Kwinyara kwinyara Tumia lugha nzuri kukosoa

Kwinyara kwinyara Tumia lugha nzuri kukosoa

Mimi kama mtanzania ,naomba nitoe ushauri kwa kijana huyu wa chadema ,ambaye anatumia lugha Kali kukosoa na kutukana viongozi mitandaoni, naomba nimkumbushe hii awamu ni tofauti, akipotea au kutekwa ,watakaopata tabu ni familia na ndugu zake , maana viongozi wake wa chama wanaishia kushinda fb na tweeter wakipost tu, wana jf watasema R.I.P kwinyara na atasahaulika,

Naomba nimkumbushe kwinyara kutumia lugha nzuri tu, awamu hii ina manyang'au yatamfanya kama wenzake , .

Niishie hapo, mlio karibu naye mpeni huu ushauri ,

NA LAZIMA UJUE KUWA WATANZANIA WA SASA SIO WAJINGA NA WAKATI PIA UMEBADILIKA ,CHECK AL BASHIR SUDAN !

YUPO JELA ILEILE ALOTUMIA KUWAWEKA NDANI WAPINZANI.

KUTEKA WATU NI USHAMBA WA HALI YA JUU,

UJANJA NI KUKAMATA NA KUFUNGULIA MASHTAKA WATU ! THEN HAKI ITENDENDEKE !!

SIKU ATAKAPOTEKWA NDUGU YAKO WA DAMU NDIPO AKILI ZAKO ZITAKURUDIA.
 
My fellow Gooner fun kumbe upande huu una mambo ya ovyo sana. Kwa hiyo mtu akikutukana kwa lagha yenye maneno makali adhabu yake ni kifo?. Pathetic....
Rafik yangu umenielewa vibaya, simaanishi hivo, maana yangu ni hii tukosoe kwa lugha nzuri maana tutazipa taabu familia zetu, huku viongoz WA chama wakitweet tu na kulaani
 
NA LAZIMA UJUE KUWA WATANZANIA WA SASA SIO WAJINGA NA WAKATI PIA UMEBADILIKA ,CHECK AL BASHIR SUDAN !

YUPO JELA ILEILE ALOTUMIA KUWAWEKA NDANI WAPINZANI.

KUTEKA WATU NI USHAMBA WA HALI YA JUU,

UJANJA NI KUKAMATA NA KUFUNGULIA MASHTAKA WATU ! THEN HAKI ITENDENDEKE !!

SIKU ATAKAPOTEKWA NDUGU YAKO WA DAMU NDIPO AKILI ZAKO ZITAKURUDIA.
Umenielewa nilicholenga lakini?
 
Kwani Sheria unasemaje kuhusu kutukana? Inasema anatukana au kukosoa kwa lugha adiyoipenda mkosolewaji apigwe risasi au atekwe?
Tatizo utawala huu haujui cha sheria wala mtoto WA sheria ,hivo wakosoaji wawe makin maana zinazoumia ni familia zao ,huku washadadiaji wakubwa mnasubir watekwe muandike BRING BACK flan
 
Kuna maneno ya kukosoa yanakua personal attack na abusive language jambo ambalo linaondoa maana ya ukosoaji hata kama una nia njema,maana mkosolewa akiona umetumia matusi mengi zaidi kuliko hoja anadhani ni mhuni tu na hata zingatia
Tatizo ni kutaka sifa....wanashindwa kutofautisha kati ya kukosoa na kutukana.
 
Serikali imetukanajwe? Tuwekee hayo maneno ya kuitukana serikali....
Usituambie kusema ukweli ni matusi, mana kweli siku zote huuma kama si kuchoma mioyoni mwa wanaoambiwa...
Serikali ikubali kukosolewa ili irekebishe changamoto....no way out.


Matusi mnayotukana ni mengi sana.

Msipoacha mtapigwa tu! Na Mimi ninasema mpigwe tu maana hakuna namna.

Umeambiwa acha hutaki, sasa unataka nini zaidi ya kushughulikiwa??
 
Kama ndugu kwinyara ana akili timamu, afuate ushauri wa mkuu AROON na mkuu Aikambee

Kama ana akili timamu lakini!

Watanzania hawadhaminiki, kama anataka kuwa dhamana ya watanzania ajitafakali upya.
Wanaoshabikia kuwa aendelee kutukana ,akipotea wanakaa nyuma ya keyboard kusema Bring back....

Na kusema R.I.P huku kina mbowe wakitweet TUNALAANI...
 
Badilikeni na lugha itabadilika toka lugha ya kuuzi mpaka hiyo nzuri unayoitaka....

MF. Albert Bashite tutamwita Akili ndogo badala ya Ziro brain.., au Mr ovyo ovyo. Endapo tu atatubu na kubadilika

Hapo atakuwa awachoshi wakubwa zake kumuombea msamaha madhabahuni.

Yaani hakuna jina zuri la mtu Fisadi, Mwizi Malaya, Mzushi, Mfitini kama hizo ndio tabia zake...

Dikteta ni Dikteta hata kama ni Uchwara, ili mradi tu ana vitendo na vitabia vya kufanana na hivyo.

Serikali isiyochukia na kupambana na Rushwa kwa vitendo na wananchi wake wakaona...hiyo tunaita serikali ya kifisadi na viongozi mafisadi...hakuna neno zuri zaidi ya hapo.....so mwache kwinyara azidi kukosoa ili mradi avunji sheria....


Uwezi kukosoa unga juhudi wala sio kosa...dhamiri yako ndio itakusuta.
Jiulize toka muite hayo majina ya kuudhi je wamebadilika? Wanaoumia ni kina nani?? Mbona wanaotukana ndio wanazidi kuumia ,huku washadadiaji wakibaki mitandaoni wakisema TUNALAANI

lkn familia za watukanaji ndio zinaathirika
 
Lugha nzuri kwa manyang'au ikoje hiyo ambayo itayafurahisha? Nyang'au ni nyang'au tu yeye mwenyewe siyo mstaarabu anastahiri lugha tofauti.
Hizo lugha tofauti mwisho WA siku mnaoumia ni nyinyi ,kumbuka wao ndio wameshika mpini
 
Alipotea Mo Dewji watu tukaishia kutamanishwa na ile bilioni moja, sembuse huyu muungwana ambaye hata sura yake watu hawaifahamu.
 
MAKAMANDA WEKENI NAMBA YA KUMCHAGIA MDUDE. TUSIIJIFICHE NYUMA YA MKIA WA MBUZI
 
Jiulize toka muite hayo majina ya kuudhi je wamebadilika? Wanaoumia ni kina nani?? Mbona wanaotukana ndio wanazidi kuumia ,huku washadadiaji wakibaki mitandaoni wakisema TUNALAANI

lkn familia za watukanaji ndio zinaathirika
Harakati za ukombozi ni zaidi ya familia.

Fisadi, Mwizi, Mhujumu Uchumi utumie jina gani zuri, ili akuelewe....

Bunge Dhaifu, Spika Dhaifu utumie jina gani tofauti na udhaifu ili wakuelewe....

Masuala ya kuteka watu na kuua watu hayasaidii

Muhimu ni kusikiliza kilio cha wananchi ambao ndio chimbuko la serikali . ....


Vinginevyo endeleeni kujitutumua kama Chatu na Kifutu.....iko siku mtashushwa....nimekumbuka maneno ya Baba Askofu Dk. Shoo.


Dk. Bashiru. Katibu wa Chama anaelewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom