Kwenu wanaJF: Saint Anne ninawashukuru mno

Saint Anne

JF-Expert Member
Aug 19, 2018
35,409
2,000
Natumaini mnaendelea vizuri.

Nikiri msiba unauma jamani. Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea. Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama. Ameondoka usiku wa kuamkia tar29/5/2021. Taarifa ilinipa mshtuko mkali,hadi sasa mapigo yangu ya moyo hayaendi sawa. Mwendo ameumaliza,nina imani kabisa kwamba nitakutana naye Mbinguni.

Baba alipoanza kuugua,nilipokuwa nikiingia katika maombi,kila nikiomba uponyaji,nafsi ilinisukuma sana kuomba naye toba na pumziko Zuri. Nilikosa raha sana lakini Roho wa Mungu alikuwa ananisihi sana kulipokea hilo. Amepumzika.

Baba yangu alikuwa baba mzuri na mtu wa watu,licha ya mapungufu madogo ambayo kila mtu ana yake. Mwezi mmoja kabla hajaugua,alifanya usafi sana nyumbani(Nikiri mzee alikuwa smart sana hasa katika kuweka sawa mazingira ya nyumbani), akaacha ametengeneza bustani nzuri, akatuaga akatuambia anaenda kuhangaikia usafi wa mashamba..akiondoka atakaa muda mrefu bila kurudi. Kumbe alikuwa anatuaga.

Aliwahi kusema kwamba mwanangu nitakuhudumia hadi pale utakapomaliza mambo yako ya shule.
Kweli, alilitimiza hilo, hadi alipokamilisha,akasema sasa mwanangu nimemaliza kazi yangu.

•Shukurani kwa Mungu kwa ajili ya baba:

Namshukuru Mungu kwa ajili yake, kwa neema aliyompa Miaka yote 64 akiwa duniani, Alikuwa mtu wa kujishughulisha mno hasa kutafuta chakula shambani kwa ajili ya familia. Sijui maisha yatakuwaje ila naamini Mungu atafanya njia. Inaniwia ngumu kuamini kama kweli mzee hayupo ila ni kweli ameondoka. Jambo hili ni zito sana kwangu.

Nipo Kwenye depression nzito, sielewi nitatoka vipi. Anayeweza kunisaidia namna ya kuondokana na hili wimbi la mawazo naomba anisaidie. Kiufupi akili yangu nahisi haipo sawa kabisa. Mziwanda wa baba Mimi
Nyumbani ni pazito mno, usingizi hauji kabisa.

SHUKURANI ZANGU KWENU:
Kiukweli upendo mliouonyesha kwangu ndugu zangu ni upendo wa ajabu mno hadi nashangaa.
Natokwa na machozi ya huzuni lakini pia natokwa na machozi ya furaha kwa jinsi mlivyonionyesha upendo wa ajabu.

Namshukuru MUNGU sana kwa kunipa marafiki /ndugu wazuri sana namna hii ambao ni nyie. Kuna watu mmekuwa wazazi wangu, dada zangu, kaka zangu..yaani nawaona ni zaidi ya ndugu kwangu. Baba yangu hayupo ila ninaamini humu nitapata baba,nitapata wazazi,ninaamini mimi si yatima.

Baba yangu hayupo tena ila natiwa nguvu sana maana yupo MUNGU ambaye NI BABA YANGU. Amesema yeye ni baba wa yatima.

•Mungu awabariki wote ambao kwa namna moja ama nyingine,mmekuwa karibu na mimi kwa hali zote kunitia nguvu,kuniombea,kunifariji,kuniliwaza na kutoa michango yenu ya mali(rambirambi) kwangu. Yaani sina namna nzuri ya kushukuru zaidi ya kusema Asante.

•Napeleka shukrani zangu kwa dada yangu Heaven Sent. Mungu akubariki sana dada yangu Heaven Sent. Umefanyika kuwa faraja kwangu. Nilipopata msiba,mtu kwa kwanza kumuambia alikuwa ni huyu dada.
Amani ya moyo ilinituma nimwambie yeye. Ni dada ambaye kwa kweli nikimuona namtukuza Mungu maana ananitia moyo mno. Sina namna nzuri ya kumuelezea vile ninavyomuona ila itoshe kusema ni dada ambaye Mungu amenipa.

•Mungu akubariki kaka Mshana Jr kwa moyo wako wa upendo na kujali.

•Mungu akubariki rafiki yangu Karma ..nimefurahi kukuona na ninaona sipo mwenyewe,,nina rafiki anayejali.

•Mungu awabariki wote walionitia moyo kwa namna mbalimbali. Kuna walionitafuta PM,kuna walionitafuta kwa namba yangu ya simu,Kuna walionitia moyo hapa jukwaani..Kila nikisoma comments zenu natiwa moyo mno kwa faraja ninayopata. Natamani nitaje mmojammoja ila naona nitakesha ninataja.

•Nakosa namna nzuri ya kuwashukuru,itoshe kusema Mungu na awabariki mno. Ninaleta shukrani zangu hizi kwenu..ninaomba mzipokee.

