Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Wakuu nina mjomba wangu anasumbuliwa na kwikwi. Tafadhali anayejua dawa naomba anijuze. Natanguliza shukran
 
Dawa ya kutibu Kwikwi Chukua mua mweusi Kamua upate maji yake Glasi 1Uchanganye na Kijiko 1 cha Asali safi ya nyuki unywe kutwa mara 3 kwa siku 3 inshallah atapona. Atumie Mjomba wako hiyo dawa akisha pona uje unipe maendeleo ya Dawa yangu Give me a feedback mkuu.@chamlungu

Attachments

  • stock-photo-black-sugarcane-isolated-on-white-54141133.jpg
    stock-photo-black-sugarcane-isolated-on-white-54141133.jpg
    8.8 KB · Views: 295
Pia anywe maji kama nusu lita huku anaziba pua ili kutokuruhusu hewa kupita akifanya hivyo kwa siku mara tatu atapona.
 
Achukue kijiti cha kiberiti, akiwashe, kikiwaka akizimishie kwenye glasi iliyo na maji ya kunywa ya uvuguvugu, na kisha anyanywe hayo maji.
 
Wakuu nina mjomba wangu anasumbuliwa na kwikwi. Tafadhali anayejua dawa naomba anijuze. Natanguliza shukran
Mkuu dawa ya kwikwi ya haraka sana ni maji ya kunywa..

Kwanza kabisa weka maji safi ya kunywa katika chombo cha kunywea maji i.e kikombe, glass etc

Pili, hii ndiyo hatua muhimu kabisa katika matibabu...

Fanya hivi....

Wakati utakapotaka kunywa maji, usinywee ule upande wa kawaida ambao huwa tunaweka mdomo na kupata kimiminika, hapana!
Jaribu kunywea upande wa pili ambako pua yako inaelekea, wakati ukinywa utaona unainama kadiri maji yanavyozidi kuisha kwenye glass yako!

Usihofu kudondoka! Hayo ndiyo matibabu yenyewe tena yasiyo na gharama duniani hapa! Hakikisha unakunywa bila kusimama (non stop drinking).

Baada ya muda kama dakika 1 hivi, kwikwi itakatika!

NB : USIPOONA MABADILIKO TAFADHALI WAHI HOSPITALINI UONANE NA WATAALAMU.

hii njiaimenisaidia sana mimi na jamii yangu,
Ashukuriwe mwalimu wangu wa sayansi darasa la kwanza mwaka 1999.
 
asante sana mkuu Excel, tutafanya hilo zoezi. Ubarikiwe
 
Achukue kijiti cha kiberiti, akiwashe, kikiwaka akizimishie kwenye glasi iliyo na maji ya kunywa ya uvuguvugu, na kisha anyanywe hayo maji.

Mkuu Madika nakushuru kaka. Nadhani hilo tutaanza nalo tuone matokeo
 
Wakuu nina mjomba wangu anasumbuliwa na kwikwi. Tafadhali anayejua dawa naomba anijuze. Natanguliza shukran

nimewahi ugua kwikwi kwa awamu mbili mara ya mwisho ni mwezi wa nane mwaka huu.ninapo sema kwikwi si kwikwi ya nusu saa bali ni kwikwi ambayo kuisha kwakwe ni wakati wa kulala na inapofika asubuhi anaanza tena hadi usiku wakati wa kulala. Kuhusu dawa nimejaribu mbinu nyingi zikiwemo hizo zilizo tajwa hapo juu lakini hazikufua dafu ingawa zingine zilituliza kwikwi kwa muda wa dakika kadhaa.Kwikwi iliyo nipata mwaka 2011 nilitibu kwa dawa za aina mbili kutoka hospitali moja ya dawa hzo ni pamoja na dawa za kusafisha kifua,kwa kwikwi iliyonipata mwaka huu nilipewa vidonge vinne ambavyo nilimeza siku mbili hatimaye kupona kwikwi kwa maranyingine.haya kazi kwa ndugu yangu kusuka au kunyoa.
 
Tafuta udi karaha katika maduka yanayouza dawa zakisuna, mpe atafune kisha ameze maji maji yake, kama nimgonjwa sana asiyeweza kutafuna mchemchie na maji kidogo sana kisha mpe kama vijiko viwili hivi. Mimi ilimsaidia baba yangu.
 
mpe tukio la kushtua palepale kwikwi inakoma - kuja kummrudia ni badae sana. nimeijaribu hii kwa wengi imefanyakazi. kwa mfano unamwambia fulani amegongwa na gari etc.

dawa ya MziziMkavu inaelekea ni suluhisho la kudumu ijaribu. hii ya kwangu haiponyeshi once and for all
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli akitumia dawa amepona haitarudia tena hiyo kwikwi mimi hiyo Dawa nimepata kwa babu yangu mjomba wake na mama yangu kwenye kitabu cha uganga MAKAH Huyo Babu yangu amefariki bado mimi mdogo mwaka 1970. Miaka 44 iliyopita.
 
Habari jf doctor... Nina ndugu yangu kuanzia jana ana kwikwi inayomuumiza hadi kufua haitulii naomba msaada wa haraka atumie nini ili ipoe??
 
Back
Top Bottom