Kyela mafuta hakuna wiki tatu sasa

Kabinti ka ludilo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
409
461
Wakuu heshima kwenu,

Nasikitika kuwatangazia kuwa, eneo la Kyela halina mafuta kwa wiki ya tatu sasa.

Inasemekana depo ya kutunzia mafuta huko Dar es Salaam wauzaji mafuta wamegoma kuaupply mafuta sheli ndogo za mikoani.

Kinachoshangaza Ni kuwa sheli za eneo la boda na Tukuyu hata mbeya jiji mafuta yapo.

Ifahamike kuwa kyela Ni eneo tambarale hivyo matumizi ya mafuta Ni makubwa Sana kwani kuna idadi kubwa sana ya pikipiki.

Tetesi zinasema huenda kuna mgomo wa mafuta kutokana na kushuka sana kwa bei.

Wachuuzi wa mafuta wakati huu maarufu kama njemke wamejipatia ukwasi mkubwa kwa kuuza mafuta kwa bei inayofikia 4000 kwa lita.

Wakati haya yakiendelea, Aliyewahi kuwa mbunge wa kyela, Dr msomi Harrison Mwakyembe, yupo Jimboni na anazunguka kila kata na vijiji kukutana na viongozi wa chama na kuitisha mikutano ya kiserikali kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Akiwa katika kata ya kiutawala ya Mwaya ameeleza kuwa anawahurumia wananchi wa Mwaya kwani walisahaulika muda mrefu kutokana na yeye kutingwa na majukumu ya kitaifa.

Nitaendelea kuwapa habari zaidi
 
Kuweni makini uchaguzi ujao, la sivyo mtakosa hata chakula mkiendekeza ccm.
 
Back
Top Bottom