La katiba wabunge myakumbuke ya Late Chiruba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

La katiba wabunge myakumbuke ya Late Chiruba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Danniair, Nov 16, 2011.

 1. D

  Danniair JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katiba ya nchi ni kwa faida ya wote. Wakati Chiruba akiingia Madarakani iliundwa katiba ili kumlinda yeye , chama chake na washirika wake, huku ikiwakandamiza wapinzani kama kwamba nchi ilikuwa ni kwa chama chake tu. Eloi bariki ikafika siku naye akapigwa chini na ile ile katiba ikaanza kumtafuna kama ilivyokuwa ikitafuna wenzake,"Malipo juu ya uso wa dunia". Sote tunaelewa jinsi alivyolalama akitaka serikali mpya kuibadili katiba aliyoitunga yeye mwenyewe na kuitumia kwa furaha.

  Ushauri; waheshimiwa wabunge, hakuna aliyeiona kesho na hakuna chama kitakacho tawala nchii hii milele. Tujifunze ya chiruba na tuamue mambo yenye faida kwa kila mtanzania.
  Rais; Tumia busara kabla ya kuusoma mswada huu na kuutia sahihi. Tumia wapelelezi wako kujua m-tz anataka nini. Ukiliangalia bunge limegawanyika, kwa nini? Tumia busara kusahini kitu ambacho kila mtu anakililia na makubaliano yasiyo na mgogoro. Ukiwasikia wabunge wanaounga mkono mswada utaona lugha yao ni moja kejeli na kujipendekeza. lugha yao haimwambii m-tz kwamba jambo hili lina amani bali UBABE wa kwa nini fulani aseme. Ukitazama wale wa upinzani wa mswada huu ni dhahiri wanayoyasema ndiyo yanayotakikana ukizingatia wa-tz wengi ni walala hoi na wapinzani wameliteka kundi hili kwa hiyo linawakilisha mawazo hai kabisa ya wa-tz. Kundi la wanaounga kama Mh. Kombania alivyosema leo starTV limo ktk wale waliopewa jukumu la kuongea na wa-tz na ndilo kubwa, lakini hapa nilipo sijawahi kusikia matangazo ya mwananchi kuelekea kwenye kikao chochote cha mbunge kwenda kusikiliza maoni ya KATIBA. Rais wetu Eloi akujalie busara na hekima. Kama unahisi unapungukiwa hekima omba kama Mfalme Selemani. USIONE UVIVU. Omba.
   
Loading...