britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 17,177
- 41,623
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Venezuela wa 2024, María Machado mpinzani aliyekuwa na nguvu na akimsumbua Maduro alizuiwa na Tume ya Uchaguzi (CNE) kugombea. Alipigwa "ban" ya kisiasa. Viongozi wengine wa upinzani waliokuwa na nguvu walikamatwa na kufungwa gerezani, kama vile Freddy Superlano na Roberto Abdul.
Wengine walikimbia nchi kunusuru maisha yao, wakiwemo Edmundo González Urrutia na Leopoldo López waliokimbilia Hispania. Maduro akabaki mgombea pekee mwenye nguvu.
Akavikusanya vyama 13 vya upinzani (vilivyo dhaifu) vikatangaza kumuunga mkono. Kwenye karatasi ya kupigia kura, picha ya Maduro ikatokea mara 13 idadi ya vyama vilivyomuunga mkono. Yani usipomuona kwenye kisanduku cha kwanza utakutana naye kwenye kisanduku cha pili, cha 3, hadi cha 13.
Vikawepo vyama vingine dhaifu ambavyo vilishiriki uchaguzi ili kuhalalisha ushindi wa Maduro. Wazee wa kutumika kama Chauma.
María Machado alipoona hivyo, akaamua kumshawishi Edmundo González arudi Venezuela na kugombea. Pamoja na hofu ya kukamatwa lakini akarudi. Maria akamuunga mkono González na kumfanyia kampeni.
Wananchi wakamwelewa González akapata uungwaji mkono mkubwa. Maduro akaona hii sasa balaa. Ikabidi abuni "mbwinu" za kulinda Urais wake.
Julai 28 siku ya uchaguzi mawakala wa González wakafukuzwa vituoni. Makada wa chama tawala PSUV wakavalishwa kiraia na kuzungushwa kwa mabasi kupiga kura zaidi ya kituo kimoja. Yani linakuja basi na abiria 60 wanashushwa kwa escort ya polisi, wanapiga kura, kisha wanasepa kwenda kupiga kura vituo vingine.
Upinzani ukalalamika lakini nani atawasikiliza wakati Hakimu ndiye Mlalamikiwa?
Wakati zoezi la kuhesabu kura na kujumuisha matokeo likiendelea, intaneti ikazimwa nchi nzima. Kesho yake (July 29) intaneti ikarudishwa na matokeo kutangazwa papo hapo. Watu wakajiuliza kura za nchi nzima zimewezaje kujumlishwa bila intaneti ndani ya siku moja tu?
Lakini pamoja na hujuma zote hizo Maduro akapata ushindi mwembamba wa 51% akifuatiwa na González 44%.
Waangalizi wa kimataifa (EU na The Carter Center) wakasema uchaguzi haukuwa huru wala wa haki. Hata hivyo malalamiko yote yakakosa nguvu kwa sababu Katiba ya Venezuela inazuia matokeo ya Rais kupingwa mahakamani.!
Britanicca