Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 308
- 1,354
Natamani sana watu wote tuwe kama Mandonga, si kuwa watu wa kushindwa ila kuwa na ile roho ya upambanaji. Mandonga anajiamini sana, ni mtu anayekuonyesha kwamba kila kitu kinawezekana! Hutakiwi kukata tamaa hata kabla ya kulifanya jambo fulani.
Nikimwangalia Mandonga, namuona mchizi fulani aliyekuwa amepigwa na maisha, akapigika sana mwisho akasema acha niingie kwenye ngumi, labda naweza kupata pesa fulani kuyaendesha maisha yangu. Akaingia humo.
Sasa kilichotokea, akapigwa mipambano hiyo lakini cha ajabu akaanza kuingiza pesa kupitia maneno yake na majigambo. Leo, Mandonga anapata pesa kuliko hata wale waliompiga, leo hii ana jina kubwa kuliko hata wale waliomtwanga, ni maisha tu yaani.
Tanzania imefika kipindi msongo wa mawazo unatutesa, hatuna furaha na mapenzi yanatutesa kila siku. Sasa anapotokea mtu akatufurahisha na kutuondolea msongo wa mawazo, huwa tunampenda sana. Tunamuhusudu mno na ndiyo maana tunasema tupo pamoja na Mandonga mpaka wamuue ulingoni.
Jamaa anatuburudisha sana, na burudani hizi zinamfanya kuvuna pesa kila siku. Leo anapopiga, anakuwa na maneno mengiiiii, akipigwa, anakuwa na maneno mengi pia.
Mandonga anajua kuongea, hata akifanya interview na kumsikiliza, unagundua kuna mtu yupo nyuma yake. Si kawaida kwa msela, mtu aliyekulia maisha ya kisela kuwa na uwezo wa kufanya interview kama yeye.
Makampuni yameanza kumiminika, K Security, Yanga, Silent Ocean na wengine wengi watamfuata, unajua kwa sababu gani? Ni kwa sababu ya uburudishaji wake tu.
Imefika hatua watu wana hamu ya kufuatilia pambano la Mandonga kuliko hata wapambaji wengine. Leo ukimuuliza mtu kati ya Mwakinyo na Mandonga, ungependa kuangalia pambano la nani? Mtu atakujibu Mandonga, kwa nini? Ni kwa sababu tunataka burudani ya maneno kwanza kabla ya pambano.
Nafurahi kumuona Mandonga akitengeneza noti kupitia maneno yake, mwili wake. Hakati tamaa, harudi nyuma. Tumchukue Mandonga na kumuingiza kwenye biashara zetu, hata tukifeli vipi, tuendelee kuwa na imani ya kufanikiwa siku moja.