Mapenzi ya Mungu lazima yatimizwe,haijalishi yatatuumiza ama yatatufurahisha. Bado Mungu atabaki kuwa Mungu na ninamuamini mno,hata kama hajajibu kwa kadiri ya mapenzi yangu.

1623132256963.png

Pia soma: TANZIA - MwanaJF Saint Anne, amefiwa na baba yake mzazi leo
 

Hank_31

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
492
1,000
Natumaini mnaendelea vizuri.


Nikiri msiba unauma jamani.
Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea..
Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba.

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama.
Mwendo ameumaliza,nina imani kabisa kwamba nitakutana naye Mbinguni.
Pole sana mwana JF mwenzetu naamini Mungu atakuvusha hapa kwa kukutia nguvu na faraja.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,098
2,000
Natumaini mnaendelea vizuri.


Nikiri msiba unauma jamani.
Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea..
Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba.

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama.
Mwendo ameumaliza,nina imani kabisa kwamba nitakutana naye Mbinguni.

Baba alipoanza kuugua,nilipokuwa nikiingia katika maombi,kila nikiomba uponyaji,nafsi ilinisukuma sana kuomba naye toba na
Pole sana
 

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
12,246
2,000
Poleee dia, msiba usikie kwa mwingine.mpaka namaliza kusoma machozi yanatoka, utakuwa na wakati ngumu, ukiwaza uko aliko yupo mwenyewe.

Kila mwenye mzazi hata mmoja wapo mwambie mama/baba nakupenda. Na usimalize siku mbili bila kuongea nae.pia kumuombea.
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
139,632
2,000
Hakuna njia ya mkato katika kuomboleza. Kwa sasa ukijisikia kulia lia. Tena lia kabisa bila woga. Na huwa tunasema kuwa muda ni tabibu mwema. Naam! Jipe muda. Endelea kusali. Omba faraja na mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Kwa sasa ni giza lakini kwa jinsi muda utakavyokuwa unapita, pole pole kutaanza kupambazuka na Mungu wako unayemwabudu hatakuacha. Japo pengo la mzee halitazibika kamwe lakini tabasamu litarejea tena katika uso wako, moyo huo unaouma utaanza kupona na maisha yataendelea. Dumisha mema yote aliyokufundisha baba yako; na kupitia kwako mzee huyo ataendelea kuishi.

Pole sana. Mungu Atakuinua tena
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,336
2,000
Time is a best healer,

Vitu vinapotukuta huwa tunaona kama tumeisha au dunia imeishia hapo ila muda hutufundisha kuishi na kumbukumbu zote pasipo kutuumiza kama mwanzoni..

Mungu akawe chanzo cha nguvu, faraja na uponyaji wako katika kipindi hiki kigumu saint Anne
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,730
2,000
Natumaini mnaendelea vizuri.


Nikiri msiba unauma jamani.
Yaani maumivu niliyonayo nashindwa namna ya kuyaelezea..
Nimempoteza mzazi wangu wakati ambao bado nilikuwa namuhitaji ,umri wangu bado ni mdogo kuweza kusimama bila baba.

Tumempumzisha tayari mzee wetu na amani ya moyo inaniambia amepumzika salama.
M

Pole sana Saint Anne! Inauma sana kumpoteza mzazi ila ni mapito ya hapa duniani cha muhimu ni kujikaza najua ni ngumu ila haina jinsi mzazi anauma sana. Waliosema msiba usikie kwa wengine ila usiwe kwako hawakuwa mbali kabisa na uhalisia yani it hits so hard ila tuko pamoja na wewe kama moja ya wanafamilia wa jf i pass my condolences for the loss!
 

Saint Anne

JF-Expert Member
Aug 19, 2018
35,409
2,000
Poleee dia, msiba usikie kwa mwingine.mpaka namaliza kusoma machozi yanatoka, utakuwa na wakati ngumu, ukiwaza uko aliko yupo mwenyewe.

Kila mwenye mzazi hata mmoja wapo mwambie mama/baba nakupenda. Na usimalize siku mbili bila kuongea nae.pia kumuombea.
Nilikaa siku nzima,
Japo nimuone baba,basi hata aseme neno,ila haikuwezekana.
Bado nahisi ni ndoto,nilimwita lakini hakunisikia tena
Jamani acheni kabisa

Sijawahi kulia maishani kama ninavyolia Sasa
IMG_20210531_100720_9.jpg
 

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,944
2,000
Pole ndugu, ila nikupe moyo tu usiwaze Sana kuhusu maisha bila ya baba, aliefanya wewe uwepo atajua utaendelea vipi, aliefanya baba yako kuwepo na wewe kutokea kwake na aliefanya baba yako asiwepo muda huu ndie huyo huyo atahakikisha haukwami.

Mimi nimeishi bila baba na mama tokea nikiwa chini ya mwezi mmoja na niliweza kuvuka na Leo nimesimama vipi ishindikane kwako? Tena wewe unaeamini?

Ombi langu Ni baba yako ajaliwe kukutana na Mungu wetu alietuumba bila ya Shari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom