Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Jana kwenye hotuba yake ya kulishukuru Bunge, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda alitoa changa moto ambayo alidai ndiyo yenye uwezekano mkubwa wa kumkomboa mkulima, mfugaji na mvuvi mdogo mdogo hapa nchini chini ya sera ya "Kilimo kwanza"...............
Alidai Bunge libuni mikakati ambayo itafanikisha azma hiyo ya kumletea mnyonge wa Tanzania maendeleo ya haraka haraka...........................
Hapo Mheshimiwa Pinda ndipo aliponiacha kwenye mataa.........maendeleo ya Mtanzania huyo ambaye anamwita ni mnyonge yataanza pale ambapo amewezeshwa kujichagulia viongozi wake mwenyewe bila ya kuingiliwa na dola...........................
Kwa hiyo kama Mheshimiwa Pinda ni mkweli ataanza kwa kufanyia kazi malalamiko ya Chadema ya kutaka uchaguzi wa Uraisi uchunguzwe na Tume huru ambayo itateuliwa na Bunge letu ili kujua kama kweli kulikuwa na tofauti kati ya kura za Uraisi zilizohesabiwa vituoni na zile ambazo NEC ilizitangaza.....................
Bila ya kufanya hivyo sera ya CCM ya kilimo kwanza itakuwa ni sera ya wakubwa tu kama tulivyoona kwenye matrekta ambapo tumejionea wanajeshi wa ngazi za juu ndiyo wamekumbatia tenda za kuuza matrekta bomu kwa wakulima...............
Matrekta hayo sasa hivi hayana wakuyatumia kwa sababu ni madogo na yameshindwa kuhimili vishindo vya kulima........Hivi sasa waliyoyanunua hawawezi kurudisha mapesa waliyokopa kutokana na mitaji hiyo kushindwa kulima na kuleta uzalishaji................................
Na ugumu hapo unakuwa ni vipi wananchi hao hao wataweza kuiondoa madarakani serikali hii ambayo yaelekea ipo mstari wa mbele kuwafurahisha wakubwa serikalini kulikoni mkulima, mfugaji au mvuvi huyu wamwitaye ni mdogo mdogo?
Kwenye uvuvi badala ya kumkamata mtengeneza na muuza nyavu ni mvuvi mdogo mdogo ndiye ananyang'anywa hata kila kidogo alichonacho.................Kweli kwa utani utani huu mnyonge wa nchi hii analo bao hapo?
Mheshimiwa Pinda acha unafiki na uwe mkweli....................