Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
WATUMIA TREKTA KUSAFIRISHA MAITI
Wananchi Wilayani Kyela wanalazimika kutumia gari aina ya trekta kusafirishia maiti baada ya magari mengine kushindwa kupita katika barabara ya mwaya baada ya kuharibika vibaya kutokanana mvua zinazoendelea kunyesha.
Mkazi wa kijiji cha Mwaya Juliana Mwamaja alisema juzi alifiwa na kaka yake hospitali ya wilaya walitumia usafiri wa trekta kusafirisha maiti hadi kijijini kutokana na magari mengine kushindwa kupita njia hiyo.
Kutokana na hali hiyo alioma halmashari kuifanya matengenezo barabara hiyo ambayo inategemewa na wananchi wa vijiji vya mwaya na lughambo.
“serikali iliangalize tatizo hili kwa jicho la tatu ili kuokoa maisha ya wananchi ambayo yamo hatarini pia bidhaa kwenye maduka na zimepanda bei kutokana na wafanyabiashara kutumia usafiri wa majini wakitumia fedha kuvuka “ alisema.
k