzuri kwao, mahali ambapo tamaduni na mila zao mwanaume ndiyo alikuwa mwenye sauti na mamlaka.

Nimalizie kwa ushauri ufuatao, Mojawapo ya laana kwa taifa au njia ya hukumu ya Mungu dhidi ya taifa ni pale anaporuhusu viongozi wasio na uwezo kutawala,Jambo hili liliwapata Yuda kutokana na uasi wao, Mungu akawaondolea wale waliokuwa nguzo kwenye jamii yao na kuwaacha dhaifu ili wawaongoze, Madhara yake yanaweza yasionekane mapema lakini yataonekana tu kadri muda unavyokwenda, kikubwa ni watu kutubu na kutafuta rehema za Mungu, Viongozi wana mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa lolote lile, hivyo wakiwa imara na wacha Mungu, mambo yatasonga, bali kinyume na hapo ni maumivu ndani ya taifa hilo, Maneno tunayosema na matendo tutendayo yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu ni dhambi, huu ni ukweli usiopingika, Si tu matendo hata maneno tunayoongea yanaweza leta ghadhabu ya Mungu juu yetu binafsi na hata taifa, tujitahidi kuchagua aina ya maneno ya kuongea mbele za Mungu, tuishi maisha yetu katika standards za Kimungu pia.

Mungu anachukia maskini wanapoonewa, Taifa linajiingiza katika shida pale maskini wanapoporwa haki zao na watawala au watu matajiri, Ni uovu mbele za Mungu kuwadhulumu maskini haki zao na kujilimbikizia mali, Mungu hapendi mambo hayo kwa watawala yanaliingiza taifa katika shida na laana pia, Mungu anatarajia wanawake wote wawe na nidhamu na hofu mbele zake, kiburi na kujiona wazuri na bora kuliko wengine ndilo jambo lililowagharimu mabinti wa Yuda. bado, Mungu anataka unyenyekevu mbele zake, Uzuri ni ubatili bila Mungu, Ni muhimu mabinti na wanawake wasiomcha Mungu wakatambua hilo na kutubu na hata wamchao nao wanatakiwa kuendelea kunyenyekea mbele za Mungu.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty reduction.
 
Ulali wa Agano la Kale na Agano Jipya (Testament)

Mambo ni tofauti sana sivyo kama jinsi yalivyo

Miili yeti ndilo Hekalu la Roho wa Mungu sio hii ardhi

Twende polepole tutaelewana
 
mambo ya kusadikika hayo, mabudha wa huko asia wanaabudu miungu yao ya ajabu na hwajawahi kupungukiwa chochote
 
Asante mtumishi!!

MUNGU akubariki,

Next time usisahau kuhitimisha HIVI;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba mpya"
 
Back
Top Bottom