La kushangaza nondo za CCM kuendelea kutesa ni................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

La kushangaza nondo za CCM kuendelea kutesa ni.................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 24, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,442
  Likes Received: 418,957
  Trophy Points: 280
  Wale adui watatu ambo tuliambia na CCM/TANU/ASP wangeliwatokomeza kumbe ndiyo lulu sasa kwa CCM ili kuendelea kututawala bila ridhaa yetu.

  Adui hao ni umasikini, ujinga na maradhi.....

  Kwa umasikini wanatuahidi kutuhonga miundo mbinu lukuki ili tuendelee kuwachagua na wako tayari kuwanunua mawakala kutokana na umasikini wetu ili wachakachue matokeo na kuibuka kidedea kwenye chaguzi hii........

  Miaka takribani 50 tangu tupate uhuru bado CCM wanazungumzia kujenga zahanati, hospitali za rufaa n.k kazi ambazo ungelitegemea ziwe zilikamilika miaka 30 iliyopita.....

  Leo tunaahidiwa shule za kata, nyumba za waalimu, malipo saawia kwa waajiriwa kwenye fani hii kazi ambazo zingelikuwa zimekamilishwa miaka 30 iliyopita.

  Hoja ya kimsingi mbona umasikini, maradhi na ujinga vinaendelea kuongezeka kwa kasi ya kutisha kama kweli siyo sera ya CCM kuwatumia adui hawa kama ndizo nondo zake za kutukandamiza?

  Chaguzi hii tujiulize kama kuna uhaja wa kuendekeza ghiliba hizi za CCM au la.......
   
Loading...