Na awamu hii wale jamaa wanaojifanya hawajulikani,cha ajabu kila mtu anawajua.
Ni kikosi maalum cha utekaji kilicho chini ya serikali ya awamu ya tano.
Mi niwashauri viongozi wa awamu hii,kwamba..ukiwa rais,waziri ama kiongozi mahali popote lkn hasa raisi,
Ujue kwamba madaraka uliyo nayo ni makubwa sana.
Una watu zaidi ya milioni 55 wanaokuangalia kama baba yao.
1)Si wote wanataka uwe rais wao,kama ilivyo kwa familia,si watoto wote wanampenda baba yao.
Lkn baba anawapa chakula,nguo, malazi na elimu bila kubagua.
Baba hawaui watoto wasiomoenda.
2)Baadhi ya raiya wana matatizo mbali mbali ya kimaisha,labda kuna kitu wanakosa ktk utawala wako,na watakuambia kadiri ya mawazo yao na lugha yao inaweza kuwa ya maudhi,hata hivyo kama baba yao huwezi kuwaua.
3)Wapo wanaotamani nafasi yako,kwa hiyo watasema lolote ili uonekane unakosea. Hupaswi kuwasikiliza,wajibu kwa ukweli.
4)Wapo wanaoona mapungufu yako na wanakuambia,haidhuru kwa lugha yoyote,
Tafuta ukweli ktk hoja yao,ikiwa kuna ukweli basi kumbuka,wewe hukuwa bora kuliko wengine,wewe ni mdhaifu kama walivyo binadamu wengine jisahihishe na maisha yatasonga mbele
5)Kuteka,kutesa na kuua watu wako mwenyewe hakuwalazimishi watu wakuheshimu na wakupende.
Badala yake wanakuchukia zaidi na zaidi,wala hutakuwa na heshima.
Utadharaulika kuliko tawala za awamu zote zilizopita.
6)Upo msemo wa waswahili kwamba:mtoto akikunyea mkononi huukati mkono wako,bali unausafisha na maisha yanaendelea.
Nisiseme sana ili ninyi mnaojiita manyang'au msije kuniteka,nilikuwa nawashauri tu.
Wala siwalazimishi