Kilosa: Watumia punda na machela kusafirishia wagonjwa kisa hakuna barabara

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,835
Watu wa Mjini Huwa wanadhani Kila sehemu ya Nchi hii maisha ni simple kama kwao.

Hii ndio Hali halisi ya sehemu kubwa ya Tanzania japo Serikali inajitajidi sana kuweka Juhudi but kazi inatakiwa kuongezeka zaidi.

=====

Screenshot 2023-09-25 145030.png

Wakazi wa Kata ya Uleling’ombe wilayani Kilosa mkoani Morogoro wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo hilo hali ambayo imekuwa kikwazo kwao kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji mali ikiwemo usafirishaji wa bidhaa za mazao kwenda katika masoko mbalimbali.

Hali hiyo imesababisha wakulima kutumia usafiri wa punda kusafirisha mazao yao kupeleka katika masoko na wagonjwa kubebwa kwenye machela kwa ajili ya kupelekwa kwenye matibabu pale wanapopatiwa rufaa za kimatibabu.

Baadhi ya wakazi wa Kata hiyo wakizungumza na waandishi wa habari wilayani hapa kuhusu ubovu wa miundombinu hiyo wamesema pamoja na kuwa kikwazo katika shughuli za kiuchumi pia imekuwa kero kwa wagonjwa na wajawazito kushindwa kusafirishwa pale wanapopatiwa rufaa za kimatibabu

Mmoja wa wakazi hao wa kata hiyo Michael Kitime, amesema tangu uhuru eneo hilo halijawahi kuwa na barabara nzuri ambayo inaweza kutumika kupitisha magari.

“Suala la barabara hapa tangu uhuru barabara iliyokuwepo ni ile iliyochimbwa na wananchi ambayo nayo inatumika na punda siyo magari hali hii imesababisha kata yetu kuwa masikini katika jimbo hili la Mikumi kuliko eneo jingine mkoani Morogoro.

“Vijana wengi hapa wanajitahidi sana kulima mazao ya biashara lakini usafiri hakuna barabara wanalazimika kutumia punda karne hii ya 21 kweli bado sisi tunatumia punda kusafirisha bidhaa na kutumia machela kubeba wagonjwa wamepita wabunge wengi ambao wanamekuwa wakiahidi wakati wa kampeni kutujengea barabara lakini wanapochaguliwa hakuna kitu kinafanyika”amesema Kitime

Aidha, amesema hali hiyo imesababisha hata watumishi ambao wanapangiwa kituo cha kazi katika Kata hiyo kuomba uhamisho kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya barabara.

“Kata hii ilianzishwa mwaka 1982 lakini hadi sasa hakuna maendeleo yoyote ukilinganishwa na Kata zingine tulizoanza nazo hadi leo tunatumia punda tupo enzi za ujima kama kunakosa tulifanya serikali iseme ili tutubu watuletee maaendeleo” amesema.

My Take
Serikali ongezeni Bajeti ya Tarura badala ya kujaza mapesa kibao Dar tuu.Bil.800 ni pesa kiduchu sana Kwa Nchi nzima.

View: https://www.instagram.com/p/CxmiRIdsmpx/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Acha kuisingizia serikali ya ccm.
Barabara zimejengwa kila kona tena lami zote.
Kidumu chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom